Msaada: Namna ya kukagua gari used Tanzania kabla sijanunua

Msaada: Namna ya kukagua gari used Tanzania kabla sijanunua

Nisije kuonekana mbishi hapa haya jameni kanunueni hayo magari ya aftatu alafu muone kama mtu hajaenda kutubu kwa mfalme zumaridi hapa
unapenda kulazimisha mambo ambayo hayalazimishiki,mfano kama wewe hujawahi shika millioni 100,basi watu wote dunia nzima hawajawahi shika?ni kweli wewe ulinunua gari mbovu kwa hiyo hela,lakini sio kwamba dunia nzima watanunua gari mbovu,kwa kuwa wewe tu ulinunua mbovu,hapana,fikiria kidogo tu...
 
Well,ukifika kwenye gari kwanza kabisa kagua kwa kuiwasha,sikiliza mlio wake wa engine,kisha ukiwa ndani ya gari funguo bonet moja kwa moja nenda upande wa engine ya gari lako,chomoa deep stick kisha iache ingurume kwa sekunde kadhaa,ukiona pale ulipo chomoa deep stick kuna fuka/toa moshi basi jua engine ipo njiani kusumbua,kisha rudisha deep stick yako kisha funguo mfuniko wa engine kagua kama oil inapanda kwa usahihi,hapo utaona vijitone vya oil vinaruka mithili ya mtu anaekaanga labda kitu kwenye jikoni kwa kutumia mafuta kuna vile vijitone huwa vinaruka vidogo sana,ukiona vitone hivyo havitoki basi jua engine haipandishi oil kwa usahihi hapo kuna mawili uchukue ukarekebishe tatizo hilo au uachane na hiyo gari,vuta accelerator ili ukague vizuri mlio wa engine yako,nock alert kama ipo kwenye engine pia kagua exhaust kama kuna moshi unatoka ambao tofauti,ukikuta kwenye exhaust kuna moshi mweupe basi jua engine ya gari ina SMOKE pia itakuwa engine inakula oil ili utatue tatizo hilo yapasa overhaul ihusike,na ukifanya overhaul engine hiyo kuna mawili ikae sawa kabisa ama iendelee kukusumbua hivyo nakushauri uachane nayo.Kagua Arternator kama inachaji vizuri tumia kitu chenye asili ya chuma gusisha pembeni mwa Arternator kama unahisi kuna mvutano flan kama wa sumanku basi jua hiyo ipo fresh kwenye kufua mfumo wa umeme na swala zima la mfumo wa Ac pamoja na kupoza joto la engine kwa kuwa engine inapozwa kwa vitu vitatu{maji,fan belt,na fan yenyewe}.

Kila kitu kikikaa sawa hapo kwenye mfumo mzima wa engine basi funika bonnet rudi ndani washa Air condition ukiona hewa safi baridi inatoka vizuri basi jua ipo vizuri,ukiona gari inatetemeka basi jua kuna vitu vichache vya kubadilisha ama kurekebisha.

Endesha gari ili ukague uzima wa miguu ya gari hapa nakushauri uingize gari kwenye barabara za mtaani haswaa zile zilizopo rough ukisikia kuna milio inayotoka tofauti na ile ambapo upo kwenye lami basi jua uandae hela ya kutosha ili ukarekebishe.

Ahsante karibu Pm kwa ushauri zaidi

Note
Swala la kukagua gari sijui imepata ajali sijui haijapata hili lisikusumbue,hata gari tunazo letewa kutoka huko nje baadhi zimepata wewe kagua vitu hivyo nilivyokuambia.
Kama ntakua kuna sehemu sijaiweka sawa ama nimekosea basi humu kuna wataalam zaidi na watarekebisha pia
Umemaliza kila kitu.
 
Kwa kifupi na kifupi sana tena ,ukitaka gari nzuri kwa hapa bongo land uwe na kuanzia milioni nane mpaka 13 nje ya hapo sijui uba milioni sita sijui tano yatakukuta kama yaliyonikuta mimi kwa kifupi kama bajeti yako ndogo sana bora uongezee ongezee ukishindwa nunua hilo gari na turubai lake kabisa nna uhakika utalifunika tu
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hao wanaoogopa kununua magari ya mikononi nikwamba hawana ujuzi tu na magari, ukiwa na pesa hakuna kinashindikana, ukinunua gari kwa mtu let say milioni sita ukakuta injini inazingua, ilala ipo pale kamatia mswaki wako funga piga mwendo. ukiona gear box inagonga, piga chini weka nyingine piga mwendo, sasa wewe unanunua gari kwa mtu afu ukitegemea utalikuta halina changamoto yoyote? issue ni kupambana na hiyo changamoto and you are good to go.
 
Back
Top Bottom