Msaada: Mwanangu anatokwa na vipele vingi sana

Msaada: Mwanangu anatokwa na vipele vingi sana

Labda baada ya Bima kwa wote!! Mambo mengine muwe mnaangalia mazingira. Udaktari sio kukalili.

Just imagine mtoto anaumwa, mzazi kampeleka pharmacy ikashindikana kaja kuomba ushauri hapa we unamwambia ampeleke kwa dermatologist kwa pesa hipi??
Mkuu mimi nimeshauri kitaalam inavyopaswa kuwa kutokana na hii inafuatwa sana huku nilipo na mimi ni muumini wa procedure na patient satisfication, kupitia hilu nimeona manufaa yake sana.

Afya ni mtaji ukiona unapiga shortcut na kuona bima ni maumivu iwe chachu kuamka mpaze sauti msisubiri kina Lissu tu.

Huyo Ummy unafikiri akiumwa why anaenda nje kwa matibabu sababu ni mbili tu correct procedures na patient satisfication , hii ni haki kwa kila mtanzania sio hao wanasiasa uchwara wanaowadanganya.
 
Hili swali Nimetoka Kujiuliza Muda si mrefu Kwa nini Hii wiki Nimekutana na watoto wengi waliojawa na upele mwili mzima Nikajua Labda Ni kawaida tu au Joto La Dar Then Nakuja Hapa Naona uzi Unaohusu Upele.Mtaani Kwangu Watoto wengi sana wamejawa na Upele Karibia Mwili Mzima Ila Usibweteke Kutafuta Tiba Huenda ni suala Tofauti
Kweli mkuu aweke picha kwanza
 
Labda baada ya Bima kwa wote!! Mambo mengine muwe mnaangalia mazingira. Udaktari sio kukalili.

Just imagine mtoto anaumwa, mzazi kampeleka pharmacy ikashindikana kaja kuomba ushauri hapa we unamwambia ampeleke kwa dermatologist kwa pesa hipi??
Kwahiyo pharmacy ndiko wanakotibiwa wagonjwa? Mbona mm naona ww ndio unakalili?
 
Nisome tena!! Mzazi kumpeleka mtoto pharmacy it means hana huwezo wa kumpeleka hospital!! Au hauna watoto??
Ni wapi ameandika hana uwezo wa kumpeleka mtoto hospital? Hayo mazoea ya kwenda pharmacy bila kumuona Dr mwenzenu juzi kati kakatwa kiganja Cha mkono baada ya mkono kuoza kisa kuchomwa sindano ya UTI pharmacy.
 
Hii Daaah ni changamoto kubwa sana ndani ya kitaa na familia.kuna hadi watoto wa chini ya mwaka mmoja
 
Ni wapi ameandika hana uwezo wa kumpeleka mtoto hospital? Hayo mazoea ya kwenda pharmacy bila kumuona Dr mwenzenu juzi kati kakatwa kiganja Cha mkono baada ya mkono kuoza kisa kuchomwa sindano ya UTI pharmacy.
Duh!...hizo sindano wanachomaga mkononi ?
 
Ni wapi ameandika hana uwezo wa kumpeleka mtoto hospital? Hayo mazoea ya kwenda pharmacy bila kumuona Dr mwenzenu juzi kati kakatwa kiganja Cha mkono baada ya mkono kuoza kisa kuchomwa sindano ya UTI pharmacy.
Sawa umeshinda Dr
 
Ana miaka miwili . Huo ni mgongo tu anajikuna sana. Na hospital nimeenda labda nibadili hospital
IMG_20231230_185147_4.jpg
 
Kwahiyo pharmacy ndiko wanakotibiwa wagonjwa? Mbona mm naona ww ndio unakalili?
Nilichogundua Tanzania kuna tatizo sana kubwa la viongozi ambao ni mediocre na ndio linakuja kuwaumiza wananchi huku wao wakienda kutibiwa nje.

Imagine hapo tu red skin patches zinamfanya mtu afanye hitimisho ni scabies.

Je huyo mtoto kama ana serious autoimmune disease kama systemic lupus atajuaje bila kuchukua sampuli muhimu kama nilivyoshauri.

Wakuu narudia tena afya ni mtaji ila naona kwa Tanzania viongozi wenu hawajali how on earth viongozi wasitibiwe ndani kama nyinyi waje kutibiwa nje?

Huyo waziri niliwahi kumuuliza kwenye ukurasa wake wa X kuwa anipe record zake za kimatibabu walu miezi 6 iliyopita katika hospitali za umma iliyopita tu details muhimu kuhusu ugonjwa ,vipimo na dawa kama alipata aache jina la hospitali na jina lake yeye hajawahi kuleta hadi leo.

Hapo mmepata picha gani, mimi nilikua na majibu tayari waziri anawahadaa wananchi huku yeye anatibiwa first class hospitals na sometimes anaweza kuwa anapewa huduma ya mobile clinic toka kwa super specialist simply because anatumia pesa za wananchi kujikatia bima katika vifurushi ghali zaidi ambavyo watanzania wote walistahili kupata kupitia universal health coverage.
 
Nisome tena!! Mzazi kumpeleka mtoto pharmacy it means hana huwezo wa kumpeleka hospital!! Au hauna watoto??
Kipindi nampeleka pharmacy, hapo nyuma (mwezi wa 11) niliwai mpeleka hospital kama 2 tofauti walimpa (sonadem) nilimpaka kwa wiki mbili mfululizo havikuisha na wengi walinambia ni vipele vya joto , vitaisha lakini havikuisha nikaona vinazidi,
Kuna pharmacy nilielekezwa nikampeleka ,ndipo akanishauri nitumie hiyo Calamine lotion lakini hola, nikaona nimrudishe hospital, awamu hii wakanibadilishia dawa wakanipa silverex ,tangu nimpake hakuna mabadiliko.
 
Habari Wana JF
Naomba msaada Mwanangu anatokwa na vipele vingi sana na vinazidi kuenea mwili mzima (vidogo vidogo) mpaka anakuwa mwekundu kwa kujikuna mara kwa mara.
Nilienda pharmacy walinipa Calamine lotion nikawa nampaka lakini bado ,nilienda hospital walimpima mchafuko wa damu , lakini damu iko safi na walinipa silverex ambayo nimetumia kwa wiki sasa lakini bado pia.
Naomba msaada
Usiwe mchoyo jombaa kwa mwanao Share naye ARVs zako
 
Back
Top Bottom