Habarini za mchana,
Wakuu mimi huwa situmii pombe, ni juice na soda tu na soda yangu pendwa ni Pepsi.
Kila siku huwa nakunywa Pepsi tena napenda ikiwa baridi sana. Nilianza kunywa moja kwa siku, ikaja mbili ikaja 3 now nakunywa nne kwa siku; mbili mchana na mbili usiku. Hizo mbili nakunywa kwa mpigo.
Nifanyeje ili kuacha? Pia Mimi sio mpenz wa chai asubuhi, niko radhi nile vitafunwa vikavu au na maji au soda, na usiku siwezi kulala bila kunywa maji baridi-huwa nalala na jug la maji pembeni.
Nikinywa maji baridi akili huwa inarelax, nalala kwa haraka tofaut na nisipokunywa maji. Nifanyeje?
Soda za Pepsi na Coca kwa sasa zinawekwa kahawa. Kahawa ina nafasi ya kwenda kusisimua ubongo kupitia sehemu ya furaha kwenye ubongo.
Kwa kadri unavyoendelea kutumia kwa wingi ndivyo unavyofanya sehemu husika kuitegemea kahawa ili mwili kuwa wenye uwezo kutimiza majukumu yake.
Pia, kwa upande mwingime, matumizi haya yanaweza kuwana matokeo ya ukosefu wa madini au vitamini mwilini. Kama inavyotokea kwa watu kula mkaa, udongo au barafu. Hivyo tathmini nzuri inahitajika kufanyika pia kwa upande huo.
Kumbuka:
Kahawa : Huweza kukufanya uwe macho mda mrefu na mwenye nguvu, ila inaweza kukufanya pia kuwa mtu mwenye wasiwasi, usingizi usiotosheleza/mang'amung'amu au usipate kabisa nk.
Matokeo yake ni:
1: Utegemezi kwenye chanzo cha kahawa.
2: Mapigo ya moyo kwenda mbio. Kunakuwa na hatari ya kupata mapigo ya moyo yasiyoendana na hali yake ya kawaida. Ugonjwa wa moyo unaweza kuanzia hapo.
3: Kuwa na kiasi kikubwa cha sukari mwilini, na pale kongosho litakapochoka/litakaposhindwa kutoa kiasi hitajika cha homoni ya insulini utakuwa na tatizo la kisukari.
4: Kuongezeka uzito.
5: Kuongezeka mafuta kwa wingi mwilini.
6: Tatizo la mishipa ya fahamu.
7: Tatizo la figo.
8: Tatizo la macho.
9: Unaweza kujikuta kuwa mtu mwenye wasiwasi uliopitiliza au hata msongo wa mawazo kwa mambo yako kubadilika au kutokwenda vyema.
Nini kifanyike?
1: Jitambue kuwa hali hii si njema kwa mustakabali wa afya yako na maisja kwa ujumla.
2: Fika kituo cha afya kupata vipimo na ushauri.
3: Anza zoezi la kupunguza kiasi na si kuacha mara moja. Unaweza kujipa muda wa kupunguza kiasi cha soda 2 kwa wiki na baada ya hapo unapunguza tena na mwisho kuacha mazoea ya matumizi husika.
4: Tafuta kitu mbadala ya soda ambacho hakitakuwa na athari ya moja kwa moja kama: kupata matunda na maji ya kutosha au mlo kamili.