Msaada mwenye connection ya ajira nchi za Kiarabu

Msaada mwenye connection ya ajira nchi za Kiarabu

Nimekaa nikafikilia maisha yamenipiga, kazi niliyokuwa nayo haikidhi kabisa mahitaji yangu ya kila siku, nina mke, nina mtoto, ninao ndugu wanao nitegemea, baba, mama na wadogo zangu mbaya zaidi mimi ndie kaka mkubwa wa familia, najiona kabisa nimeanguka, najiona napoteza uelekeo kila kukicha, nimekuja humu najua kuna watu wa hadhi na kariba tofauti tofauti, maana waswahili husema "mficha maradhi kifo humuumbua"

Nimehangaika kutafuta kazi, ni kweli nipo kwenye kazi ambayo mshahala ni 250k baada ya makato, huo mshahala unanifanya niishi kwa madeni hata kabla sijaupokea unakuwa teyari umeshaisha, sasa ndugu zangu kwa umri wangu huu 25+ najiona kabisa ndoto zangu hazitotimia, nikiwa na akili timamu ninaomba kwa yeyote mwenye connection ya ajira, ata ya ULinzi, na nyinginezo kwenye nchi za kiarabu haswa Doha, Qatar anisaidie pengine huko maslahi yanaweza kuongezeka.

Nimejaribu kufuatilia kwenye mitandao nakutana na maagency ambao wapo nchi za jirani inakuwa ngumu kwangu kuwafikia kwani wengi wao wapo Kenya ama Uganda.

Ndugu zanguni ni matumaini yangu kilio changu kiapatiwa ufumbuzi.

Elimu yangu ni ya kidato cha nne, sijasoma kihivyo ila ujinga wa kuelewa kingereza kidogo nimeuondoa hivyo ninaweza kingereza japo si sana.

VILE VILE mimi ni dereva wa magari...mwenye leseni yenye daraja A, A2, B, C1, C2, C3, D, E


Doha ni nchi gan Mkuu
 
Kiongozi mimi passport ninayo, na mkwanja unaweza kupatikana. Hizo picha mbili siyo issue. Yellow fever card kama mchongo wa uhakika itapatikana.

Mkuu kila kitu naweza kukipata, nahitaji connection ya hao madalali. Hata kenya naweza kufika maana mara nyingi sana huwa naenda sirari, so kuvuka siyo issue.
Hiyo yellow fever card siyo kikwazo kwako. Tambua umeshapata sasa wew songa mbele
 
Baada ya kufatilia sana, kuna kitu nimegundua. Makampuni mengi nchi za kiarabu wanaprefer zaidi wakenya kuliko watz.

Kuna agent wa Kenya ananishughulikia issue yangu, siku ya kwanza tu aliniuliza kuhusu passport yangu ni ya nchi gani, baada ya kumwambia ni ya bongo akasema nimtumie. Ni miezi sasa imepita but kila nikiongea nae anasema bado hajafanikisha kwani passport ndio kikwazo japo kanihakikishia kuwa ni 100% kupatikana kwa kazi.


Kwahiyo ndugu zangu, kama bado hujapata passport fanya mchakato upate ya Kenya. Kuna watu nikisema passport ya bongo au ya kenya hawaelewi, paasport ni ile ile but ombea kenya uwe kama mkenya. Ni rahisi sana kupata mchongo uarabuni ukiwa raia wa kenya
 
Vipi kuhusu iraq ulifatilia maisha yao yapoje na Maisha kiujumla
huko sijafuatilia...nilichogundua ni kuwa nchi za kiarabu zinamalipo mazuri...ila ni kujitoa muhanga nchi hizo zina joto kali kupita kiasi
 
Nimejifunza mambo mengi Sana ktk huu uzi Mkuu.. sina mpango wa kwenda kuishi nje ya nchi ila huu uzi ukiugeuzageuza ni darasa tosha.
kweli kaka...ila hapa duniani kuna viumbe vinataabika sana...nilitaabika nikaja na wazo la kuikimbia nchi yangu ndo kama hivyo unavyoona bado nipo darasani najifunza...na mimi mtoa mada najifunza kupitia uzi huu
 
Back
Top Bottom