Uungwana ni vitendo, wewe ni muungwana ila pia kuwa makini na chukua tahadhari unapotoa taarifa za uhalifu hasa kwa jeshi letu la polisi ambalo lina wajibika kulinda mali na usalama wa raia.
Askari polisi (baadhi) sio wote wanakiuka maadili yao ya kazi, ndio maana nimesisitiza umakini unatakiwa.
Kama upo mtaani kuna watendaji wa kata, mtaa au mwenyeki wa mtaa, diwani, mkuu wa wilaya au mkoa( kwa ngazi ya wilaya au mkoa). Hao niliowataja wanaingia kwenye vikao vya ulinzi na usalama na wanaweza kukusaidia ukitoa taarifa au ukiona vipi kuna ofisi ya DSO au RSO unaweza ukapeleka taarifa pasipo kujulikana na wakaifanyia kazi taarifa yako.