Msaada: Mwanangu anatokwa na vipele vingi sana

Msaada: Mwanangu anatokwa na vipele vingi sana

Chief, nina mtoto ana shida kama hii ya mtoa mada.
Sijaelewa vyema haya maelekezo. Inahitajika Ivermectin syrup au tabs?
Ana umri gani?
Ivermectin syrup Nyingi Ni mchanganyiko na Albendazole hivyo kukua umri wa mtoto ni muhimu sana
 
Mm sio daktari
Ila fata ushauri..utakuja kunishkuru hapa jukwaani

Hakuna dawa ya scabies kama scaboma

Iko ya lotion na cream..nunua lotion
Mpake mara moja tu na umpake akiwa hajaoga
Yaani ameshacheza ndio umpake

Inauzwa elf 12 tu..inatoka malaysia

Usimpake zaidi ya mara moja ataendelea kuwashwa ila siku ya pili vitakau vyote....

Usimpake mara nyingi maana inaingia kwenye mishipa ya damu plus inaenda kwenye figo na ini
Fua nguo zake zote
 
Ukipata Syrup sio mbaya na akipata Tabs pia sio mbaya ila zingatia Uzito..
200mcg/kg
Hizo dawa zinapatikana kwenye Pharmacy zetu za kawaida mkongwe?
Maana unaweza ukaenda Pharmacy, muhudumu akakujibu haijui na wala hajawahi kuiona dawa unayohitaji.
 
Mm sio daktari
Ila fata ushauri..utakuja kunishkuru hapa jukwaani

Hakuna dawa ya scabies kama scaboma

Iko ya lotion na cream..nunua lotion
Mpake mara moja tu na umpake akiwa hajaoga
Yaani ameshacheza ndio umpake

Inauzwa elf 12 tu..inatoka malaysia

Usimpake zaidi ya mara moja ataendelea kuwashwa ila siku ya pili vitakau vyote....

Usimpake mara nyingi maana inaingia kwenye mishipa ya damu plus inaenda kwenye figo na ini
Fua nguo zake zote
Reseach nyingi zimefanyika Hivi karibuni Lindane (Scaboma), imefail mara kadhaa kutibu kuliko BBE na permethrin imayoongoza ni BBE inakuja Permethrin ya mwisho ni Lindane..

So inaweza kuwa Dawa nzuri (Scaboma) ila sio kwa watu wote..Ila BBE ni universal
 
Zipo mkuu!
Sawa chief. Maana kuna mtu alinishauri nitafute dawa inayoitwa Permethrin, hauwezi amini. Nimezurura Kibaha nzima kutafuta hiyo dawa sijaipata, nilimuagiza mtu Kariakoo, alivyoingia Pharmacy kuulizia, mhudumu alimjibu hajawahi kuiona hiyo dawa maisha yake yote.
 
Toka mwaka jana bado anapokea ushauri wa ndipo aende hospital. Nchi hii dah
 
Reseach nyingi zimefanyika Hivi karibuni Lindane (Scaboma), imefail mara kadhaa kutibu kuliko BBE na permethrin imayoongoza ni BBE inakuja Permethrin ya mwisho ni Lindane..
Hata mimi nimetumia Scaboma kwa mtoto wangu haijamsaidia.
Hiyo BBE nahofia kuitumia kwasababu mtoto ana vidonda baadhi ya maeneo aliyoathirika na ugonjwa, amejikuna mpaka ametoka vidonda.
 
Sawa chief. Maana kuna mtu alinishauri nitafute dawa inayoitwa Permethrin, hauwezi amini. Nimezurura Kibaha nzima kutafuta hiyo dawa sijaipata, nilimuagiza mtu Kariakoo, alivyoingia Pharmacy kuulizia, mhudumu alimjibu hajawahi kuiona hiyo dawa maisha yake yote.
Permethrin ni Nzuri sana na haina Maumivu sana kama BBE..
Zipo sehemu unajua watu siku hizi Wanatumia Sana Trade name badala ya GENERIC ones.(Majina halisi ya Dawa)...
Permethrin Ina majina mengi sana pharmacy.

Kama Acticin , Elimite, Scabwell, Scabfree, lotrix cream,Nix cream, Malin cream N.k..
 
Habari Wana JF,

Naomba msaada Mwanangu anatokwa na vipele vingi sana na vinazidi kuenea mwili mzima (vidogo vidogo) mpaka anakuwa mwekundu kwa kujikuna mara kwa mara.

Nilienda pharmacy walinipa Calamine lotion nikawa nampaka lakini bado ,nilienda hospital walimpima mchafuko wa damu , lakini damu iko safi na walinipa silverex ambayo nimetumia kwa wiki sasa lakini bado pia.

Naomba msaada
Jaribu SKIDERM CREAM Ina dawa tatu antibacterial, antifungal na whitening agent ikikataa hii wahi hospital
 
Kipindi nampeleka pharmacy, hapo nyuma (mwezi wa 11) niliwai mpeleka hospital kama 2 tofauti walimpa (sonadem) nilimpaka kwa wiki mbili mfululizo havikuisha na wengi walinambia ni vipele vya joto , vitaisha lakini havikuisha nikaona vinazidi,
Kuna pharmacy nilielekezwa nikampeleka ,ndipo akanishauri nitumie hiyo Calamine lotion lakini hola, nikaona nimrudishe hospital, awamu hii wakanibadilishia dawa wakanipa silverex ,tangu nimpake hakuna mabadiliko.
Inawezekana mwanao aliumizwa na chanjo.
 
Nilichogundua Tanzania kuna tatizo sana kubwa la viongozi ambao ni mediocre na ndio linakuja kuwaumiza wananchi huku wao wakienda kutibiwa nje.

Imagine hapo tu red skin patches zinamfanya mtu afanye hitimisho ni scabies.

Je huyo mtoto kama ana serious autoimmune disease kama systemic lupus atajuaje bila kuchukua sampuli muhimu kama nilivyoshauri.

Wakuu narudia tena afya ni mtaji ila naona kwa Tanzania viongozi wenu hawajali how on earth viongozi wasitibiwe ndani kama nyinyi waje kutibiwa nje?

Huyo waziri niliwahi kumuuliza kwenye ukurasa wake wa X kuwa anipe record zake za kimatibabu walu miezi 6 iliyopita katika hospitali za umma iliyopita tu details muhimu kuhusu ugonjwa ,vipimo na dawa kama alipata aache jina la hospitali na jina lake yeye hajawahi kuleta hadi leo.

Hapo mmepata picha gani, mimi nilikua na majibu tayari waziri anawahadaa wananchi huku yeye anatibiwa first class hospitals na sometimes anaweza kuwa anapewa huduma ya mobile clinic toka kwa super specialist simply because anatumia pesa za wananchi kujikatia bima katika vifurushi ghali zaidi ambavyo watanzania wote walistahili kupata kupitia universal health coverage.
Uko sahihi, inaweza kuwa ni autoimmune issue ambayo huwa inasababishwa na chanjo za mkupuo (the elephant in the room) wanazochomwa watoto. Hizi chanjo zinaharibu ufanisi wa mwili katika kiwango cha seli. Nimeona hapa DR Mambo Jambo ameongelea ivermectin, hii dawa huwa inasaidia mwili kuondoa haraka seli zilizoharibika (apoptosis) na kuuwezesha mwili kufanya kazi vizuri.
 
Uwe unamtoa mtoto NJE apate mwanga wa jua wakati wa asubuhi jua likichomoza Hadi saa 3 asubuhi na jioni. Mvalishe nguo za wazi. Kama anatumia uji basi tumia mafuta ya asili kwenye chakula mf. Ufuta n.k pia usimpe vitu vya sukari badala yake mpe asali na tende. Pendelea kumpa matunda mchanganyiko ila machungwa ni MUHIMU inasaidia kukausha. Mungu hakupe nguvu wewe na mtoto. Asante
 
Husimpake Mtoto mafuta yeyote,
Muogeshe hata mara Nne Kwa siku na sabuni hisiyona manukato kama sabuni za miche kama Jamaa
Mchana Mtoto mvalishe chupi Pekee kote awe uchi.
Jitahidi Mtoto hasikae kwenye Jua Kali, wala mahali penye Joto.
Mishe Mtoto Vyakula venye Lishe ya asili kama ulezi Wa kutengeneza mwenyewe, Mbogamboga na matunda.
Jitahidi awe anakunywa maji mengi.
Mengine mwachie Mungu.. Ugonjwa utaona taratibu taratibu na mwili utajitengenezea Kinga dhabiti ya kupambana na Hilo Tatizo.

Kwa Waganga husiende ila kwenye majumba ya Ibada nenda. Na maombezi udhuria Ila mambo ya mafuta na maji ya upako achana nayo.
 
Back
Top Bottom