Msaada: Nilipata ajali mkono wa kulia haufanyi kazi japo nafeel

Umewezaje kuandika text humu kama mkono haufanyi kazi
Mimi mwenyewe nilivunjika mkono wa kulia mwezi Julai,2023. Na nilianza kuandika kwa mkono wa kushoto ingawa ni ngumu sana. Kwa hiyo kuumia kuvunjika mkono wa kulia hakukuzuia kutumia simu kuandika.
 
Pole sana kamanda ,cha muhimu fanya mazoezi na kusikiliza kila Madr. wataamua. Mimi mwenyewe hapa nilipo bado mkono wangu wa kulia haujanyooka na siwezi kunyanyua kitu, maana nilipata ajali mwezi wa saba,2023. Lakini mimi nilivunjika mfupa moja tu, nikawekewa chuma, naendelea kufanya mazoezi ingawa vidole bado vinauma na havijanyooka vizuri. Ni changamoto kubwa sana maana siwezi kuoga mwenyewe.
 
Kukata tamaa ni dhambi Mungu yupo atakuponya. Mimi nilishawahi kupata shida kama yako nilipooza mguu wa kushoto sababu nikosewa kuchomwa sindano mchomaji alichoma kwa bahati mbaya kwenye mshipa wa fahamu. Nilizima kabisa mguu kila hatua ya mwanadamu nilianza kujifunza upya kuongea, kukaa, kusimama, kutembea nk. Nimepona sasa ni mzima natembea ila uponyaji wa mishipa ya fahamu si wa haraka zingatia vyakula asili, herbs, mazoezi na maombi.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Miaka ya 90's ndugu yetu mmoja alifanyiwa upasuaji kwa Dr. Kairuki pale pale Mikocheni nadhani na mwyewe enzi zake. Alipona kabisa.

Ulikuwa mishipa ya fahamu kama wewe na alifanyiwa shingoni.
 
Pole sana kwa Changamoto hizo;
Jambo moja kubwa elewa kwamba hakuna changamoto mpya chini ya jua na uzuri sasa dunia sasa ni kijijini am sure in very near future changamoto yako itapata utatuzi kwa sababu si mpya hata kidogo.

Pata kwanza ushauri wa kitabibu ikiwa watashauri mfano eneo lilikopata changamoto kuwa linashtuliwa kwa maana na ku-message wapo wapemba fulani maeno ya kigamboni waliwahi nisaidia kumkanda ndugu aliye-pooza hadi akakaa sawa ingawa ilichukua muda kidogo.

Wanayo huduma ya kufuata mgonjwa pia ingawa inahusisha gahata kama za nauli etc. Nasisitiza pata kwanza ushauri wa kitabibu then kama itahitajika hii ya kukandwa basi nitakupatia Number zao!
 
Kwenu wana JF, najua madoctor mmo humu, tatizo hili linaweza tibika? Sababu nimechoka wakuu, nimekaa hospital since March seriously.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu unaweza niambia nizingatie hass which herbs? au vyakula gani vya asili nizingatie? niambie ili nitumie zaidi , zinaweza saidia pia
 
Kama zimenyofoka ndani ya pingili za shingo. Huwa ni ngumu kidogo lakini Kama zimekatika nje ya pingili utafanyiwa neuro surgery zitaungwa. Kikubwa kaza moyo ondoa woga utapona

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Mungu yote yanawezekana kwa yeye amuaminie na moyoni mwake asiwe na mashaka.
Damu ya Yesu ikutendee mema.

So painful but be stronger 💪
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…