Msaada: Nilipata ajali mkono wa kulia haufanyi kazi japo nafeel

Amen mkuu, asante sana kwa ushauru huu mzuri, mungu anisimamie
 
Pole sana mkuu! Hiyo mishipa ya fahamu ni shida sana kwa kweli, ingawa mimi siyo dr ila kuna dogo wakati wa kuzaliwa alikuwa mkubwa sana, so kutoka haikuwa rahisi na operation haikuwa option alipata injury ya mkono ambapo baada ya kusoma sana online pia nilitambua inaitwa "brachial plexus injury", pia huwapata watu wazima wakipata ajali ambayo inahusisha sehemu za shingo, bega au kwapa. Jaribu kusoma online kupata taarifa zaidi. Pole mkuu
 
my God😥 nmeona mkuu, nmesome wikipedia, dah guys nipone aisee, inatisha, hadi nmetetemeka
 
Hii ni theory yangu.
Kwanza hiyo Hali ni aina ya paralysis, na kama inavyojulikana Hali hiyo hutokea Kwa sababu mbalimbali.
Ajali ikiwa ni sababu Kuu basi kwako na pia tukiangalia undani wake ambao ni kuwa paralysis huchangiwa na mambo makubwa mawili upungufu wa madini calcium/organic calcium ambayo hupelekea harden of arteries/mishipa ya damu kuminywa na kufanya mzunguko wa damu kutofanyika vizuri ktk maeneo mbalimbali ya mwili ,ndio maana wengine hupata stroke au kutohisi seheme ya kiungo ktk mwili.
Baada ya kujua Hilo basi ni lazima tufaute njia za kurudisha hiyo calcium na pia fanya damu iwe nyepesi/blood thinning Ili kuwezesha damu kusafiri vizuri.
Mimi ni muhuburi wa dawa Halisi /Naturapath hivyo.nitashauri baadhi ya mambo uyafanye ,
Tafuta capscum/cayenne pepper/pilipili (unga wake) tumia ktk maji ya moto mara nyingi uwezavyo hata mara 4 Kwa siku.
Cayenne Ina dawa inayoitwa capscin ambayo ni maalum Kwa blood thinning kama vile aspirin na pia hubalance mapigo ya moyo Kwa waliyo chini kupanda na yaliyo juu kushuka ,so ni perfect Kwa aina mbili za blood pressure pia.
Calcium ambayo hufanya arteries mishipa kusinyaa ni sehemu ya matibabu Yako na hii ni vizuri iwe katika organic form na mmea wenye hiyo Kwa wingi ni Comfrey.
So ukipata chai yenye majani ya comfrey na cayenne pepper hizo ni Tiba tosha Kwa maswala yote yanayo husiana na paralysis.
Zaidi unaweza kufanya dawa ya kuchua huo mkono Kwa kutumia hiyo cayenne na mafuta ya nyonyo/castor oil ambayo hupenye haraka katika nyama kufikia mishipa ya damu.,hii SI muhimu sana kama ila support ya hiyo Tiba ya juu.
Good luck bro.
 
Asante mkuu, naomba Mungu nirudi kuwa sawa, mazoezi nafanyiwa isipokuwa huu mkono wa kulia haufanyi chochote hata vidole havifanyi kitu, hivyo ni kazi sana, imagine naogeshwa cas siwezi jiogesha, dah is painful kiukweli, nipone tu
Jipe moyo mkuu utapona tu. Issues za nerves huwanzinachukua muda mrefu sana kurudi katika hali yake. Uko kospitali gani hiyo mkuu? Kama utakuwa hizi hospitali zetu kubwa hizi onana na physiotherapist wa hapo huwa wana mitambo ya kustua nerves wanakuwa wanakufanyisha mazoezi kila siku kwa muda kama mwezi hivi. Kijana wangu naye alikuwa na shida ya mgongo alikuwa hawezi kukaa karibia kama mwezi hivi akapewa ratiba ya mazoezi hayo. Muda mfupi akapata nafuu sana!
 
wakuu habari zenu.
Dah nilipewa majib juzi sema nilikua stressed kiasi hata skuingia online😩

nilikutana na docter bingwa wa mishipa ya fahamu na mifupa, kaniambia wamefanya vipimo vyote , shida ni mbili tu, mifupa iko ok so inahitaji mazoezi tu ya kutosha itakaa sawa ba kunyooka tena japo uvumilivu muhimu cas inahitaji muda kidogo😢.
Pili ni mishipa ya fahamu ya right hand ndio imepata hitilafu, wanfeweza suggest operation but operation sio solution sahihi, hiyo nerves kupona yenyewe taratibu so it depends, inaweza chukua,4 weeks, or miezi 3, 6 au hata mwaka😢 it depends, so ameniandikia dawa za kutumia ili kupunguza pain ya mifupa ya mikono, kuondoa ganzi nk , so ameaisitiza kuwa mtulivu na kuzngatia nazoezi tu.

Wakuu naskitika sana, yani sjui tapona lini,,yani kweli my life iishie hivi kweli? bora ajari ingeniua nmeumia sana

Japo kuna doc mmama alisema kijana issue,za mishipa ni,comppicated kiasi hivo nijaribu pia watu wa dawa za qsili watu hua wanapona hata huko cas ameona watu wakiaaidiwa kutibiwa mifupa, mishipa ya fahamu nk.

Wakuu nisaidini please ntumie dawa gani za asili kusaidia, pengine unafahamu mtu ambae husaidia hivi vitu nielekeze mkuu, cas at least nijaribu tu maybe ztasaidia, nisaidieni, naumia sana😩
 
Anaendelea aje hadi sasa mkuu? angalau nijue ameweza vipi kua ok
 
asante, wacha nimuone aniassist
 
Pole sana mkuu.

Endelea kutumia hizo dawa unazopewa hapo hosipitali kwa matumaini na imani ya kupona wakati unatafuta dawa mbadala.

Kumbuka; hofu huumiza kuliko ugonjwa wenyewe.
 
Pole sana mnyakyusa wa IPinda. Tafuta kiungo fulani kinaitwa Star Anise, kinapatikana kwenye maduka ya dawa asilia au sokoni kwenye eneo wanakouza viungo vya chakula. Saga kwenye blender ya vitu vikavu, tumia kijiko kimoja cha chai level kwenye chai ya rangi au uji au juisi. Ukiwa na asali ni vizuri zaidi, kutwa mara tatu. Ni kiungo cha chakula hivyo huhitaji kwenda njia panda kutambika. Tumia bila kukata tamaa, kisha utatoa update hapa✌
 
Sijui pia umeumiaje ila huku niliko kuna wataalamu wa tiba za jadi huwa wanaunga mifupa iliyovunjika nimeshuhudia kabisa kijana aliyevunjika mguu kabisa Leo hii anacheza mpira tena
Wapi mzee ?maana nilishawahi kusikia ni sehemu inaitwa kibibino kwa wadigo...Nataka kujua na huko maana kwa jamaa alipelekwa mguu ulisagika alikuwa bodaboda alipona kabisa walimuunga ila ilikuwa mwaka 2013 -2014.
 
Hujui kiswahili vizuri? Unachanganya lugha ili iweje? Au ugonjwa wako hautaki kiswahili?
 
Umewezaje kuandika text humu kama mkono haufanyi kazi
Hajapoteza kumbukumbu bali ni mkono mmoja wa kulia ndio umesizi.

Halafu hatumii kalamu kuandika humu bali ana bofya herufi moja moja kwa kutumia mkono wa kushoto kupitia dole gumba. Ila hii inahitaji simu isiwe kubwa sana.

Kwa taarifa tu, hii komenti yangu nimeiandika kwa mkono mmoja wa kushoto huku simu nikiwa nimeishika kwa vidole vinne na dole gumba ndilo linabofya.
 
Pole sana mkuu jitahidi kusikiliza ushauri wa madaktari na kufanya mazoezi na kuomba Mungu utakaa sawa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…