Msaada: Nimehamisha fedha kutoka Benki kwenda M-Pesa yenye makosa, nifanye nini?

Msaada: Nimehamisha fedha kutoka Benki kwenda M-Pesa yenye makosa, nifanye nini?

Kimla

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2008
Posts
3,810
Reaction score
6,599
Ndugu wanabodi,

Nimehamisha kimakosa fedha kutoka account ya benki kwenda M Pesa ya mtu lakini nikawa nimekosea. Nimepiga customer service ya benk kwa sasa wamefunga na nikipiga voda 100 imeishia kunipeleka Wassap.
 
Hapo majanga,kama ameishazitoa,Voda hawana msaada,inabidi umtafute huyo mtu uongee naye akurudishie.Niliwahi kumtumia mtu 76 k,baada ya Voda kushindwa kusaidia nikamtafuta akamipiga sound mwishowe alinirushia 26 k kwa taabu Sana. Nilikula hiyo hasara mpaka nikashiba.
 
Hapo majanga,kama ameishazitoa,Voda hawana msaada,inabidi umtafute huyo mtu uongee naye akurudishie.Niliwahi kumtumia mtu 76 k,baada ya Voda kushindwa kusaidia nikamtafuta akamipiga sound mwishowe alinirushia 26 k kwa taabu Sana.Nilikula hiyo hasara mpaka nikashiba.
MAISHA HAYA..SIJUI NIMEKOSEAJE,, YAANI HATA JINA SIKULIONA, UNAWEZA KUHISI JAMAA ALIKUWA ANAULOZI
 
Kama namba uliokosea kutuma haitumiki Pesa yako itarudi japo kwa kuchelewa sana.. ila kama inatumika inakua mtihani hapo unaweza kuta nae ameshazitoa.
 
Wasiliana na mtandao wa yule uliyemtumia, watauzuia muamala, na utapata pesa yako within 72 hours
 
Nahisi vodacom huduma kwa wateja kuna shida hawapokei simu kwa haraka.
 
Kuna mmoja alikosea internet banking alihamishia kwenye account ya mtu asiyemjus. Bank walisema ni makosa yake.

Hilo tukio lilinichelewesha sana kuwa na internet banking.
 
Umenikumbusha mbali mkuu Niliwahi kukosea kutuma pesa nilikuwa natoa M Pesa napeleka Bank nikakosea namba ya akaunti ikaingia kwa mtu mwingine!!

Halafu nilikuwa nimefulia vibaya,nilihangaika kweli kuipata ile hela nikienda huku wananiambia niende huku basi tabu tupu,lakini baadae ilirudi baada ya kama wiki 2 hivi nikiwa tayari nimeshakata tamaa!!

Usichoke kufuatilia!!
 
Pole sana, kwani hawana option ya kusitisha muamala uliyotumwa...
 
Ndugu wanabodi,

Nimehamisha kimakosa fedha kutoka account ya benki kwenda M Pesa ya mtu lakini nikawa nimekosea. Nimepiga customer service ya benk kwa sasa wamefunga na nikipiga voda 100 imeishia kunipeleka Wassap.
Bilion ngapi? Ndio tukushauri. kama hizi za kawaida, uchune tu. wala haina noma
 
Voda washenzi sana!
Nilikosea kutuma pesa ( mimi nilitumia M-pesa) nilituma kwenda Tigo pesa.

Nilipogundua nimekosea niliwapigia voda wakaanza kunizungusha.

Ikabidi niwapigie Tigo, haikuchukua muda pesa ikarudi ( kipindi kile hakukuwa na option ya kurudisha muamala)

Ilikuwa ni Tsh. 500,000/=

Voda hawana la maana!
 
Back
Top Bottom