Msaada: Mwanangu ana miezi 12 bado hajaanza kutambaa, yeye ni kukaa tu

Ukitaka kujibiwa kiuzoefu: wtt wanatofautiana katika makuzi, wakati mwengine unaweza kuwa na wtt 2,3 au zaidi lkn wakatofautiana kwenye muda wa kuanza kukaa, kutambaa, kusimama, kutembea na kuongea...vilevile unaweza ukawa na wtt 2,3 au zaidi na wakafanana kwa kila kitu kwenye makuzi yao.

Wengine wanasema ziwa la mama linachangia kwenye makuzi ya mtt, wengine kuwa na speed ya kufanya hivyo vitebdo na wengine kuwa wapo slow.

Ushauri wangu kama mzazi mzoefu ambae nimejaaliwa kupata wtt waliowahi kila kitu katika makuzi yao Alhamdulillah....vyema mtt umpeleke kwa wataalamu wa afya km alivosema mmoja wa members hapo juu, mpeleke kwa paediatrician au mtaalam wa masuala ya viungo pamoja na kumtafutia wale mabibi wataalam wa masuala ya wtt, wanakuwa wanawachuachua kuamsha nerves. Miezi 12 kutokutambaa kachelewa na hivyo unasema miguu yake haijishiki kuna shida mahali, either mgongo au kichwa.

Pole sana, Mungu Atakufanyia wepesi...na wewe wahi kumshughulikia mtt
 

Pole sana mkuu ,kama hana shida zozote kwenye brain basi atatambaa na kutembea inshallah.

Degedege mbaya sana kwa watoto ,jitahidi kujua joto la mtoto na kumkanda na kitambaa kabla ajapata degedege.
 
Relax mfanyishe mazoezi kidogo kidogo ku encourage vitu vya kuvutia. Mshike mkono pull like vile wanatembelea matako.
Kila siku zoezi moja au mbili kwa siku. Ndani ya mwezi mmoja naomba uje hapa kunishukuru.

Siku hizi watoto wanazaliwa na uvivu. Sijui ni haya maziwa tunawanunulia?
 
Well
 
Hahaha waswahili hao😅😅
 
Keep her active✌️
 
Anapata lishe mkuu, ila mama yake hanamaziwa yakutosha pia.
Je, anasimama kwa kutumia viti n.k? Kama ndiyo, basi usiwe na hofu yoyote wala usimharakishe. Watoto wengine ni waoga sana kutembea au huweza kuchelewa bila sababu yoyote. Nilikuwa na wangu alikuwa mwoga kweli kweli hata kusimama. Ila baadae akaja kutushangaza siku moja anatembea mwenyewe.
 
Miguu yake hajaweza kuikaza kwa kumnyanyua, na tulimpeleka kwa daktari akasema mbona hanashida ya miguu ila hawezi kuikazisha chini hata ukimnyanyua
1. Uwe unamfanyisha mazoezi na stretching ya viungo.
2. Asubuhi kabla ya jua kuwaka mtoe nje mtembeze peku kwenye bare soil sio tiles wala pavings blocks...natural healing ya soil. Sisi ni udongo
 
Nakazia kwenye hii, kila sku umpake olive oil. Mafuta ya nyonyo, epuka kumshika ukitoka kwenye mihangaiko. OGA kwanza. Mpeni lishe safi, maziwa ya ng'ombe ninmuhim, azingatie ratiba ya menu za mtoto kila siku. Amuwekee michezo mbalimbali lkn pia jiunge na hii app jisajili. Uwe unapata weekly update na uzizingatie. Ni kama kipimio Cha watoto wore wenye age hiyo. BabyCenter | The Most Accurate & Trustworthy Pregnancy & Parenting Information


Mwisho kabisa namuombea moto wetu kwa Allah ampe makuzi mema amiin
 
Shukrani mkuu😭
 
Sawa mkuu
 
Hajaweza bado kusimamia hivo vitu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…