Msaada: Nilipata ajali mkono wa kulia haufanyi kazi japo nafeel

Sijui pia umeumiaje ila huku niliko Kuna wataalamu wa tiba za jadi huwa wanaunga mifupa iliyovunjika nimeshuhudia kabisa kijana aliyevunjika mguu kabisa Leo hii anacheza mpira tena
Waganga wa tiba za asili (Herbalists) wanasaidia sana kwenye inshu za mifupa.

Watu wakishafika miaka 30 na kuendelea mifupa huwa imekomaa sana na kuwa changamoto kupona kwa tiba za hospitalini, nimeshuhudia hili mimi mwenyewe.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Sijui pia umeumiaje ila huku niliko kuna wataalamu wa tiba za jadi huwa wanaunga mifupa iliyovunjika nimeshuhudia kabisa kijana aliyevunjika mguu kabisa Leo hii anacheza mpira tena
shukrani mkuu, mifupa iko ok ni ya kunyoosha yes, hivyo nikitoja huku takudm uniconnect nije huko uliko wanishulikie pia
 
Kama kweli uligongwa na treni mkuu shukuru sana Mungu ni mzima aisee , japo Mungu atakurudisha katika hali Fulani itakayokuwezesha kuishi
kabisa, kila mtu haamini kama hata niliweza kuamka, cas niliwekewa oxygen nachine hata faham sina, nakuja kufungua macho madocter wanashangaa cas nmekaa 3 weeks kana nmekufa hata nacho sifumbui so ni Mungu tu
 
asante sana kiongozi, tafanya hivo kadri niwezavyo cas cna namna ilimradi nipone
 
Tiba zipo ila unaweza kupona au i
 
Kwanza ningependa umshukuru Mungu kwa kuendelea kukupigania na kukupa nafasi ya uhai ambao ni kitu cha thamani sana kwako......

Lakini pia lazima tujue kuwa sisi wanadamu hapa Duniani mitihani ni sehemu ya maisha yetu......kwa kuwa maana ya maisha ni muunganiko wa shida,raha na misukosuko ya kila aina......hivyo tunavyokutwa na majambo yawe mazuri au mabaya utulivu unahitajika wa nafsi ,mwili na akili...........

Tunajua kuwa unapitia magumu kibinadamu kwa kuwa hali hiyo imepelekea kusimama kwa mambo yako mengi ya kimaisha lakini jambo la msingi kwa sasa ni uzima wako tu.......

Kitu ninachokuhusia kwa sasa usipanik bali unatakiwa utulie huku ukifuata ushauri na maelekezo ya wataalamu wanaokutibu au kukuhudumia...........

Lipokee tatizo kwa moyo mkunjufu huku ukiangalia namna njema na Bora ya kulitatua....... kwenye kulitatua kuwa na msimamo usiyumbe yumbe kwani kutokuwa na msimamo kunakufanya kuwa fursa kwa wajasiliamali wa dawa waliojaa mitandaoni...........

Naamini tatizo lako sio kubwa na Mungu atakuponya............
 
asante sana kiongozi, tafanya hivo kadri niwezavyo cas cna namna ilimradi nipone
Shukuru Mungu hata unatembea
Kuna waliopata ajali hata kujilisha chakula hawawezi.

Hilo la kuogeshwa ni suala la kawaida sana mtu unapouguza majeraha,japo linaumiza kwa namna nyingine ila yakupasa tu ushukuru Mungu kwa uhai aliokuachia.

Baadaye utaanza kushika mswaki,taratibu tu hivyohivyo,mara utanyanyua jag,baadaye kikombe.
Nenda tu taratibu kwa stage.
Yaani usiuonee huruma mkono,ukunjue,,utauona kama mzito ila kamwe usiubebelee..ukunjue hivyohivyo.
Ukikubali kuuacha unalemaa mazima.
 
Nimekurupuka ilihali nimekueleza kwa usahihi alichokiandika? umepaniki vizuri sana [emoji1]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Kuna watu mnakaza fuvu, swala la wewe kunieleza kiufasaha haihusiani na kile ulicho comment kwangu.

Rejea #29 uone alivyosema kuwa amefanya update.

Sasa wewe unakuja kunilaumu kuwa sikusoma ikiwa yeye hakueleza hiyo report mwanzao, mpaka pale alipoulizwa akafanya update.

Sasa kosa langu liko wapi ??
 
Brachial plexus injury tafuta physiotherapist atakusaidia

Angalizo damage ya Mishipa ya fahamu huchukua muda kupona, hivyo basi ili kupata matokeo mazuri uvumilivu unahitajika.
 
Pole sana

Nikweli hapo kweli ishu ni taarifa hazifiki.

Ninae ndugu yangu ana shida kama hiyo, japokua yeye hakupata ajali yoyote, ila ana ganzi mikononi hawezi kushika kitu, muda mwingine hata akiumia hajui kama kaumia mkononi mpaka aone damu ndio anashtuka.

Vipimo vilionyesha mishipa imebamwa kwenye upande wa shingoni kwa nyuma, pendekezo la madaktari bingwa ilikua ni upasuaji kuipa nafasi mishipa iliyobanwa.

Changamoto nyingine ni maumivu anapata kwenye mikono, inauma tu yenyewe.

Nadhani case zenu zinafanana kwa kiasi fulani.
 
Pole sana,hakika hujafa hujaumbika.Pole sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…