Msaada: Natafuta kazi ya kufanya. Ni mwepesi kujifunza kazi yoyote

Msaada: Natafuta kazi ya kufanya. Ni mwepesi kujifunza kazi yoyote

Dunia ni codes,zifungue uwe huru.
Mfano jiulize kwann wazungu wanatoa sana misaada afrika ukidhani wanatupenda sana,jiulize mbona tangu tuanze kusaidiwa mbona hatuendelei wao ndio wanaofaidika na kuendelea siri wanachukua baraka zetu,
Au kwann watu wanakesha wanaomba makanisani but still wanatandikwa na umasikini, maombi si jibu pekee kwa Mungu bali uzijue codes za kiMungu ili ufanikiwe.
Duuuh mkuu share hapa basi chochote..
Mana naona unaongea vitu confidential sana mkuu 🙌🙌🙌🙌🙌
 
Hapana mkuu, ila hata mimi siku yakinikuta lazima nipite njia hii
 
Kanijibu kwa bonge la risala lililojaa hasira za mkizi ndaniyake....[emoji1787][emoji1787] christophany
Tunavumiliana mkuu, naweza kukujibu kwa jazba ukashangaa kumbe hasira zangu zimetoka mbali sema sikuwa na sehemu ya kuzipunguzia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hujajua nimekutafakar kias gan ushawah kuwaza wewe ndio unashida halaf mm nmekuchukulia ulivyochukulia?

halaf kwenye halaiki ya watu namna hii. Au hujui kama comment yako Moja inaweza mfanya mwingne awaze kma ulivyowaza

na inaweza mnyima mtu nafasi ya kumsaidia mtu

ukitaka kujua Hilo fuatilia wangap watalike na kusupport ulichoandika ndio utajua kwann nimeweza kuandika maneno meng kias hiko kwenye maneno yako machache

ila okey umeeleweka na hongera [emoji120]
Mkuu kumbe huwa una busara aisee, hii safi nimeipenda
 
Hapana ila nmegundua asilimia kubwa ya watz tunapenda sana dhalau hasa Kwa Watu tusiowajua na hii imewagharimu wengi. Haiwezkan from no where unamashaka na mtu kuwa mpyaa JF inamaana Kuna idadi maalumu wa wahusika humu au

hiyo haitoshi mtu hawaz hitaji alilonalo mtu anaandika comments zinazolenga kuleta taharuki Kwa wengne , kma umefuatilia comment yake wapo walioisupport kitaalamu pale ishaniondolea idadi ya Watu ambao wangekuwa na msaada kwang .
Uko sahihi mkuu, ila nakushauri jaribu kuzuia hasira zako, maana humu tupo watu wa aina nyingi sana, wengine anaweza kukukwaza si kwa nia mbaya ila anataka kujua kiwango chako cha uvumilivu, sasa mtu wa kukusaidia anapoona kuwa jambo dogo una panic kidogo inaleta ukakasi. Kikubwa usaidike na mimi nakuombea heri mkuu
 
Hayo mashamba yaliuzwa shilingi ngapi na ada ya sekondari ilikuwa ni kiasi gani hadi isitoshe kukusomesha hadi chuo kikuu?

Na kama mashamba yaliuzwa halafu ukakomaa na masomo, ilikuwaje haukufaulu, hebu naomba ufafanuzi na please jitahidi kunyoosha maelezo huku ukitoa figures?
 
Habari wanajukwaa wa JF

Mm ni kijana mwenye umri wa miaka 31 elimu yangu ni kidato Cha sita(6) naomba msaada wa kupata kazi yoyote itakayoniingizia kipato ili maisha yangu yaende ,

Unaweza jiuliza umri huo na elimu ya kidato Cha sita ilikuwaje ?

Kimsingi nilimaliza kidato Cha sita 2013 nilipomaliza nilitaka kuendelea na masomo ya chuo kikuu ila sikufanikiwa kupata mkopo

Na familia yangu haikuwa na uwezo kabisa wa kuweza Tena kunilipia ada sio Siri kwasababu hata kufika kidato Cha sita chenyewe yaliuzwa Hadi mashamba ili tu nisome japo shule ni za serikali

Kwahyo baada ya kushindwa kuendelea na masomo nikalazimika kubaki nyumbani Kwa mwaka huo nikiamini yamkini mwaka unaofuata mambo yanaweza yakawa vzr nitaenda

Lakini mambo hayakuwa mazuri nilipata changamoto nyngn nying za kifamilia ambazo siwez ziandika hapa zote hivyo ikapelekea nipoteze kabisa ndoto za kusoma

Nikaanza kujihusisha na shughuli ndogo ndogo mtaani sasa kwakuwa nilipokuwa naishi ni kijijini hakukuwa na shughuli kubwa sana ambayo ingeweza kunisaidia Kwa upana

Nikaja nikapata changamoto ya magonjwa katikati nikaumwa lakini Mungu mwema kwasasa nimerecover Niko vzr

Hivyo naomba msaada kwa yoyote mwenye uwezo wa kunisaidia nipate kazi ya kufanya sichagui iwe ya ofisini au kokote kikubwa niweze kuendesha maisha kwani kwasasa Hali yangu ni ngumu na umri ndio unakimbia.

Note:
1: Nina uwezo wa kutumia computer kwa baadhi ya maeneo.

2: Ni mwepesi kujifunza kitu kipya na kukifanyia kazi kwa haraka

3: Ni mtunzi wa Nyimbo za dini ya kikristo ila sijapata support kutokana na mazngira niliyopo, naamini nilipata support naweza fanya kitu kikubwa.

Kwa anayesukumwa kunisaidia karibu inbox nahitaji sana msaada Mungu akubariki.🙏
Habar, ukuweka mawasiliano
 
Back
Top Bottom