Msaada namna ya kulipa witholding tax kwenye mfumo wa TRA taxpayer portal

Marco Polo

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
13,538
Reaction score
21,664
Kuna majengo ya serikali nasimamia kama mtumishi wa umma sasa katika kuwalipa mafundi na suppliers Kuna Kodi inatakiwa kulipwa TRA, kwakuwa sina uzoefu na haya mambo nikasema niende ofisini kwao hawa TRA kupata ufafanuzi ila mtumishi wao niliyemkuta anifahamishe namna ya kufanya haya malipo hajanipa ushirikiano nilioutegemea, yule jamaa nahisi ni hawa kamlete wanaoajiriwa bila kufanya interview maana ana dharau vibaya mno kajiachia kama ofisi ya baba yake jinga sana Lile jamaa.

Kama Kuna mtu humu anaweza kunipa japo hints kufanikisha hili jambo nitashukuru sana
 
1) Login kwenye Taxpayer account yako.
2) Click sehemu imeandikwa File Returns
3) Mfumo utakupeleka kwenye Dashboard, Kisha kwa juu kuna sehemu kumeandikwa Manage Tax, basi Click hapo
4) Ukisha Click zitakuja Options, wewe chagua Withhold Option na kisha Chagua Option iliyoandikwa Batch
5) Kisha chagua kwa juu kulia kumeandikwa Add Batch
6) Kisha itakuja Page ya kujaza info za hiyo transaction yako, jaza kisha Click Submit
7) Baada ya hapo Utaiona hiyo Submission yako, utai-Click na kuchagua neno limeandikwa View/Add Deductions
8) Kisha page ikifunguka kushoto kwa juu utaona option imeandikwa Add new deductions, click hapo kujaza taarifa zako kama kiasi, TIN ya huyo mtu unayemkata Withhold, na taarifa zinginezo.
9) Ukimaliza Click Submit.
10) Then ukii-click tena hiyo submission yako utaona option ya ku-generate Control number. Au unaweza kwenda home na kuchagua Tax Payment Option ili kutengeneza Control number

Good luck…
 
God bless you, kwa kutoa elimu.
 
Back
Top Bottom