Msaada, Naulizia power tiller zuri,lenye nguvu kwa pesa ya Mtanzania

Adolph Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
5,950
Reaction score
9,511
Wasalaam..

Heri ya pasaka kwa wakristo na waislam tuendelee na al-futar ili mradi kila mmoja afanye kinachomfaa na kumpasa..

Leo nimeamka na mood ya kuendeleza mpango wangu wa mwaka (kilimo) na baada ya kufika shambani kutazama shamba nasikitika tu, mazao ni kidogo mno, nimewaza huwenda nyenzo ninayotumia ni duni (jembe la mkono na kutegemea mvua za msimu).

Hivyo nimeamua kuanza na power tiller ambapo mimi sina uzoefu kuhusu mashine hizo ila huwa nazisikia tu na kuona baadhi ya watu wanabebea tofari vijijini....

Maswali ninayo uliza.

1-Je power tiller gani ni nzuri kwa nguvu ya kupiga kazi muda mrefu(HP) bila shida za mara kwa mara.?

2-Je ni power tiller gani ina speed ya kufanya kazi maana naona ya huku kijijini yana shindana mbio na baiskeli, ili kuokoa muda shambani?

3-Final, je naweza naweza ipata kwa gharama chini ya 6m Tz sh kama budget ?

Natanguliza shukrani...
 
Kwa Bei ya chini ya million 6 hapo utapata za kichina na kihindi. Hizo Zina speed na nguvu changamoto ni kupasua GIA box na service za Mara Kwa Mara baada ya misimu michache ya kilimo. Kama utafikia maamuzi ya kuchukua za kichina chukua amec tiller au toyo kidogo zinajikongoja Kwa muda mrefu Bei ni milioni 7-8 ikiwa complete na milioni 4- 5 bila tela.

Kwakilimo chauhakika na kudumu Kwa muda mrefu chukua Siam Kubota Kwa milioni 10 bila tela au 12 likiwa na tella.
 
Pawer tiller nzuri ni kubota tu kutoka japan achana na wachina na wahindi.. kubota budget ni mil 10 bila trailer. Complete na trailer ni mil 12
Duuuh kumbe bado nina safari ndefu
 
Kwa Bei ya chini ya million 6 hapo utapata za kichina na kihindi. Hizo Zina speed na nguvu changamoto ni kupasua GIA box na service za Mara Kwa Mara baada ya misimu michache ya kilimo. Kama utafikia maamuzi ya kuchukua za kichina chukua amec tiller au toyo kidogo zinajikongoja Kwa muda mrefu Bei ni milioni 7-8 ikiwa complete na milioni 5 bila tela.

Kwakilimo chauhakika na kudumu Kwa muda mrefu chukua Siam Kubota Kwa milioni 10 bila tela au 12 likiwa na tella.
Samahani naweza kufahamu kuhusu hao amec tiller au toyo kidogo maana hao kubota niliisha wasikia ila wana bei iliyosimama haswaa
 
Amec ni kampuni ya kihindi ambao mwanzo walikua wakitoa pawatila aina ya amec lakini zenye mikono mifupi. Pawatila zao zilikua zikidumu Kwa muda mrefu na zenye nguvu ingawa speed ilikua ndogo. Kwasasa wamekuja na amec za mikono mirefu zenye nguvu na speed Kama Siam Kubota. Changamoto yao kubwa ni service za Mara Kwa Mara baada ya miaka miwili au mitatu kutegemeana na matumizi na huduma ya oil.

Toyo ni kampuni ya kihindi ambayo hutoa mashine mbalimbali ikiwemo zakusaga, kukoboa, pikipiki, maguta na pawatila za mikono mifupi. Kwasasa nao wanayo Toyo tiller ya mikono mirefu ambayo nayo ni kama Kubota. Ubora na udhaifu hazipishani Sana na amec tiller. Lakini kwakilimo Cha mahindi tu zitakufaa Sana. Kwasababu kwenye mpunga tu huku Zina survive Kwa misimu mpaka mitatu bila service kubwa.
 
Shukrani sana na ubarikiwe huwenda nikafanya mabadiliko mwaka huu ....eeeh vipi kuhusu (HP) horse power ipi ni nzuri?
 
Toyo
download.jpg
 
Shukrani sana na ubarikiwe huwenda nikafanya mabadiliko mwaka huu ....eeeh vipi kuhusu (HP) horse power ipi ni nzuri?
Huwa zinaanzia 14-16. Hivyo nzuri za HP 14 kwani hukaa muda mrefu bila kusumbua. Zile za HP 16 husumbua hasa engine na gear box kupasuka. Vile vile zipo aina nyingi za muundo na Bei sawa na hizo usijichanganye. Kama ukikosa hizo basi jichange upate Kubota au yanmar.
 
Duuuh kumbe bado nina safari ndefu
Sio sana, zipo hadi za milioni 4 kutoka china ni wewe tu mkuu.. kwa sababu umetaka kilichobora nimekupa kilichobora... Ila kama unataka al-mradi power tiller chukua za milioni 4
 
Sikuwa na maana hiyo ila nilimaanisha pesa yangu ipo chini inabidi kuongezea
 
TRA CHANG,KUBOTA K18 Thailand...
nimetumia mwaka huu tu,Kama upo kusini njoo PM tuzungumze..
 
Kwa Bei ya chini ya million 6 hapo utapata za kichina na kihindi. Hizo Zina speed na nguvu changamoto ni kupasua GIA box na service za Mara Kwa Mara baada ya misimu michache ya kilimo. Kama utafikia maamuzi ya kuchukua za kichina chukua amec tiller au toyo kidogo zinajikongoja Kwa muda mrefu Bei ni milioni 7-8 ikiwa complete na milioni 4- 5 bila tela.

Kwakilimo chauhakika na kudumu Kwa muda mrefu chukua Siam Kubota Kwa milioni 10 bila tela au 12 likiwa na tella.
Hii ya 4&5m tunazipataje mkuu, naitaji sana maana 8/8 zililetwa 6.2m kubota bilq tela
 
Unapatikana wapi maana wanazo Kishen enterprises katika ofisi zao. Kwa detail za wanakopatikana pitia page za Kishen za insta. Wanazo ofisi mikoa mingi nchini hapa naweka za makao makuu watakuunganisha na ofisi za karibu na ulipo.
Hii ya 4&5m tunazipataje mkuu, naitaji sana maana 8/8 zililetwa 6.2m kubota bilq tela

Screenshot_20240822-050322_1.jpg
 
Vitalis Msungwite mkuu nimefika Kisheni ila amec zimeisha zipo Toyo tiller, sehemu nyingine km unazijua naomba msaada wako kulajua. Nipate ya milioni 4 au 5 zile km unapajua msaada tutani.
 
Back
Top Bottom