Msaada: Nifanyaje kuhusu matatizo haya ya gari?

Msaada: Nifanyaje kuhusu matatizo haya ya gari?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mtu anaweza kuona gari beforward bei FOB ni $200 akadhani ni rahisi,
Hajajua wazee wa meli hawajaweka chao kupata CIF,wazee wa bandari bado,na kuna wale wasioshiba wazee wa TRA,Wazee wa bima bado..lazima tu alitelekeze bandarini..
Ndio hizo hizo uzionazo subiri uje pale bondeni na kwa wazee wa long room ndio utajua ni bei rahisi au bei kubwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu humu,

Juzi nilikuwa natoka Dar es salaam na gari aina ya Toyota Porte, nikatoka vizuri Dar es salaam tulipofika Manyoni gari ikachemsha, tukaenda kwa fundi akafungua injini akasema gasket zimeungua na tena cylinder head imepinda, sasa ikarekebishwa pale ikakaa vizuri,

Tukiwa njian kulekea Singida mjini taa ya check engine ikawaka tukakagua gari tukagundua kwamba oil ilikuwa haipandi sasa tukatafuta fundi usiku ule ule akarekebisha chujio la oil kule kwenye sample,

safari ikaendelea tulipofika Nzega tukasikia kitu kama kimedondoka kusimama kuangalia, tukakuta vichuma kama piston, na inaonesha injini imefumukia karibu na sample, sasa safari ikaishia hapo.

Je, wataalam humu ndani, nifanyeje? Makosa yalikuwa wapi? Manake service nilifanya wakati naanza safari
Nakushauri mkuu nenda kwa mganga, atakusaidia kuirudisha gari yako kama zamani
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mtu anaweza kuona gari beforward bei FOB ni $200 akadhani ni rahisi,
Hajajua wazee wa meli hawajaweka chao kupata CIF,wazee wa bandari bado,na kuna wale wasioshiba wazee wa TRA,Wazee wa bima bado..lazima tu alitelekeze bandarini..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha ha gari hata upewe bure jamaa zetu wanaipangia bei ili wakutandika kodi.
 
Sijui kama ni kweli ila nna jamaa yangu ana carina ya cc1490 na ashapiga sana root za mbeya dar na huwa anaikoleza sana.
Umenikumbusha Toyota Port nilikuwa nayo ikafanya mchezo huu huu ya kwako iliyokufanyia.

Nadhani hizi gari toyota zenye cc chini ya 1700 si recommended kwa safari ndefu. Ni in town cars.

Safari ndefu inabidi uende mwendo wa kobe kwa kupumzika pumzika.

Kama ni mtu wa safari utlist pendelea cc kuanzia 2000 kwenda mbele. Ikiwa six unaenjoy safari zaidi.
 
Huyo jamaa ni mzembe Kwenye kutunza gari kwasabb kama Safar ndefu mimi mwenyewe nimefanya safar nyingi Tu ndefu na carina ti na sijapata shida yeyote njiani,mwaka Jana December nimefanya Safar kutoka DAR,Mwanza Hadi bunda na nikaingia mwibara,kisorya Hadi ukerewe na gari ilikuwa poa mwanzo mwisho..
Gari yeyote ukishaanza kutumia maji ya dawasco badala ya coolant usitegemee gari hiyo kudumu mazingira yetu
Sijui kama ni kweli ila nna jamaa yangu ana carina ya cc1490 na ashapiga sana root za mbeya dar na huwa anaikoleza sana.
Pamoja na mambo mengine, uimara wa gari hutegemea matunzo sahihi na kwa wakati. Carina Ti mostly Cc 1490, sio ndogo kivile. Nina rafiki anayo, anaishi Dar na kwao ni Sumbawanga, ameshaenda mara kadhaa ni iko sawa tu.
 
Coolant unaweza kukuta lita 1 mpaka 12000/-..
Maji ya bomba ndoo ya lita 20 jero...

So, most of the people go for the cheapest..

Sent using Jamii Forums mobile app
broh naomba elimu kidogo hapa. nakiri wazi sina uzoefu wowote na magari ila nina katoyota ist nimenunua muda na nilinunua kwa mtu. narudia sina uzoefu wa magari. nachoomba kukua hyo coolant inasaidia nini?? je ina tofauti gani na maji?? naomba elimu hapa broh! natanguliza shukrani kwako!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wengi tu wana gx 100 na gx 90...zipo barabarani mpaka sasa...full ac, full power....gari kama hizi unadhani zinakosa miaka 10+ rodini..?

Ni kweli suala la uchumi wetu duni ndiyo unasababisha yote hayo...

Lakini tukiachana na umasikini.....
Point hapa ni kwamba gari likitunzwa linaweza kukaa miaka zaidi ya 10 ilihali liliingia nchini likwa used

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni Gx 100 Chaser - Avante; yaani kama vile ina addiction flani, road trips utafurahia mwenyewe. Ila kikubwa iko well maintained.
20190527_090628.jpg
 
broh naomba elimu kidogo hapa. nakiri wazi sina uzoefu wowote na magari ila nina katoyota ist nimenunua muda na nilinunua kwa mtu. narudia sina uzoefu wa magari. nachoomba kukua hyo coolant inasaidia nini?? je ina tofauti gani na maji?? naomba elimu hapa broh! natanguliza shukrani kwako!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Coolant haichemki haraka kama maji
Maji yanaleta kutu kwenye rejeta na baadhi ya sehemu ndani ya engine(maji yetu yana chumvi kiasi fulani)
Ushauri: Usiweke maji kwenye rejeta weka Coolant.
 
broh naomba elimu kidogo hapa. nakiri wazi sina uzoefu wowote na magari ila nina katoyota ist nimenunua muda na nilinunua kwa mtu. narudia sina uzoefu wa magari. nachoomba kukua hyo coolant inasaidia nini?? je ina tofauti gani na maji?? naomba elimu hapa broh! natanguliza shukrani kwako!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Coolant ni kiminika chepesi tu kama maji, kinawekwa kwenye radiator ya gari ili kupooza injini..

Coolant imeongezwa chemicals ambazo zinasaidia yafuatayo..

1. ...Njia za maji kwenye radiator na injini zisishike kutu na kupelekea kuziba au kutoboka.

2.....Chemical hizi hufanya coolant iwe antifreeze....yaani isigande na kuwa barafu kwa wale wanaoishi kwenye nchi za baridi.

3....Chemical hizi hufanya coolant ipoe haraka kuliko maji pale inapofikia maximum temperature...feni itafunguka na kupooza kupunguza joto la coolant inayozunguka ndani ya radiator.

4.....Coolant haina tabia ya ku..evaporate kama maji ya bomba....hivyo kama radiotor haivuji, unaweza kukaa muda mrefu sana bila kiwango cha coolant kupungua..

Hizi coolant huwa na rangi ya Kijani, Blue au Nyekundu kutegemeana na aina ya gari.....Hizo ni rangi tu, kinachomata ni uwiano wa mchanganyiko wa chemicals zilizotumika kutengeneza coolant hiyo..

Kwa sababu hizi, coolant inapooza injini vizuri kuliko maji, hivyo unakuwa na uhakika wa kuilinda Cylinder head yako..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
broh naomba elimu kidogo hapa. nakiri wazi sina uzoefu wowote na magari ila nina katoyota ist nimenunua muda na nilinunua kwa mtu. narudia sina uzoefu wa magari. nachoomba kukua hyo coolant inasaidia nini?? je ina tofauti gani na maji?? naomba elimu hapa broh! natanguliza shukrani kwako!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Coolant ni liquid ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kuweka kwenye radiator(rejeta) ya gari ili iweze kupooza injini.
Kuna faida kadhaa za kutumia coolant kuliko kutumia maji. Faida ni:-

1. Coolant inafanya kazi katika wide range of temperature ukilinganisha na maji hivyo ina uwezo mkubwa wa kulinda engine yako kuoverheat kuliko maji ya kawaida.

2.Coolant ina kitu tunaita rust inhibitor ni additive ambayo ipo kwa ajili ya kuzuia kutu {rust}.

3. Coolant ina lubricate waterpump.

Kwa hiyo siyo vizuri sana kutumia maji.
 
Back
Top Bottom