Msaada: Mwanaume ninayeishi naye haoneshi kunipenda na hataki tuachane

Msaada: Mwanaume ninayeishi naye haoneshi kunipenda na hataki tuachane

I hope mko poa guys

Naitaji ushauri hapa serious kabisa

Mimi ni mwanamke nina miaka 30 nina mchumba ambaye wazazi walishatupa ruhusa ya kuishi pamoja

Mwaka 2016 nilipata kazi ya muda mfupi katika kampuni fulani nilifanya kazi ndani ya miezi minne nilikutana na kaka ana 33 kwa a

Huyu Kaka nilimpenda sana alikuwa mtu fulan mpole hana Mambo ya ajabu ukweli nilitokea tu kuvutiwa nae. Nikafanya juhudi tukawa marafiki wa karibu, kusaidiana mambo mbalimbali haikupita muda tukawa tumeanza mahusiano ya kimapenzi

Uzuri jamaa alikuwa hayupo katika mahusiano serious, alikua na mwanamke ambae walikua hawafahamiani aliunganishiwa na jamaa tu so wakawa na mapenzi ya kwenye simu

Baada ya miezi 6 jamaa akanipeleka kwao kunitambulisha ilikua Desemba mwaka jana, Februaru mwaka huu alihamishwa mkoa mwingine kikazi nami nikaacha pale nikaanza biashara zangu binafsi. March akaja nyumbani kwetu kujitambulisha, Juni kupanga na kutoa mahari.

Oktoba Wazazi pande zote mbili walikutana kupanga mambo ya ndoa, wazazi wake wakaomba tuchukuane tu kwa sasa hawana uwezo tutafunga ndoa mwaka kesho. Hii ni sawa kwa jamii ya wasukuma wa kijijin kwani huamini ukishamtolea mahari mwanamke tayari wanakuja kumchukua. Familia yangu ikakubali

Kilichonileta kwenu

Baada ya kukaa kiuchumba na jamaa nilikua nahisi hanipendi tangu kabla hajanipeleka kwao nikawa najiondoa kwake ajabu nikikaa nae nikimwambia tuachane hakubali kabisa anaweza hata jitupa chini akibembeleza nisimuache

Nikimuangalia ni mtu ambae haoneshi kama ananipenda anaweza kaa siku 1 au 2 bila kunipigia. Ninaweza pata shida kunisaidia akawa mzito mno. Ni mtu ambaye hajali unaumwa, umepata matatizo unaishi vipi haelewi

Mwanzo nilihisi labda anamahusiano mengine lakini nilifanya uchunguzi sikubaini hicho. Mi nampenda najikuta naumia nahitaji kupata attention yake, muda wake, nilishaongea nae sana. Ni mtu ambae hata kuniambia nakupenda au nimekumiss au kuniita tu mpenzi wangu ni ngumu labda muwe kitandani kapandwa na hisia anaweza fanya hivyo au muwe mna ugomvi anakubembeleza au ndio mmeelewana

Atafanya hivyo for 2 days then anarudi katika hali yake

Nilishaongea nae kama hanipendi nimeshamuomba aniache niumie badae nitazoea hataki. Kuna kipindi nilimwambia aniache tu atafute mwanamke anaempenda na nikamchunia kweli

Aliteseka sana alinitafutia washauri sio ndugu zake, rafiki zake na zangu. Nashindwa kuelewa nitaishije na huyu mtu jamani. Sielewi ni maumbile yake yuko hivi, makuzi au tu hanipendi!

Amekulia kijijini hasa tena hasa nashindwa kuelewa labda ndivyo alivyo. Nawaza labda yupo kwangu kimaisha tu sababu yeye ana kazi nzuri mshahara mkubwa lakini familia ya kwao inamuelemea ukoo mzima unamtegemea yeye

Mimi kipato changu kidogo kwake lakini nina maendeleo kidogo namzidi na ninafanya vitu vya msingi. Nahisi labda jamaa amefata maisha!

Wadau samahani kwa kuwachosha naombeni mawazo yenu
Hapo uliposema kakulia kijijini tena sana,ndo nmepata jibu la swali lako, huo ni ushamba unamsumbua tuu wala sio kingne...tafuta marafk wa kiume wa kwake wambie shda yako then wamshaur
 
Pale unapojiita lady in action but unashindwa kushuka mzima mzima na mtu anayeichezea future yako. Anyway

Ninakukumbusha tu, at 30s huna muda wa kuchezea tena.
 
Mbona kama unausemea moyo...huyo jamaa dada angu hakupend..

Naongea kutokana na experience,nna madem wa3,simpend hata m1,..na jins alivyo huyo jamaa ndo nahia namim hao madem zangu wananiona hvyo...

Nnaempenda mmi tuliachana 6yrs ago,sjapataga naempenda tena..mim ni kula na kuacha,

Perhaps,niliepangiwa bdo hajatokea
 
Huyo Kama mimi. Kwa kifupi ni nature yake. Mimi huwa ananilalamikia mke wangu Kama wewe hivyo unavyoeleza. Kiukweri ninampenda , namhitaji name Sina michepuko But nipo baridi Sana jambo la kukushauri ni kwamba Huyo mmeo anakuhitaji zaidi wewe uwe active kwenye mahusiano Sana kuliko wewe unavyomhitaji yeye awe. Na anaponilalamimia huwa najihisi Kama mke wangu ni too demanding Kwa vitu vidogo vidogo visivyo vya msingi. But Naoma Tofauti yangu na mmeo ni kuhudumia family Hapa nipo very responsible.
Wanawake wasumbufu tu muda mwingi.

Sasa anataka kilq muda umwambie unampenda ili iweje wakati hadi unaamua kumwoa ni dhahiri unampenda.

-Kama anaumwa ukishamwambia meza dawa na ukamletea dawa..visimu vya kumpigia vya nini?

Usumbufu tu mkuu.
 
Pole sana.

Nachelea kusema anakupenda. Ukiwa na upendo utamjali mwenzako kwa hali na mali. Nashanga sana hataki kukusaidia wakati unaumwa pia unapohitaji halafu ni mchumba nashindwa kuamini hilo sasa anaona kama unamchuna ama vipi
 
Wanawake wasumbufu tu muda mwingi.

Sasa anataka kilq muda umwambie unampenda ili iweje wakati hadi unaamua kumwoa ni dhahiri unampenda.

-Kama anaumwa ukishamwambia meza dawa na ukamletea dawa..visimu vya kumpigia vya nini?

Usumbufu tu mkuu.
Masai unayosema ni sahihi.

Mtu anaumwa huendi hospital kumwona wala kumpa hela ya dawa. Aise upendo wa siku hizi wakuvamiana vamiana
 
Hyo hutokea kama mtu hajaweka mapenz sana kipaumbele
 
Huyo anakup3nda kabisa anaoneka,Ile elewa tu wanaume tuko tofauti sana
 
nilipoona huu uzi nilidhani wife kaja kunisemelea humu nikakumbuka yeye na jamii forum vitu 2 tofauti,sis kiufupi ni tabia za mtu mwenyewe mke wangu sometime huwa hadi anajifanyisha kama anaumwa ili anione nita chukulia vipi but huwa nashindwa kabisa.vitu vingine sio rahisi kuvirekebisha sio kila mtu ameumbwa kuwa romantic.
ila huyo wa kwako amizidi kama hajali familia hiyo ni case nyingine
 
Vumilianeni tu pengine hata wewe unamapungufu flani anayavumilia, jitad kumshape vimsg vya mahaba muda mwingine usisubir akuanze
 
Wanawake wasumbufu tu muda mwingi.

Sasa anataka kilq muda umwambie unampenda ili iweje wakati hadi unaamua kumwoa ni dhahiri unampenda.

-Kama anaumwa ukishamwambia meza dawa na ukamletea dawa..visimu vya kumpigia vya nini?

Usumbufu tu mkuu.
Yaani mpenzi wako amelazwa unashindwa kuwa karibu yake eti wanawake ni wasumbufu kweli?

Kwahili wanaume mnakosea, mkumbuke tu kuwa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. Kama unashindwa kumjali mwenza wako katika wakati mgumu tambua kuwa huna mapenzi naye.
 
Back
Top Bottom