Msaada: Naomba kujuzwa dawa ya kutibu maumivu ya jino

Msaada: Naomba kujuzwa dawa ya kutibu maumivu ya jino

Unaweza nielekeza
Na Mimi mwanzo nilielewa hivyo lakini baada ya kujishughulisha kutafuta ukweli. Si lazima dawa ya Jino iwe ni kung'oa. Kama Jino halitoboka sana kiasi cha kubakiza vipande vya mizizi basi dawa yake ni kuziba ama baada ya kuua mishipa ya fahamu ya Jino hilo ama Hata ba kuua mishipa hiyo.

Watafute madaktari wa meno mahiri. Mahiri neno Lina uzito hili. Hao watakupa huduma Bora. Madaktari hawa wanapatikana kwa wingi kwenye hospitali za serikali na za binafsi. Pole sana mleta mada.
huyo dr
 
Hebu fata maelekezo yangu, leo utalala bila maumivu. Kesho, utajiona umepona.

Ni hivi: -

Kama nilivyosema, dawa yenyewe, waweza kushangaa. Nakushauri usiidharau, na kwa vile ni ya KAWAIDA SANA, ijaribu hutapungukiwa na kitu.
--
Chukua maji ya kawaida tu, sio ya moto au baridi, piga mswaki ukiyasugua meno yote. Ukimaliza, chukua soda ya Cocacola, isiyo ya baridi, ni vizuri ukiimimina kwenye kikombe au jagi. Anza kwa kujaza funda mdomoni.

Sugua meno yote kwa mswaki, kisha unatema hiyo soda. Hakikisha unasugua vizuri yale meno yaumayo, kwa juu na pembeni. Uwe unachukua muda kidogo, ili hiyo soda ipenye vizuri kwenye hayo meno. Na hakikisha hiyo soda inaisha yote.

Nakuhakikishia, baada ya zoezi hilo, hapo hapo utaona mabadiliko fulani. Nishawashauri watu wengi sana, hakuna hata mmoja ambaye hakusaidiwa na DAWA hiyo. Na sio kuwa inatuliza, inaponyesha kabisa.

Nakushauri, we jaribu tu!
 
Tafuta mti(mfumbi) kata magamba yake yaanguke chini yawe ma5...
Okota magamba yaliyofunuka yale yaliyojifunia achana nayo...
Nenda kachemshe mpaka yakaribie kuungulia,ule mchuzi wa mwisho uhifadhi kwenye kikopo...
Piga mswaki kwa hayo maji ukiamka na muda wa kulala...

NB:NASUBIRI FEEDBACK
 
Unaweza nielekeza

huyo dr
Kwa Mbeya nenda Agha Khan hospital ipo Karibu na stend kuu ya mabasi ya mikoni. Pia hospitali y UWATA Mbeya, ingawa sina hakika kama yule dentist bado yupo pale. Hospital za serikali, nasikia huko Morogoro Kuna hospital ya Sabasaba. Kwa Dar es Salaam. Nadhani walioko huko wanisaidie kukuelekeza. Asante.
 
Wapendwa za jioni

Aki jino linaniuma sana na sitaki kulitoa mwenyew anajua dawa mzuri aki nisaidieni nashindwa kuongea na simu kabisa pleas anaejua dawa
Nina nti hapa ukiuchemsha na kusukutua Yale maji ndani ya nusu SAA utakua umepona. Najua jina lake kwa kilugha. Sijui nitakuambiaje.

Mti huu unapatikana Sana Dar.
 
Chovya njiti ya kiberiti kwenye furushi bichi la kimba la mtu mzima lililoshushwa dakika 5 zilizopita na upake kidogo kwenye jino Sumbufu nakwambia utakuja nishukuru humu
 
Acheni kudanganyana, kung'oa ni option ya mwisho kabisa, mi kuna jino niliwah kung'oa najilaumu mpka kesho.

Tafuta daktari anayeeleweka, kuna root canal treatment na kuna kuziba, maumivu utayasikia kwenye bomba tu.
 
Nunua vidonge vya ampiclox dozi .
Vitakusaidia kuua maambukizi ya bacteria kwenye jino na kukausha pia , meza ampiclox pmj na paracetamol ,
Pili zingatia usafi wa kinywa asubuhi na jion uswaki >>>tumia Colgate max n nzur , baada ya kula pia chakula Cha mchana sukutua usibaki na mabaki ya chakula .
NB: jino litatulia tu kwa muda mrefu had utasahau maumivu ya jino but haziponeshi otherwise ukang'oe[emoji1]
 
Dawa ipo.nenda duka la asili.kuna dawa jina nimeisahau.ni kusukutua.ukiweka mdomoni inatoa povu.ni nzuri Sana.wanauza 2,000 mpaka 3,000.
Unatumia asubuhi,mchana na jioni
Nenda kanunue.inaua wadudu wote
 
Uko wapi nikuelekeze...dawa hupatikana kulingana na mazingira yako...mkoa wako.

Kuna mti unaitwa mchunga kaburi unapatikana Arusha, Dodoma, singida hata Shinyanga Tabora na Mwanza.

Kata tawi lake menya maganda na yale maji maji yake sukutua meno.

Pili...kama utapa ndulele;
- ifunge kwenye kitambaa safi cha pamba
-mwagia mafuta ya taa
-chukua jani au mrija wa jani la mpapai
- washa hiyo ndulele kwa moto
-vuta moshi wake kwa mrija wa mpapai

---huo moshi usiumeze bali ufunge mdomo kwa dakika zisizopungua tatu then fungua mdomo
.....
.....
Matokeo yatakushangaza hasa haya na namba mbili
Mim naumwa jino hapa ,napitia maoni ya wadau ili nijitibu, ila pia naogopa hii dawa yako mkuu inaweza kuanza kunipa experience ya kuanza kuvuta shisha!😂
 
Mim naumwa jino hapa ,napitia maoni ya wadau ili nijitibu, ila pia naogopa hii dawa yako mkuu inaweza kuanza kunipa experience ya kuanza kuvuta shisha!😂
Wasiwasi wako tu
 
Habari za muda huu,

Msaada kwa anae fahamu dawa ya kutibu maumivu ya jino watu wengi wananishauri kung'oa ila mi naona sio njia nzuri...

Naomba kama kuna anae fahamu dawa za hospital au hata za kienyeji mana sio kwa maumivu haya jana usiku mpaka nikameza Magnesium asee.

Kamuone Dr wa meno ili ujue kwanini hasa jino linauma. Je una tobo chini ya jino, infection au nini hasa
 
Mimi jino lilitoboka niliamua tuu kuosha meno kwa CLENORA mouthwash sasa hivi hata punje ya mhindi ikiingia haliumi. Mimi siyo daktari niliamua tuu na imenisaidia sana.
 
Back
Top Bottom