MSAADA: Nakojoa kitandani licha ya kuoa

MSAADA: Nakojoa kitandani licha ya kuoa

lelulelu

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2017
Posts
444
Reaction score
400
Habari z muda kaka na dada zangu wote wa humu jukwaani. Wakuu nimekuja na shida mficha uchi hazai hata kidogo.

Mimi ni mtu mzima 27 yrs nimeoa na mtoto hadi leo bado nakojoa kitandani inauma sana, mke wangu ananivumilia na kunipa moyo sana.

Nikikojoa huwa naota ndoto nzito halafu kwemye ndoto najiuliza kama naota au live, kisha najiridhisha ndotoni kwamba hapa sioti halafu nakojoa mkojo karibia kuumaliza wote kitandani bila kushtuka.

Lakini HII HALI HUNITOKEA MARA MOJA MOJA PENGINE NAKAA MIEZI SITA,AU MITATU NDO HUTOKEA MARA MOJA.

Inaninyima raha sana mimi nikienda ugenini siwi huru, naweza nikakataa kunywa maji saa 10 jioni ili nikwepe fedheha.

Natamani kuvaa condom nikienda ugenini ili nikikojoa mkojo usifike kwenye godoro.

WAKUU NAOMBENI MSAADA WENU TAFADHALI, NAZIDI KUWA MKUBWA SITAKI AIBU KABISA
 
Utakuwa na matatizo fulani kwenye mishipa ya ubongo wako kwenye kusambaza taarifa mbalimbali kwenye mwili wako, nenda hospital daktari anaweza kukusaidia hiyo sio hali ya kawaida.
 
Hapo ni mambo 2.
1. Psychological issue
2. Magic issue.
Kama ni tatizo no. 1 dawa ni kumwambia mke wako alale na fimbo pembeni, siku akisikia unakojoa tu ile hujamaliza akutandike fimbo moja takatifu.
Hutakojoa tena.
Kama tatizo ni #2, Dawa ni kukutoa hilo pepo la kikojozi basi.
Uko wapi ?
 
Zamani nilisikia wakisema dawa ni mguu wa ng'ombe zile kwato unazichoma then unatwanga zinakuwa unga, unga wake unalamba.

Ni miaka mingi iliyopita ngoja nitajaribu kupiga simu huko nyumbani ngaa wengi waliishaondoka kwenda Mbinguni naamini kwa waliobaki sitakosa wa kunisaidia jibu.

Pia tafuta mwombaji anayeaminika ili muombee hilo tatizo.

Pole.
 
Ingekuwa wewe ni mtoto mdogo tungekutegea wakati umelala fofofo bado hujalimwaga tunakufungia nyoka aliekufa kiunoni kama mkanda ,Ukishamaliza kukojoa ile unajisogeza sogeza ndio unasikia mdudu ambae humuelewi yuko kiunoni , kinachofata ni kupiga nduru na huto kojoa tena labda uzaliwe upya.
 
Duh!! Pole ndugu yangu.

Huko kijijini kwetu hua kuna dawa ya kienyeji, personally sijui inachanganywa na nini au ikoje. But hua najua dingi yangu mdogo mmoja ndo alifundishwa na bibi. Ye ndo hua anaiadminister.

Pamoja na hyo kuna ingine ya kuwacha pombe, hiyo sisi wote tumeikataa. Mtu pekee aliepewa kuitumia ni huyo huyo dingi etu mdogo, na mpka leo hata akoskia puya la pombe mnagombana.

Kuna maza mmoja kijana wake alikua anapiga dude mpka akashindwa kupelekwa boarding alipomaliza primary. So dingi mdogo akaenda huko kumpa hiyo dawa. Siku hizi walaaa hamwagi kojo.

Jaribu kuongea na wa kijijini huko huez kosa mitishamba.

Pia hospitali ni sawa but siez kujua watakusaidiaje
 
Kama tabia hii umetoka nayo utotoni jua muda unaokojoa, ukishaujua weka alamu kwenye simu yako dakika chache kabla ya huo muda kufika. Alamu ikilia nenda chooni kakojoe, ukiona huna muda maalumu wa kukojoa kitandani weka alamu ya masaa mawili mawili au matatu hadi usiku unaisha, alamu ikilia nenda kakojoe.
Kufanya hivyo hutokaa ukojoe kitandani labda liwe tatizo la kiafya au kiroho.

Kama ni tatizo la kiafya nenda hospital na kama ni la kiroho omba Mungu au mshirikishe mchungaji au rafiki wa kiroho unayemwamini akuombee. Ila nzuri zaidi kuomba na mke wako, chukua maombi ya kufunga tatizo litatoweka/kuisha.

Habari z muda kaka na dada zangu wote wa humu jukwaani. Wakuu nimekuja na shida mficha uchi hazai hata kidogo.

Mimi ni mtu mzima 27 yrs nimeoa na mtoto hadi leo bado nakojoa kitandani inauma sana, mke wangu ananivumilia na kunipa moyo sana.


WAKUU NAOMBENI MSAADA WENU TAFADHALI, NAZIDI KUWA MKUBWA SITAKI AIBU KABISA
 
Back
Top Bottom