Msaada: Nimefikia hatua ya kunywa Pepsi 4 kwa siku, nifanyeje kuacha?

Msaada: Nimefikia hatua ya kunywa Pepsi 4 kwa siku, nifanyeje kuacha?

Mlevi anamshauri mnywa soda aache soda nae mnywa soda anamshauri mnywa pombe aache pombe... Mifumo yao ya ndani ikishazidiwa na hivi vitu matatizo yao yanafanana.
 
Ni ulimbukeni tu
ni mtu kuishi ndoto zake. unaeza kukuta kabla hajajipata alikuwa anazitaka izo soda ila walezi wake wakawa wanabana. sasa kajipata hamna mambo ya breki tena. si umeona anakwambia huwa soda zinajaa kwenye friza. kwa sasa hamna namna acha anywe tu sisi tutashiriki matanga yake.
 
Mimi sidhani kama sukari inasababishwa na kunywa Pepsi,

Mimi nakunywa Pepsi hata 7 Kwa siku lakini nipo fit.,mwaka wa 5 sasa.

Napima magonjwa yote Kila mwaka na Sina hata kiluwiluwi..
Vipo.vingi vya kuleta sukari lakini sio Pepsi.

Nasema ALHAMDULILAH.
 
Ndio maana umekuwa kipipa, kwa pepsi 4 daily, kilo 93 ni kawaida. Jitahidi uache masoda sio mazuri kabisa lwa afya.
 
Nilikuwa na mtindo wangu wakipekee sana juu ya pepsi, nakunywa mbili, moja ya kukata kiu zile gulp (fundo) za haraka yaani 3 na fundo la Nne namalizia kukata ile hamu, chupa inayobaki sasa ndo kupigia stori. Kreti zinakaa pepsi tupu 😂

Nilionywa na wataalamu afya nikaufyata mwenyewe...mbadala sasa ni maji na juice tu
 
Mkuu!

Unaharibu figo na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula!

Nilimpoteza rafiki mwaka wa pili chuo kikuu!!alikua mnywaji sana wa pepsi!

Kunywa chai badala ya pepsi!
Ahsante kwa nasaha, nipepunguza sana, watu wanaonifahamu wameshangaa nimewezaje !
 
Duh! Noma sana

Mimi mara ya mwisho kunywa soda juice za viwandani na zile energy na vingine vya namna hiyo ni 2015
 
Pepsi kijasho sio mchezo.

Amua toka ndani kuwa naacha na maanisha..

Mwaka 2016 January kama hivi niliamua tu kwamba na quit soda hasa hiyo Pepsi kijasho na ikawa hivo.

Sweet poison sio mchezo. Kuna muda usipokunywa kichwa kinauma unapata wenge kabisa. (ushakuwa tejaa... tena Teja wa Pepsi)

Njia nyepesi ni kujilazimisha kutumia mji kama mbadala.

Weka nia toka ndani kuwa imetosha sasa kuendeshwa na kiu na unanze kuiendesha kiu yako.

Pepsi dare for more( Hawa jamaa wanauza sana kuliko Coca na hii ni tathimni yangu kwa mikoa kadhaa. Sijui kwanini Coca wamekuwa walegevu sokoni. 😅)
 
Sijafika Iko Niko kwenye late 20'
Binti mdogo bado, afya yako ni muhimu sana. Pumguza taratibu hadi uache, walau basi moja kwa siku inatosha sana, then hizo kilo zishuke kidogo. Jaribu kutokula usiku utashangaa matokeo yake.
 
Binti mdogo bado, afya yako ni muhimu sana. Pumguza taratibu hadi uache, walau basi moja kwa siku inatosha sana, then hizo kilo zishuke kidogo. Jaribu kutokula usiku utashangaa matokeo yake.
Nimeshaanza diet mkuuu...hii kutokula usiku unafanyaje ili usiskie njaaa
 
Nimeshaanza diet mkuuu...hii kutokula usiku unafanyaje ili usiskie njaaa
Kula vizuri asubuhi na mchana, usiku kula matunda na/au mbogamboga, kama vipi kunywa juice. Fanya hivyo kwa mda ili tumbo na mwili uzoee, baadae utashangaa tu ham ya kula usiku inapotea. Hii itasaidia saba kupunguza uzito wako. Hata mimi uzito ulipanda hadi 90s ila baada ya kuamua kuacha kula usiku nimeona tofauti kubwa.
 
Sawa nitafanya ivi
 
Nilikua nakunywa 2 kwa siku hasubui ndo chai yangu gafra najiona nanenepa na kitambi kinakuja
Sasa hivi nimepunguza moja kwa siku
 
Back
Top Bottom