Msaada: Naomba nijue stahiki za watoto wangu

alishaenda yeye kudai watoto ustawi naona wamepewa hongo maan wananishaur baba ana haki ya kuwachukua eti watoto ndo maan nikataka kuenda mahakamani
Ni ukweli Sheria ya Ndoa inapa baba haki ya kukaa na watoto. Katika hali ya kawaida, mtoto wa chini ya miaka saba anapaswa kukaa na mama yake kama mazingira ni mazuri. Maamuzi ya nani akae na mtoto hutegemea umri na maslahi mapana ya mtoto.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kama huwezi kuwahudimia mwachie akawatunze. Baadhi ya wanawake wamekuwa wakitumia hali hii kama mradi.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana bibie,
 
Siyo kumis tu maana mala nyingi ma single mother ndo huwa chanzo cha uchochezi wa watoto wa mtaani
 
2. NI UMRI GANI MTOTO AKAE NA MAMA.
Kifungu cha 26( 2 ) cha Sheria ya mtoto, namba 21 ya 2009 kinasema kuwa ni vizuri mtoto aliye chini ya umri wa miaka saba akae na mama. Hata hivyo ni vema kufahamu kuwa kifungu hiki hakikusema ni lazima( shall) mtoto wa umri huo akae na mama.
Kifungu kinasema suala la mtoto chini ya umri wa miaka saba kukaa na mama ni dhana inayoweza kutozingatiwa( rebuttable presumption). Ni dhana inayoweza kutozingatiwa kwa maana kuwa zipo sababu ambazo mtoto chini ya umri huo inaweza kuamuliwa kukaa na baba au mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kufaa zaidi kuliko mama.
Kwahiyo lazima tuzingatie kuwa sio lazima mtoto chini ya umri wa miaka 7 kukaa na mama.
3. SABABU ZIPI MTOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA 7 ATAAMULIWA KUKAA NA BABA.
Kifungu cha 37( 4 ) kinasema kuwa katika kutoa amri ya mtoto akae na nani mahakama itatakiwa kuzingatia maslahi mapana ya mtoto husika( best interest of the child). Kwahiyo habari sio kwamba lazima mtoto akae na mama au baba laa hasha, isipokuwa habari ni maslahi mapana ya mtoto, wapi mtoto atapata malezi bora.
Hii ndiyo sababu au kigezo kikuu kinachozingatiwa na mahakama inapokuwa inaamua. Kwa ufupi maslahi mapana ya mtoto ni kama, wapi kuna mazingira mazuri kwa mtoto, ni mzazi yupi anajali kuliko mwingine, wapi atapata matunzo bora, wapi hatanyanyaswa, mzazi yupi ni mlevi, kahaba na ana tabia mbaya, ikiwa kuna mzazi ana matatizo ya akili, magonjwa ya kuambukiza n.k.
Kwa hiyo kwa ujumla niseme kuwa mtoto chini ya umri wa miaka 7 ni vizuri kukaa na mama lakini ikiwa baba atathibitisha mambo ambayo hayafai kwa mama basi anaweza kupewa mtoto na akaachwa mama .

nimeitoa kutoka: Ruheso-Tanzania
 
KUPITIA UZOEFU WANGU,
NAONA KUNA MASHINDANO KATI YENU WAZAZI NA WANAO UMIA NI WATOTO.
KUNA UWEZEKANO MKUBWA NDUGU ZAKO, AU MWANAUME WA NJE ANAKUPANDISHA KICHWA, KIASI UNAJIONA UNAWEZA KUSHINDANA NA MZAZI MWENZIO. HAPA NDIPO WENGI WANAKOSEA.

WANAUME ALIUMBIWA KUPENDA, NA KAMA ALIKUCHAGUA KATI YA WENGI NA LEO KAKUKIMBIA NI ISHARA KUNA TATIO UPANDE WAKO.
VYEMA UKAKUBALI HATA WEWE UNA MAPUNGUFU KAMA ALIVYO YEYE, NA NI CHANZO CHA ANGUKO LENU
ANGALIA SANA WALIO KUZUNGUKA WANAWEZA WASIWE WASHAURI WAZURI KWAKO HATA KAMA NI WAZAZI.

NAKUSHAURI: TAFUTA SULUHU NA MWENZIO NJE YA HAYA MAMBO YA SHERIA KWA AFYA NA USTAWI WA WATOTO WAKO.
MAHAKAMANI ANAWEZA AMLIWA KULIPA LAKI MOJA KWA KILA MTOTO KWA MWEZI. MKIKUBALINA WENYEWE, KWA HIARI YAKE, BABA ANAWEZA KUWA NA UWEZO WA KUTOA MATUNZO ZAIDI YA LAKI TANO KWA MWEZI, KUSOMESHA SHULE NZURI, KUWAWEKEA BIMA YA MAISHA, KUWATAFUTIA VITEGEA UCHUMI KAMA VIWANJA NA MASHAMBA NK

AISEE POLE SANA
 
nimekuelewa mkuu asante sana
 
Tatizo wanawake mnakuwa na akili za kitoto sana. Kwa nini unashindana na mtu mwenye hela. Sisi wanaume tukijua huyu mtu ana michongo tunajifanya wajinga ili tutusue. Kama hauwezi kuwalea watoto mwenyewe mpe tu Jamaa. Ukibaki nao utakuja kupigwa mimba na wahuni. Naomba nikuambie ukweli mchungu "hakuna chochote kilichokuwa kinakuweka mjini mbali na cheo cha mke alichokupa jamaa" . Hicho cheo huna anza upya yaani ni kama Tajiri aliyefilisika. Wasogeze watoto kwa baba yao. Jiongezee thamani,jifunze kitu kipya kama ni biashara au fani yenye kupata faida. Mdogo mdogo utasimama mwenyewe. Nakupa hii option kwa sababu hautaki kujishusha mwanzo ni mgumu lakini utaisha.
 
sawa ila mkuu watoto wadogo aka kengine kananyonya miez 10? nimpe baba yake?
 
mtoto siku zote ni wamama kuwaba ubini ni sheria na taratib zilivyo sio kwamba eti kisa ubini wako mtoto wa baba sio kwel aliyomzaa ndo mwenye mtoto[emoji23]
Na ukibeba mimba huwa mnasema mimba ya nani?, Wanawake hwana mnanichekedhaga sana. Sasa kama mtoto ni wa mama inakuwaje huwa hamuwezi kuwatunza mpaka baba ndo atunze watoto, na wakiwa kwa baba zao huwa hamchangii matunzo
 
sawa ila mkuu watoto wadogo aka kengine kananyonya miez 10? nimpe baba yake?
Hapo hamna jinsi komaa tu ili usichoke kujishusha. Na kuomba msamaha itachukua muda lakini wanaume tunapenda kunyenyekewa. Ila kwenye mambo mengine badilisha maisha yako bana matumizi tambua kuwa unaanza upya komaa utatoboa.
 
Hata kama wamefikisha miaka Saba au zaidi ya Saba. Mahakama haiwezi kumkabidhi Watoto huyo baba kirahisi hivyo. Kinacho angaliwa ni maslahi mapana ya hao watoto. Kama mama anazo changamoto ambazo zinaathiri kabisa Maendeleo na ustawi wa hao watoto itamkabidhi baba. Pia mahakama itasikiliza maoni ya hao watoto walio na umri zaidi ya miaka Saba wao wanataka kuishi upande upi na Kwa Nini wachague upande huo
 
Sheria nyingi za ndoa zina m favour mwanamke, hii sio sawa
 
mtoto siku zote ni wamama kuwaba ubini ni sheria na taratib zilivyo sio kwamba eti kisa ubini wako mtoto wa baba sio kwel aliyomzaa ndo mwenye mtoto[emoji23]
Pole kwa uliyopitia ila kwa hii coment yako hapo inaonyesha wewe ni miongoni mwa wanawake jeuri sana na wakujifanya wajuaji huku hawana lolote labda kama umecomment bila kufikiri.
Kila la heri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…