Lakini vipi kuhusu kukomaa hapa hapa bongo!Kwa sababu, mara nyingi mazingira maskini yana fursa nyingi sana kuliko nchi zilizoendelea.
Namanisha, huku bongo unaweza hata kufuga kuku, kulima bustani, kuanzisha viwanda vidogo vidogo nk, tofauti na ukiwa huko Ulaya.
Mimi nilipokuwa chuo kikuu nilianza harakati za kwenda majuu nikiamini ndo kuna maisha. Kwa bahati nzuri strategies zangu zilifeli.
Nikaona isiwe shida, nikaamua kuanzisha harakati za kutafuta pesa humuhumu bongo, ili nikipata hela nyingi najua ntakwenda Ulaya kutembea na kurudi. Sidhani nikiwa na hela ya kutosha ntanyimwa visa ya kwenda kutembea.
Unajua, nilichojifunza, kwa sasa jamani hapa TZ maendeleo yanazidi kushamiri vijijini, na huko ndiko kuna fursa nyingi ambazo ni ngeni lakini zimezoeleka mijini. Kule kijijini unaweza kuanzisha, ufugaji au kilimo cha kisasa, ukafungua steshenari kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari za kata, usafirishaji ndiyo kabisaa unapiga hela mfano ukiwa na kigari kidogo tu kama Noah, Ukanzisha kiwanda cha welding, ukanzisha video shooting, ukafungua studio ya kurekodi miziki, ukanzisha maduka ya bidhaa za kichina, ukanzisha glosari au bar, mabanda ya chipsi nk. NB; Siyo vijiji vyote vina fursa tajwa hapo juu.
Tujifunze kitu;
Ilikuwaje wazungu wengine walitoka Ulaya na kuja kutafuta fursa Afrika katika karne 19? Inasemekana hao wazungu wengine walikuwa jobless na maskini huko Ulaya, hivyo Afrika ilikuwa ni sehemu comfortable kwao kuukimbia ubebari Ulaya.
Ni kwa nini wazungu hao walikubali kuja Afrika na siyo kukimbilia nchi nyingine za Ulaya? Jibu; Ukiachilia mbali ishu ya rasilimali, wazungu wengine walikuja Afrika kwa kuwa lilikuwa ni bara lenye maisha ya kimaskini kwa hiyo fursa zilikuwa ni nyingi sana.
Hivyo, tuzitoe fursa mijini na kuzipeleka vijijini tupate hela na maisha yaendelee. Ukipata hela unaweza kurudi mjini tena. Wewe wa mjini ukienda kule kijijin utabaki unashangaa maisha yalivyo cheap. Mjini unalipa kodi ya nyumba elfu 75 kwa mwez lakini kijijin utalipa elfu 10. Hautabweteka kukaa kijijini kwa sababu wewe unajua kilichokupeleka huko.
Twendeni tukazitumie fursa vijijini humu Tanzania na siyo kwenda kutafuta ajira Ulaya.
Sent using
Jamii Forums mobile app