Ukitaka kujibiwa kiuzoefu: wtt wanatofautiana katika makuzi, wakati mwengine unaweza kuwa na wtt 2,3 au zaidi lkn wakatofautiana kwenye muda wa kuanza kukaa, kutambaa, kusimama, kutembea na kuongea...vilevile unaweza ukawa na wtt 2,3 au zaidi na wakafanana kwa kila kitu kwenye makuzi yao.
Wengine wanasema ziwa la mama linachangia kwenye makuzi ya mtt, wengine kuwa na speed ya kufanya hivyo vitebdo na wengine kuwa wapo slow.
Ushauri wangu kama mzazi mzoefu ambae nimejaaliwa kupata wtt waliowahi kila kitu katika makuzi yao Alhamdulillah....vyema mtt umpeleke kwa wataalamu wa afya km alivosema mmoja wa members hapo juu, mpeleke kwa paediatrician au mtaalam wa masuala ya viungo pamoja na kumtafutia wale mabibi wataalam wa masuala ya wtt, wanakuwa wanawachuachua kuamsha nerves. Miezi 12 kutokutambaa kachelewa na hivyo unasema miguu yake haijishiki kuna shida mahali, either mgongo au kichwa.
Pole sana, Mungu Atakufanyia wepesi...na wewe wahi kumshughulikia mtt