MSAADA: Nakojoa kitandani licha ya kuoa

MSAADA: Nakojoa kitandani licha ya kuoa

Habari z muda kaka na dada zangu wote wa humu jukwaani. Wakuu nimekuja na shida mficha uchi hazai hata kidogo.

Mimi ni mtu mzima 27 yrs nimeoa na mtoto hadi leo bado nakojoa kitandani inauma sana, mke wangu ananivumilia na kunipa moyo sana.

Nikikojoa huwa naota ndoto nzito halafu kwemye ndoto najiuliza kama naota au live, kisha najiridhisha ndotoni kwamba hapa sioti halafu nakojoa mkojo karibia kuumaliza wote kitandani bila kushtuka.

Lakini HII HALI HUNITOKEA MARA MOJA MOJA PENGINE NAKAA MIEZI SITA,AU MITATU NDO HUTOKEA MARA MOJA.

Inaninyima raha sana mimi nikienda ugenini siwi huru, naweza nikakataa kunywa maji saa 10 jioni ili nikwepe fedheha.

Natamani kuvaa condom nikienda ugenini ili nikikojoa mkojo usifike kwenye godoro.

WAKUU NAOMBENI MSAADA WENU TAFADHALI, NAZIDI KUWA MKUBWA SITAKI AIBU KABISA
Hii hali ilinipataga enzi za mwanzo naoa ila ilipotea yenyewe baada ya miaka 4 kwwnye ndoa, but mm nlikuaa nashtuka mapema sana katikati mkojo ukikuchoma tu unastuka coz unakuwa kati ya reality na ndoto yaan kunakuwa nawazo kwamba umelal na wazo lingine upo maeneo unakojoa kawida . Sasa ile ya mazingira halisi huwa inapita ndo unaanza kukojoa, mkojo ukikugusa akili inaamka na kufikiria upo kitandani then unashtuka.
 
Ukiwa ugenini afanye hivyo hamna namna
Kwa kuepuka aibu itabd nifany hivyo,maana naweza kujiamini kwamba sina tatzo alaf nalala kwa kujiachia kumbe hiyo ndio siku ya tukio daah.

Kuna siku nilikesha maana niliendaga sehemu naheshimika kdg so nikasema hapa nikilala nitaharibu inshu ikabidi nitoboe kitandani kwa nyusingizi nyepes nyepes,kwa kweli hali hii inaniumza san
 
ukiona huna muda maalumu wa kukojoa kitandani weka alamu ya masaa mawili mawili au matatu hadi usiku unaisha
Yani kaka huwa sinaga muda malumu wa kukojoa,kuna siku wiki mbili nyuma siku ya kwanza ilinipata saa kumi na robo usiku,maana nimeshtuka tayari mkojo umeisha.
Siku ya pili yake ukanipata saa kumi kasoro,so sinaga muda maalumu mkuu.
Alafu mkuu nikitega alarm kila baada ya masaa mawili ina maana huwenda nina uvivu wa kuamka mkuu au
 
Yaani unakosa hata kujiamini mke akikukosea kidogo,huwezi hata kumsema
Wife wangu hajawah kuninyima confidens mkuu,wiki za nyuma jimekojoa mkojo mwingi sana kaka.
Wife akapendekeza tutoe godoro nje tulianike.
Mimi nikagoma kwa kwel majirani sumu
 
Pole sana mkuu

Wanaokudhihaki wasamehe tu hawajui magumu unayopitia
Ni kweli kabisa,nikikojoa wife anasema tutoe godoro,mimi nagomaga kwamba hakuna kulitoa godoro litategeshwa humohumo chumbani upande ambao jua linapiga na litakauka.
Alafu kitaa nakubalika ni mtu naonekana poa tu.ila ya ndani tunajua mm na waif
 
Utakuwa na matatizo fulani kwenye mishipa ya ubongo wako kwenye kusambaza taarifa mbalimbali kwenye mwili wako ,nenda hospital daktari anaweza kukusaidia hiyo sio hali ya kawaida.
Mkuu sasa mbna mchana huwa sikojoi hata nikilala fofofo vipi basi kama nna mkojo huwa nashtuka naenda choon,ila shida ucku sasa.
Au matatizo ya neva hayo yanapenda usiku tu naomba muongozo mkuu
 
Wife wangu hajawah kuninyima confidens mkuu,wiki za nyuma jimekojoa mkojo mwingi sana kaka.
Wife akapendekeza tutoe godoro nje tulianike.
Mimi nikagoma kwa kwel majirani sumu
sasa si mtavunda humo ndani,kariakoo kuna mattress proof cover kanunue mnusuru ilo godoro na aibu ya majirani
 
Ingekuwa wewe ni mtoto mdogo tungekutegea wakati umelala fofofo bado hujalimwaga tunakufungia nyoka aliekufa kiunoni kama mkanda ,Ukishamaliza kukojoa ile unajisogeza sogeza ndio unasikia mdudu ambae humuelewi yuko kiunoni , kinachofata ni kupiga nduru na huto kojoa tena labda uzaliwe upya.
nyoka duh ?
 
Kuna mshipa haujakomaaa, ukisha komaa huo mshipa tatizo linaisha hapo hapo na hutakojoa tena kitandani hata uwe kwenye usingizi mnono kiasi gani
 
Zamani nilisikia wakisema dawa ni mguu wa ng'ombe zile kwato unazichoma then unatwanga zinakuwa unga, unga wake unalamba.

Ni miaka mingi iliyopita ngoja nitajaribu kupiga simu huko nyumbani ngaa wengi waliishaondoka kwenda Mbinguni naamini kwa waliobaki sitakosa wa kunisaidia jibu.

Pia tafuta mwombaji anayeaminika ili muombee hilo tatizo.

Pole.
Muelekeze Afanye hivi kwa hiyo miguu ya ng'ombe: Achome kwa moto hilo kanyagio(Asichemshe) halafu abandue kwato kwa uangalifu. Ndani ya hizo kwato zilizobandulia kuna kitu kama aina ya mnofu rangi ya kijivu. Hicho ndio dawa. Unakula unapoenda kulala kila siku kwa muda wa siku tatu. Asante.
 
Pole mkuu me nakushauri uwe unajiwekea mazoea ya kufanya kitu kabla ujakojoa mfano kupiga ngumi ukutani au kujifinya ili ukiona choo ndoton ushtuke
 
Katika wote walioshauri hakuna aliempa pole mkeo.
Kwa niaba ya Ke wote humu , Napenda kuchukua nafasi hii adhimu kumpa Hongera wifi na pole kwa kukuvumilia na kukutunzia siri hakika friji lake linagandisha....maana shilingi ingegeuzwa angekua na mke mwenza zamani sana.
 
Back
Top Bottom