Msaada namna ya kupambana na Nyoka, naanza kuchoka

Hiyo itakuwa michezo ya baba mwenye nyumba kutaka kukupima kama uko fit. Kama hujang'atwa na hawa nyoka mpaka sasa basi uko fit, we endelea tu kula watoto wa watu huko.
Kuna Demu aliniambia kaachika,lakini kila nikienda kumgonga nikufudi home tu usiku nikiwasha tu taa lazima nikutane na nyoka wadogo wawili,mmoja anakua anatembea zake varandani kuelekea chumbani,na mwingine namkuta tahari yuko chumbani karibu na Kitanda! Ilinitokea Kama Mara tatu hivi, nikaamua kumtema yule Demu kimyakimya bila yeye kujua!! Duniani kuna mengi,sema tu Mungu anatulinda sana!!
 
Katika kuhama ndipo unawapa taharuki unaweza wakuta ndani ya net
 
Haujagundua sehemu wanapoingilia?

Hicho choo kimekaaje, kina mfuniko?

Wanapenda kutembea sana kwenye mabomba ya maji taka na kuibukia chooni.

Hawaji kimiujiza, lazima kuna udhaifu pahali kwenye mjengo ndipo huingilia.

Zama tena kwenye uchunguzi na udhibiti wa mianya.
 
Huu mchanganyiko wako pia ni dawa ya mchwa!
Nimetumia Sana kutibu mchwa ni kiboko aisee,kumbe hata nyoka wanakufa kupitia mchanganyiko huu?
Katika huo mchanganyiko niliongezea na sabuni ya unga pakiti moja
 
Bro hao nyoka hawana madhara kbs wala hawaumi.NI BROWN HOUSE SNAKE..
Wanakusaidia kupunguza pest kama panya au wadudu wengine.
Hawana sumu kabisa bali ni constrictors(wanambana panya pumzi)kisha kummeza.

Uwe na amani kabisa...
Kirahisi rahisi hivi tukuamini. Ha ha ha haaa!
 
Basi huyo demu kategwa na X wake ila hajijuwi tu
 
Dada, sasa hili ni Geto la Bachelor. Yaani huwa naishi kwa week au week mbili kasoro kisha naondoka. Sipiki wala sija jiko. Shukrani sana
 
Kama ni me mtolee yule nyoka mwenzake wacheze nae. Itakua nyoka uliyonae anaita wenzie
Yeah. Yule wa kwanza nilifikiria nikaona ujinga. Nikamwambia hebu toka kapambane na mwenzio huko.....ilizaa matunda!
 
Haujasema upo mkoa gani na eneo lako lipoje umezungukwa na mazingira gani utuonyeshe.....
Nipo Kigoma, Wilaya mojawapo nje kidogo ya Mji, maeneo nje ni masafi maana watu wamelima mashamba kwa ajili ya kulima.

Ni pasafi Ila pia nyumba iko U-Shaped na Mimi room ninayoishi iko huku makalioni, kwahio kwamba nyoka ameingilia getini, kisha akaacha mlango wa kwanza hadi wake huku kwangu, napata tabu kisogo maana getini had I mlangoni kwangu so chini ya mita sita au nane
 
Hiyo itakuwa michezo ya baba mwenye nyumba kutaka kukupima kama uko fit. Kama hujang'atwa na hawa nyoka mpaka sasa basi uko fit, we endelea tu kula watoto wa watu huko.
Haahhaahah sijawahi aiseeee hata kuwaza! Nikija huku nakua na very limited time! Najikuta hats kunywa nanywea room
 
Duh pole sana aiseeee! Tuache mademu was kuokota hovyo hovyo
 
Kwani wewe hutaki wageni😂.
 
Njoo kwenye maombi mkuu hapo unatafutwa na ibilisi
Huyo Ibilisi ameshashindwa big time mwanangu, Mimi chumba changu ndio chumba changu cha ibada.

Mwaka juzi nilikua na shughuli kama hizi huko Njombe nika-opt kupanga geto kupunguza tena gharama za kuishi Guest. Basi Bibi nwenye nyunba alikua kigego balaa ila kwangu ali-blow.

Aliniweza Mara mbili tu, Siku moja nadhani sikusali vizuri halafu nikawa nimekunywa tu-Image tuwili au tatu hivi. Basi unaambiwa SAA kumi usiku nastuka nagusa maji maji kwenye MTO kama vile umande umedondokea MTO! Ila geto lilikua LA ceiling board sasa, nikajua labda nimedondosha udenda nikajichunguza nikakuta hapana ila kabla ya kile kitendo kutokea kulikua na mazingira Fulani hivi, Basi nikahitimisha tu kuwa nilikua na Wageni...

Mara ya pili nilikua namkabidhi room yake na kumuaga, kwahio nikapaki vitu vyangu maana Siku ile ndio nilikua nimefika Njombe, nikajishauri sana nilale Lodge ila nikaamua kulala geto ili niwaage kabisa, chumba kilikua nyumba ya main house....Basi unaambiwa ile asubuhi mida ya SAA kumi hivi, nilimuona Live kabisa yule Bibi. Anyway ndio maisha ya utafutaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…