Msaada: Naomba kujuzwa dawa ya kutibu maumivu ya jino

Msaada: Naomba kujuzwa dawa ya kutibu maumivu ya jino

Naomba kuuliza ni ndulele mbichi au kavu? Na je ni jani la mpapai au bomba lake lile watoto hutumia kupuliza Hali si nzuri meno karibia matatu yanauma please help 🙏🙏
Nilipata dawa mkùu nitakutumia picha ya majani fulani yani hutasikia maumivu hata
 
Habari za muda huu,

Msaada kwa anae fahamu dawa ya kutibu maumivu ya jino watu wengi wananishauri kung'oa ila mi naona sio njia nzuri...

Naomba kama kuna anae fahamu dawa za hospital au hata za kienyeji mana sio kwa maumivu haya jana usiku mpaka nikameza Magnesium asee.
Aise mi nilitafuna arovela then nikaing'ata kwenye jino linalouma na kufunga mdomo kwa muda wa nusu saa, yaani maumivu yote yaliisha ni miezi 2 Sasa Ila arovela chungu kweli
 
hamna Cha ndulele Wala nini dawa ya jino ni kuhakikisha kabila ujalala unaswaki coz sababu kuu ya maumivu ya jino ni mabaki hasa hasa wakati wa usiku so tiba ni kuhakikisha baada ya kula unaswaki hasa hasa usiku ...tafuta whitedent gel Ile ya blue...au Colgate max cooling...hizi dawa mbili zitakusaidia.....coz zinapunguza maumivu ya jino ...
 
Wapendwa za jioni

Aki jino linaniuma sana na sitaki kulitoa mwenyew anajua dawa mzuri aki nisaidieni nashindwa kuongea na simu kabisa pleas anaejua dawa
 
Wapendwa za jioni

Aki jino linaniuma sana na sitaki kulitoa mwenyew anajua dawa mzuri aki nisaidieni nashindwa kuongea na simu kabisa pleas anaejua dawa
Kama limeanza kukuuma nenda hospital wakaone limeharibika kwa namna gani. Ni vizuri ukatafuta specialist wa meno. Mimi niliwahi kuumwa Dr akanicheck akasema kwa hili linafaa kuzibwa tu. Likasafishwa lizibwa Hadi Leo Niko poa...

Pia jijengee tabia ya kuwa unatafuna karafuu ..unakuwa unazibani kwenye meno. Tafuna tu taratibu. Unaweza kuweka hata interval ya siku Moja au mbili..zinasaidia sana kwenye afya ya meno hata kukata harufu ya kinywa. Pia zinapunguza maumivu ya meno kama jino linauma
 
Ngoja nimtume mtu anitafutie karafuu asante
 
Daah jino, miye jino linataka kutoka lakini hakuna nafasi huko mwisho kinywani. Daktari alisema idha wanichane ufizi au kutoa. Looh kutoa jino zima masaa matatu ganzi mbili nilitoka hospital nalia mpk nafika home. Wiki 3 ndiyo maamivu yameisha na dozi kibao sina hamu na jino miye..
 
Dawa ya jino kun'goa amna porojo tena
Na Mimi mwanzo nilielewa hivyo lakini baada ya kujishughulisha kutafuta ukweli. Si lazima dawa ya Jino iwe ni kung'oa. Kama Jino halijatoboka sana kiasi cha kubakiza vipande vya mizizi basi dawa yake ni kuziba ama baada ya kuua mishipa ya fahamu ya Jino hilo ama Hata bila kuua mishipa hiyo.

Watafute madaktari wa meno mahiri. Mahiri neno Lina uzito hili. Hao watakupa huduma Bora. Madaktari hawa wanapatikana kwa wingi kwenye hospitali za serikali na za binafsi. Pole sana mleta mada.
 
Daah jino, miye jino linataka kutoka lakini hakuna nafasi huko mwisho kinywani. Daktari alisema idha wanichane ufizi au kutoa. Looh kutoa jino zima masaa matatu ganzi mbili nilitoka hospital nalia mpk nafika home. Wiki 3 ndiyo maamivu yameisha na dozi kibao sina hamu na jino miye..
Mimi liliwahi kuuma kipindi fulani. Maajabu yake nilikuwa nikilia kwa sauti kiasi maumivu kama yanapungua hivi, nikilia kwa sauti kubwa kabisa haliumi kabisa, nikaona isiwe tabu.
 
Mimi liliwahi kuuma kipindi fulani. Maajabu yake nilikuwa nikilia kwa sauti kiasi maumivu kama yanapungua hivi, nikilia kwa sauti kubwa kabisa haliumi kabisa, nikaona isiwe tabu.
Duuh ningekitungua kilio alafu nafunga vioo na mlango kwani shilingi ngapi. Jino ni noma, sasa hili langu lilikuwa zima sema lilikuwa linaota chini ya ufizi basi wee ufizi unavimba kula huwezi kusema pia huwezi unajitonesha.
 
Wapendwa za jioni

Aki jino linaniuma sana na sitaki kulitoa mwenyew anajua dawa mzuri aki nisaidieni nashindwa kuongea na simu kabisa pleas anaejua dawa
Kuna dawa moja, unaweza kushangaa! Leo nataka niwanong'oneze hapa JF. Kama kuna mwingine yeyote anaumwa jino/meno, inawezekana leo ndiyo ikawa mwisho wa hilo tatizo. Na naomba, atakae jiona amepona, aje atoe ushuhuda hapa JF.
Naomba ruhusa yenu!
 
Back
Top Bottom