Msaada: Nimehamisha fedha kutoka Benki kwenda M-Pesa yenye makosa, nifanye nini?

Msaada: Nimehamisha fedha kutoka Benki kwenda M-Pesa yenye makosa, nifanye nini?

Kimbia kwenye vodashop iliyoribu nawe wataizuia hiyo pesa na itarudi kwako baada ya muda
 
Ndugu wanabodi,

Nimehamisha kimakosa fedha kutoka account ya benki kwenda M Pesa ya mtu lakini nikawa nimekosea. Nimepiga customer service ya benk kwa sasa wamefunga na nikipiga voda 100 imeishia kunipeleka Wassap.
Hapa wanaotakiwa kukusaidia ni watu wa bank maan pesa imetoka kwao kwenda kwenye mpesa hivyo wenye uwezo wa kureverse muamala ni hao wa bank
 
mwaka juzi laki tisa 🙁🙁🙁 zilienda niltuma saa tisa nikakimbia kufika bank fasta nakuta wamefunga kumi jioni inaenda 11 siku yapili blaah nyingi jamaa aliwai kuzitoa jina nakumbuka mpaka kesho anaitwa RAJABU KISUNDA ni tapeli narudi tigo wanasema hawawezi nisawiliane na bank hapo bank pamefungwa tayar maana nilishaenda

ila kwa vile jamaa ni tapeli alitoa mda ule ule siku ya pili kufika bank wanwasiliana na tigo pesa pesa inaonekana ilitolewa baada ya dk 5 mbele wnamtrack mpaka wakala wapi ile line jamaa haikupatikana tena tangu siku ile
 
Pole sana! Ogopa kufanya muamala wowote unapokua na stress au shauku na haraka ya kufanya/kujua kitu. Utakuja kunishukuru.
 
Mbaya zaidi bank (NMB) huwa kuna miamala wanatoa jina na mingine hawatoi jina. Hilo swala nina uhakika nalo asilimia zote wala msimuone huyu jamaa ni mzembe wadau

Mimi binafsi mpaka leo nikituma hela kwenye namba yangu ya zantel kutoka benki huwa siletewi jina kuhakiki na hata laini zingine hizo kuna kipindi nacomfirm jina na kuna kipindi hakuna.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Sintosahau siku nimekosea kutoa bank badala ya kupeleka MPesa nikapeleka kwenye airtime... Hadi leo natumia salio la airtime bila kupenda japo nimeuza kidogo kwa washkaji nikarudisha kama laki 2 tu
Du! hii ni adhabu,hivi walisema hawawezi kurudisha kuwa pesa tena?
 
Hapa wanaotakiwa kukusaidia ni watu wa bank maan pesa imetoka kwao kwenda kwenye mpesa hivyo wenye uwezo wa kureverse muamala ni hao wa bank
Benki hawawezi ku reverse muamala ambao tayari umesha cross kwenda kwenye mitandao,hapo ilikuwa Voda ndio waiblock hela isitolewe
 
Hapo majanga,kama ameishazitoa,Voda hawana msaada,inabidi umtafute huyo mtu uongee naye akurudishie.Niliwahi kumtumia mtu 76 k,baada ya Voda kushindwa kusaidia nikamtafuta akamipiga sound mwishowe alinirushia 26 k kwa taabu Sana. Nilikula hiyo hasara mpaka nikashiba.
Unapotosha kwa faida ya nani mkuu? Unapokosea kutuma fedha hatua ya kwanza unapiga huduma kwa wateja mtandao uliotumiwa fedha watazuia muamala baada ya hapo unaweza kuamua kuwapigia fedha ilikotoka.

Mtandao uliopokea fedha utazuia fedha mara moja baada ya kuridhika na maelezo yako.

Fedha itarejeshwa ndani ya masaa 72 ya kazi
 
Du! hii ni adhabu,hivi walisema hawawezi kurudisha kuwa pesa tena?
Hawawezi na hiyo huduma haipo. Nikahangaika hadi kariakoo kwa vibanda vya vocha hamna anaehitaji wanasema bora ingekua airtime ya tigo
 
Kuna 496,000 ilijichanganya ikazama kwa mpesa, sekunde hiyo hyo nikaichomoa nikazima na simu. Nakuja kuiwasha kesho yake nakutana na sm7 kama 100 za kunibembeleza nirudishe, na muda huo nishanunua na kreti za bia.
 
Hawawezi na hiyo huduma haipo. Nikahangaika hadi kariakoo kwa vibanda vya vocha hamna anaehitaji wanasema bora ingekua airtime ya tigo
Aisee,hii ni mojawapo ya athari za teknolojia
 
Hizi bank kwann zisiweke option ya kuzuia muamala ulipokosea inakasirisha unaweza furahia isikukute
 
Hapo majanga,kama ameishazitoa,Voda hawana msaada,inabidi umtafute huyo mtu uongee naye akurudishie.Niliwahi kumtumia mtu 76 k,baada ya Voda kushindwa kusaidia nikamtafuta akamipiga sound mwishowe alinirushia 26 k kwa taabu Sana. Nilikula hiyo hasara mpaka nikashiba.
Daaah pole sana aisee kuna viumbe humu duniani ni katili sana...
 
Unapotosha kwa faida ya nani mkuu? Unapokosea kutuma fedha hatua ya kwanza unapiga huduma kwa wateja mtandao uliotumiwa fedha watazuia muamala baada ya hapo unaweza kuamua kuwapigia fedha ilikotoka.

Mtandao uliopokea fedha utazuia fedha mara moja baada ya kuridhika na maelezo yako.

Fedha itarejeshwa ndani ya masaa 72 ya kazi
Watu wa humu mna ubishi wa ajabu Sana,nmesema kilichotokea wewe unakuja na nadharia halafu unadai napotosha.Kwanza Mimi sikujua kama nimekosea nilikaa wiki nzima nikisubiri pesa irejeshwe nilipooona hairejei ndo nikapiga simu NBC wakaniambia nilikosea namba nikawaomba wanitumie hiyo namba.Nilikosea namba moja,kumpigia jamaa akasema alisubiri wiki nzima akawa hajapigiwa ikabidi aziingize kwenye kilimo huko Singida ,kulingana na alichonambia.Sasa hapo Mimi nimepotosha nini? Usiishi kwa habari za kusikia.
 
Huenda ikua ridhiki yake mkuu
Nakushauri kama nipesa finyu mkaushie tuu, acha naye aonje utamu wa maisha huenda hajala tokea Hasubuhi hivyo anaona Mungu kamtunuku
 
Kuna jamaa aliwahi kukosea badala ya kumtumia mdogo wake akasukuma mzigo kwangu, mwamba akanipigia akanieleza dhumuni la hiyo pesa, nami sikua na hiana nikamwambia atume namba ya mdogo wake nikamtumia pesa yake, mwaka 2010 jamaa alinishukuru Sana na hata mdogo wake pia alinishukuru Sana maana alikua anasoma chuo
 
0800 002 002

hii ndio namba yao,tatizo ukipiga ni kama wanajua unawamalizia hela zao bank.

niliishasubirishwa dkk 48[emoji3],fikiria umekosea kumtumia mtu laki 4 dkk 48 kama hajatoa nayeye ni mzembe tu.

lakini pia mitandao ya simu wawe na kawaida ya kusikiliza malalamiko,mtu amekosea kuingiza hela,unapiga kuwaeleza wanakwambia mwenye mamlaka ya kuzuia huduma za kipesa ni mwenye line mwenyewe,unapigwa na mtandao wanabariki.ingekuwa baada ya wewe kutoa malalamiko,basi kiasi tajwa kina fleeze hamna kutoa wala kuhamisha,mpaka mtoa taarifa alete taarifa mpya.
 
Bank zinachochea watu kupoteza pesa
 
Back
Top Bottom