Msaada nifanye nini niwe na amani?

assalam wanajamvi? bila shaka mpo salama na mnaendelea vyema na majukumu!
Acha kujiliza mkuu, pambana wewe ni mwanaume. Hiyo kampuni kwani ni ya baba yako? Anza kuchakarika kutafuta kazi nyingine upesi sana na kwa kasi. Shida ya kukaa kampuni moja miaka kibao hadi unazoeleka na kuonekana huna jipya tena.

TAFUTA KAZI SEHEMU NYINGINE, KISHA UKIPATA U RESIGN HAPO UPESI. Ujifunze sasa, usikae tena organization moja muda mrefu unless ni kampuni yako au ya baba yako, kukaa kampuni moja muda mrefu ni recipe nzuri sana ya uvivu, uzembe, majungu,kufanya kazi kwa mazoea (business as usual) na maslahi (mshahara) hafifu.

Mimi sehemu niliyokaa sana nilikaa miaka mitatu. Kampuni zingine zote ni kati ya mwaka mmoja hadi miaka miwili, nimeishia zangu...!!Unaondoka kila mtu anasikitika anataka ubaki. Kanuni yangu nikianza tu kazi, baada ya mwaka mmoja naanza kutafuta kazi nyingine.
 
Pole. Tulia kwanza upone. Mambo ya kupigania vyeo kwa sasa yape kisogo. We hakikisha kwanza ugali unapatikana huku hali yako ya kiafya ikizidi kutengamaa. Ukisha kaa sawa ndio mengine yatafuata.
 
Hiyo sio ofisi, hiyo sio kazi bali ni mishe mishe
 
Pole sana kwa kuumwa, Mshukuru Mungu kwa kupata nafuu.
USiache kazi kama hujapata kazi nyingine.
kama Bosi hakusumbui hao wengine unawalia jiwe. Endelea na kazi kampuni ilipe kodi
 
Well
 
Pole..usifanye move mpaka uwe na plan B
 
Achukue huu ushauri utamsaidia Sana
 
Mkuu nimekupa like aisee
Umemalizaa
 
Pole sana kwa yote, usiondoke kabla hujapata kazi sehemu nyingine.
 
Kwanza pole sanaaa,na utakuwa sawa kwa uweza wa Mungu.
Adui akimbiwi,fanya maombi ya nguvu sana afu Kama we n mkristo Kila ukisali mda wowote au ukijiona mpweke una maumivu sali zaburi hii ya 35 kwa imani utajibiwa.Kuwa msiri sana na mambo yko usiwape nafasi wajue taarifa zako.
 
Usiache kazi!!
 
Pole kwa ajali ndugu yangu, lakini kuhusu changamoto za kazini kwako ni kawaida na zivumilie na anachokisema huyo mkuu wa idara ukute ni kweli bila yeye ungefukuzwa so shukuru endelea kupiga kazi unaweza rudi juu tena ila ukijicjanganya kuacha kazi eti kisa hakuna amani sio rahisi kupata tena kazi na hata ukipata hayo mazingira ya amani yanaweza yakafanana tu kati ya hapo na unapopataka kwaiyo piga kazi you'll bounce.
 
Kwanza pole sana kwa yaliyokupata, naandika kwa herufi kubwa "USIACHE KAZI" pasipo kupata kazi sehemu nyingine. Pia tambua kila penye riziki mambo ya majungu hayokosekani.
Habari yako imenigusa sana, kwani nami napitia changamoto hizo hizo mpaka muda huu nipo kitandani. Nilipata ajali ya gari nikavunjika nyonga ikabidi nifanyiwe upasuaji wa kubadilishwa nyonga. Tatizo linakuja ninayoyasikia yanayoendelea huko kazini yanaumiza sana.
 
Mkuu pole sana ila kabla ya kuacha kazi endelea kutafta kazi ukiwa hapo hapo. Ukipata kazi aga vizur ondoka . Mimi nilisha fanyiwa figisu na jamaa kwenye idara ila nikavumulia na nikatafta kazi nikapata kampuni kubwa zaidi.

Kwenye ile kampuni baada ya miez 9 nikapewa idara ya kusimamia na mwaka mmoja badae mmoja wa walionifanyia figisu alikuja kwenye interview akanikuta kwenye panel. Haya maisha usilipe kisasi mwachie Mungu atapambana nao. Wanafki makazini wanaishiaga papaya sana
 
Kwanza kabisa pole na hali uliyo nayo, cha pili mkuu usije ukajaribu kuacha kazi wakati hujapata kazi nyingine, kama unaona hapo kero zimezidi tafuta kazi kimya kimya huku ukiendelea kukomaa hapo kwa mudaa. Ila usiache kazi kwa kusudi la kuanza kutafuta kwingine!
 
Ukisikia mitihani ya maisha ndo kama hiyo sasa,kila mtu anapitia wake wa kwako ndio huo
Dawa ya mtihani ni kukaa na kuusolve na sio kuukimbia mana mwisho wa mtihani watu hupata matokeo!
Baki hapo uumalize huo mtihani huku unatafuta kazi kwingine,ukipata kwingine wakati huko hapo then utajua kuwa majibu ndo hayo na ukikosa pengine utajikuta umeshazoea hiyo hali na umeona kawaida hence utapata amani!
Ila usiache hiyo kazi kwanza,utajiongezea mtihani wa pili wakati wa kwanza hujausolve bado!
 

Endelea kuwa na Utulivu.

Usiendeshwe na mitazamo ya Watu au maneno ya Watu.
Kubali na kabili kila hali inayotokea katika Maisha yako

Pole Sana Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…