Nimependa huu mjadala. Mimi pia mmoja wa watafuta ajira hasa Dubai. Dubai kwa sababu girlfriend yupo huko. Nimeanza kutafuta connection 2019. Agent wengi Bongo nishaongea nao. Hela watataja ni kubwa sana 1000 USD. Kuna mmoja nilimpata akapunguza ikawa 800 USD. Nilikubali akaanza process matokeo yake aliniibia Tsh 50,000/= aliniomba kwa ajili ya kuombea vibali Zanzibar sababu aliniambia lazima upitie Zanzibar kwa urahisi zaidi.
Yupo pia urgent wa Kenya huyo sio tapeli nimekuwa nikiwasiliane naye tangu 2019 kipindi Corona imepamba moto. Akawa anasema kwa sasa hakuna kazi. 2021 akapata urgent akasema nilipie 150k +15k kitu kama hicho msg ninazo.
Nimekuwa nijifunza sana kwa namna gani naweza kupata kazi na kufanya kazi huko Dubai hasa ya security sababu nilipata habari toka kwa girlfriend wangu kuwa kazi ya security dubai haitesi sana kama kazi zingine za helps.
Sasa kuna rafiki yangu kaniunganisha kwa rafiki yake ambaye atanipokea huko Dubai. Natafuta nauli mpaka Aprili nitakuwa dubai.
Vitu alivyoniambia muhimu kupata kazi ya security dubai
1. Passport travel
2. Passport size
3. cv one page
4. SIRA hii ni leseni unasoma huko Drm 1730
5. Uzoefu muhimu pia
6. Police clearance report utoke nayo huku
7. Medical clearance report utoke nayo
8. Hela ya mtumizi
Niongea kifupi kidogo. Ahsante