Msaada: Naomba nijue stahiki za watoto wangu

prettykind21

Member
Joined
May 16, 2023
Posts
99
Reaction score
164
Habari ipo hivi,

Mimi niliolewa ila nilitengana na mwenzangu, tuna watoto wawil. Mmoja miaka mitatu mwingine ana mwaka mmoja, sasa baba yake amekuwa mwiba kwangu ananitishia sana kuhusu kunipokonya watoto na nikikataa ananitishia kukatiza matunzo.

Jamani naombeni kufahamu endapo nikienda mahakamani nitapata haki zangu ama? Je, mahakamani ni nini wanaangalia? Mimi kwa sasa nafanya biashara napika vitafunwa mashuleni ila baba wa mtoto ni engineer, nisaidieni jamani maana sina amani na wanangu kama nimewaiba jamani wakati nimezaa mwenyewe na ananimbia akiwachukua sitawaona tena.

Nisaidieni jamani yeye anainjoi mimi nateseka na watoto halafu anajifanya anawapenda watoto wakati huduma shida, hivi jamani nifanyaje?
 
Relax,hao watoto ni wadogo wala hawezi kuwachukua,nchi inaendeshwa kwa rule of law na sio kwa atakavyotaka yeye,hawezi kustop kutoa child support kwa utashi wake tu,

Anzia kwenye ngazi za chini kabla hujafika mahakamani,ila unaweza kumsikiliza tu kwanza coz nina uhakika hawezi kufanya lolote zaidi ya kukutishia tu,

Je baada ya kuachika umeolewa na mwingine?
 
Hii ni one side story. Tungesikia na upande wa pili.
Inawezekana kuna wakati watoto wako wanakosa uangalizi au huduma sahihi toka kwako sababu ya majukumu ya kujitafutia ridhiki, au starehe, kwenye ibada, n.k.

Kama wana uangalizi mzuri wakiwa kwako hawezi kuwachukua hadi wafikishe miaka 7, hiyo kwa mujibu wa sheria. Pesa ya huduma kwa watoto lazima atoe.
Ondoa shaka anakutisha tu.
 
hapana sijaolewa
 
inawezekana ikawa side story ila ningekuwa mbaya ningeweka madhaifu yake au ningesimulia pengine upande wake kwa ubaya zaidi nilichosema haijalishi nani alikuwa mkosefu kwenye ndoa ila tumeachana shida ipo kwann haudumii watoto halaf anataka watoto? anahisi kwamba pesa anayotoa mimi nitaila?? au anawazaje? na mm sio mtu wa starehe nipo nyumban na biasharra zangu sinywi pombe sizururi ovyo nikitoka biashara nazofanya napika home naweka dukani so kwamuda mwingi nipo ndani tu nikitoka jumapil kanisani basi
 
alishaenda yeye kudai watoto ustawi naona wamepewa hongo maan wananishaur baba ana haki ya kuwachukua eti watoto ndo maan nikataka kuenda mahakamani
Katika vitu usikubali ni kuacha watoto wako wakiwa wadogo walelewe nje na wewe mama yao. Watoto wana haki ya kwenda kukaa na baba yao wakifika miaka 7. Sijajua taratibu za mahakamani ila kipaumbele cha kwanza ni kulea watoto wako wewe mwenyewe no matter what.
 
asante
 
Habari ipo hivi,

Mimi niliolewa ila nilitengana na mwenzangu, tuna watoto wawil. Mmoja miaka mitatu mwingine ana mwaka mmoja, sasa baba yake amekuwa mwiba kwangu ananitishia sana kuhusu kunipokonya watoto na nikikataa ananitishia kukatiza matunzo.

Jamani naombeni kufahamu endapo nikienda mahakamani nitapata haki zangu ama? Je, mahakamani ni nini wanaangalia? Mimi kwa sasa nafanya biashara napika vitafunwa mashuleni ila baba wa mtoto ni engineer, nisaidieni jamani maana sina amani na wanangu kama nimewaiba jamani wakati nimezaa mwenyewe na ananimbia akiwachukua sitawaona tena.

Nisaidieni jamani yeye anainjoi mimi nateseka na watoto halafu anajifanya anawapenda watoto wakati huduma shida, hivi jamani nifanyaje?
Yangu haya;

1. Watoto huwa wanakaa na mama wakiwa wadogo, kama sijakosea chini ya miaka 7. Lakini, mama lazima awena uwezo yeye mwenyewe wa kuwatunza, si ategemee kwa baba yake mzazi (babu wa watoto) au ndugu mwingine katika familia ya mama. Baba mzazi wa watoto anapewa haki ya kuwaona kwa kadri iwezekanavyo.

2. Baba wa watoto ataambiwa kuwatunza watoto kwa maana ya kiasi fulani cha fedha kutegemeana na uwezo wake. Lakini hapo, mama naye anapewa jukumu la kuchangia. Mara nyingi huwa 70% baba, na 30% mama kwa yale yaliyo wazi mfano ada etc

3. Kutengana, hakufanyi mali iliyochumwa iwe ya watoto. Maana wanasema, hata bila mali hiyo watoto mngewalea tu. Hivyo maamuzi huwa ni kuuza kila kilichopatikana mkiwa wanandoa na kugawana baada ya mauzo. Tathmini ya thamani ya mali iliyochumwa hufanywa na mahakama. Ila ikitokea mmoja ameamua kumwachia mwingine, hapo mahakama haitii neno.

4. Wakifika umri wa zaidi ya miaka 7, na jamaa akienda mahakamani, atawachukua tu.

La mwisho ni ushauri;
Acha kushindana na EX-mumeo kwa kujionyesha kuwa unaweza bila yeye. Maana hata uwakatazie vipi, akienda mahakamani anawachukua.
 
Back
Top Bottom