Habari ipo hivi,
Mimi niliolewa ila nilitengana na mwenzangu, tuna watoto wawil. Mmoja miaka mitatu mwingine ana mwaka mmoja, sasa baba yake amekuwa mwiba kwangu ananitishia sana kuhusu kunipokonya watoto na nikikataa ananitishia kukatiza matunzo.
Jamani naombeni kufahamu endapo nikienda mahakamani nitapata haki zangu ama? Je, mahakamani ni nini wanaangalia? Mimi kwa sasa nafanya biashara napika vitafunwa mashuleni ila baba wa mtoto ni engineer, nisaidieni jamani maana sina amani na wanangu kama nimewaiba jamani wakati nimezaa mwenyewe na ananimbia akiwachukua sitawaona tena.
Nisaidieni jamani yeye anainjoi mimi nateseka na watoto halafu anajifanya anawapenda watoto wakati huduma shida, hivi jamani nifanyaje?
2. NI UMRI GANI MTOTO AKAE NA MAMA.
Kifungu cha 26( 2 ) cha Sheria ya mtoto, namba 21 ya 2009 kinasema kuwa ni vizuri mtoto aliye chini ya umri wa miaka saba akae na mama. Hata hivyo ni vema kufahamu kuwa kifungu hiki hakikusema ni lazima( shall) mtoto wa umri huo akae na mama.
Kifungu kinasema suala la mtoto chini ya umri wa miaka saba kukaa na mama ni dhana inayoweza kutozingatiwa( rebuttable presumption). Ni dhana inayoweza kutozingatiwa kwa maana kuwa zipo sababu ambazo mtoto chini ya umri huo inaweza kuamuliwa kukaa na baba au mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kufaa zaidi kuliko mama.
Kwahiyo lazima tuzingatie kuwa sio lazima mtoto chini ya umri wa miaka 7 kukaa na mama.
3. SABABU ZIPI MTOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA 7 ATAAMULIWA KUKAA NA BABA.
Kifungu cha 37( 4 ) kinasema kuwa katika kutoa amri ya mtoto akae na nani mahakama itatakiwa kuzingatia maslahi mapana ya mtoto husika( best interest of the child). Kwahiyo habari sio kwamba lazima mtoto akae na mama au baba laa hasha, isipokuwa habari ni maslahi mapana ya mtoto, wapi mtoto atapata malezi bora.
Hii ndiyo sababu au kigezo kikuu kinachozingatiwa na mahakama inapokuwa inaamua. Kwa ufupi maslahi mapana ya mtoto ni kama, wapi kuna mazingira mazuri kwa mtoto, ni mzazi yupi anajali kuliko mwingine, wapi atapata matunzo bora, wapi hatanyanyaswa, mzazi yupi ni mlevi, kahaba na ana tabia mbaya, ikiwa kuna mzazi ana matatizo ya akili, magonjwa ya kuambukiza n.k.
Kwa hiyo kwa ujumla niseme kuwa mtoto chini ya umri wa miaka 7 ni vizuri kukaa na mama lakini ikiwa baba atathibitisha mambo ambayo hayafai kwa mama basi anaweza kupewa mtoto na akaachwa mama .
nimeitoa kutoka:
Ruheso-Tanzania