Msaada: Nahisi mdogo wetu wa kike kaongopa kuwa yupo field ila nahisi huenda kafungiwa na Mwanaume huko mkoani

Msaada: Nahisi mdogo wetu wa kike kaongopa kuwa yupo field ila nahisi huenda kafungiwa na Mwanaume huko mkoani

Kama kuna mwanafunzi anayesoma Chuo cha Mipango Dodoma ama mtumishi wa hicho chuo ama mzazi mwenye mtoto anayesoma hapo naomba anithibitishie hili kuna mdogo wetu namlipia ada katika chuo taja hapo juu kozi ya “Bachelor Degree in Human Resource Planning and Management (BDHRPM).

Sasa jumamosi hii nilikuwa katika huo mji mkuu wa serikali nikasema nimpigie simu ili nipate kumkaribisha mahali apate chakula cha mchana na jioni kupokea hakutaka ila akanitext kwamba ana emergence kasafiri kaenda wilaya ya jirani kwa field? na sehemu alipo hakuna network nzuri bora tuwasiliane kwa text.

Alivyotaja FIELD akili yangu ikagutuka kidogo maana miaka yetu field huwa tunafanya mwishoni mwa semester, kengele ikanijia kichwani huwenda huyu mdogo wetu ndio keshaanza kuitembea Tanzania na viunga vyake akiwa hapa dodoma pamoja na wabab wa watu.

Na isitoshe huyu mdogo wetu tunatumia gharama nyingi kumsomesha kwa kweli hata ile morali ya kujiachia nikiwa dodoma ikapotea maana nilikuwa na mawazo mengi kichwani moja wapo ni kuwa huwenda kuna kibaba cha mtu kimemsafirisha mkoani ukitegemea wiki ilikuwa na likizo ndefu kidogo takribani siku nne kupisha sikukuu ya pasaka.

Hivyo nimekuja humu ndani kupata ukweli, hasa ukitegemea JF imesheheni watu wa aina mbalimbali na katika nyaja tofouti tofouti huwenda wakawa na ABC,s kuhusiana na hiki chuo ni kweli hawa wanafunzi wa mipango wameanza field katikati ya masomo, ama huyu mdogo wetu ameamua kunidanganya kuficha uchafu anaofanya pindi akiwa chuo kwa kutoroka vipindi kwenda kufanya maovu mikoani huko.

Naomba nipate ukweli kama kweli wameanza ratiba ama laah.
Kujifanya Una wivu wakati unachepuka kwa Siri huo nao ni Uchawi[emoji846][emoji23][emoji113]
 
Ulikuwa dodoma,ulishindwa nini kufika chuoni na kuupata ukweli?
Ulishasema ni likizo mbona tena unasema anadoji vipindi
Kinachokuumiza sio kusoma ila ni mawazo ya kuliwa kwa sista ako,je yule ni mtoto unamchunga(ungekaa naye kwako)
Mwisho
Jifunze kupotezea mengine sio kila kitu akupe taarifa,japo haijakaa poa lakini jitahd i kuyapotezea
N.B miaka ya 2015 UDOM sina kumbukumbu sana wanachuo walienda kujirusha mwanza bahati mbaya wakapata ajali,kiukweli haikuwa nzuri kwa wazazi maana mzazi anajua mtoto yupo dodoma ila taarifa za kifo zinatokea mwanza
Ila mkuu usinipopoe kweli inauma jamani
From the way ameandika sidhani kama ni kaka mtu bali a jealous boyfriend as angekuwa kweli ni kaka mtu asingekazia hivyoo issue ya kuhisi huyo binti aliwa.
 
Mkuu achaa kimfatilia mdogo wako wa kikeee....ameshakuwa,kumlipia ada isiwee sababu ya kimchungaa.mbona wewe unagongaa dada wa wezako
 
Anasoma Chuo Gani Hapo Dodoma, Mipango, CBE, UDOM, IFM, ST John,DECCA
Ili Kusaidie Yupo Wilayani Ama Kongwa, Mpwapwa, Chemba, Kondoa, Bahi, Chamwino

Dodoma Nako Sasa
 
Ulikuwa dodoma,ulishindwa nini kufika chuoni na kuupata ukweli?
Ulishasema ni likizo mbona tena unasema anadoji vipindi
Kinachokuumiza sio kusoma ila ni mawazo ya kuliwa kwa sista ako,je yule ni mtoto unamchunga(ungekaa naye kwako)
Mwisho
Jifunze kupotezea mengine sio kila kitu akupe taarifa,japo haijakaa poa lakini jitahd i kuyapotezea
N.B miaka ya 2015 UDOM sina kumbukumbu sana wanachuo walienda kujirusha mwanza bahati mbaya wakapata ajali,kiukweli haikuwa nzuri kwa wazazi maana mzazi anajua mtoto yupo dodoma ila taarifa za kifo zinatokea mwanza
Ila mkuu usinipopoe kweli inauma jamani
Aisee kumbe wewe mkongwe...Mmoja ya hao namfahamu ni rafiki Yangu sana.Hiyo ajali ilikuwa mbaya sana yani
 
Kumfuatilia mtoto wa kike,mimi nilishindwa zamani sana...hao jamaa ni pasua kichwa!
 
From the way ameandika sidhani kama ni kaka mtu bali a jealous boyfriend as angekuwa kweli ni kaka mtu asingekazia hivyoo issue ya kuhisi huyo binti aliwa.
Mkuu emu kuwa serious kidogo,a jealous boyfriend?nimeshindwa kuvumilia imagine mleta uzi akiona hii comment
 
Back
Top Bottom