Msaada: Naomba ufafanuzi kuhusu haki za mtoa taarifa ya uhalifu

Msaada: Naomba ufafanuzi kuhusu haki za mtoa taarifa ya uhalifu

AFRICAN POWER

Senior Member
Joined
Jun 17, 2022
Posts
151
Reaction score
234
Habari za leo wana JF wenzangu.

Hivi raia akitoa taarifa za uhalifu kwa siri katika maeneo yake kwa mamlaka inayohusika na kupokea taarifa hizo, akakuta taarifa ile imesambazwa na mpokea taarifa kuwa fulani yupo hivi na vile ndiye aliyetoa taarifa hizi kuwa wewe fulani ni mhalifu.

Je, mtoa taarifa ana haki ya kumchukulia hatua yule mpokea taarifa mwenye mamlaka ya kulinda taarifa za siri za uhalifu kwa kuzisambaza na kuhatarisha usalama wa mtoa taarifa?
 
Ndio, kinachofanyika unatakiwa uwe na ushahidi kuwa taarifa uliyotoa imesambazwa na huyo mpokea taarifa (Mathalan ni Polisi-Mpelelezi)

Na ushahidi huu unaupeleka kwenye uongozi wa juu yake Msambaza taarifa

Hongera umefanya jambo jema kutoa ushirikiano.
 
Uungwana ni vitendo, wewe ni muungwana ila pia kuwa makini na chukua tahadhari unapotoa taarifa za uhalifu hasa kwa jeshi letu la polisi ambalo lina wajibika kulinda mali na usalama wa raia.

Askari polisi (baadhi) sio wote wanakiuka maadili yao ya kazi, ndio maana nimesisitiza umakini unatakiwa.

Kama upo mtaani kuna watendaji wa kata, mtaa au mwenyeki wa mtaa, diwani, mkuu wa wilaya au mkoa( kwa ngazi ya wilaya au mkoa). Hao niliowataja wanaingia kwenye vikao vya ulinzi na usalama na wanaweza kukusaidia ukitoa taarifa au ukiona vipi kuna ofisi ya DSO au RSO unaweza ukapeleka taarifa pasipo kujulikana na wakaifanyia kazi taarifa yako.
 
Uungwana ni vitendo, wewe ni muungwana ila pia kuwa makini na chukua tahadhari unapotoa taarifa za uhalifu hasa kwa jeshi letu la polisi ambalo lina wajibika kulinda mali na usalama wa raia.
Mi nadhani ushauri wako ni mzuri zaidi.

Na sisi wananchi tuwajibike kuwa na mawasiliano ya watu wa hizo taasisi. Nasikia yale majamaa hayavujishagi taarifa bana na mtoa taarifa anakuwa salama sana!

TULISAIDIE TAIFA LETU!!!!
 
Hao hao polisi hawana siri, hapa jirani walikuja kumkamata muuza gongo na wakasema ni fulani kasema.

Hapo juzi kuna mama amekamatwa wakasema ni mtendaji kakusemea.

Ni afadhali ufungue uzi huku jf japo ukiwataja watu nao uzi utamezwa.

Hapo sasa angalia utakavyojilinda maana ulinzi wako uko mikononi mwako mwenyewe.
 
Ahsante ndugu,ninakusanya ushahidi wa kauli na sauti za wahusika japo kuna kutishiwa maisha.
Ninafikiri kitendo cha kufahamika kuwa wewe ndiye uliyetoa taarifa za kuwa fulani ni mhalifu, ni ushahidi tosha.

Amejuaje kuwa wewe ndiye uliyetoa taarifa?
 
Back
Top Bottom