MSAADA: Nimepata kazi Serikalini dereva ila mshahara mdogo kuliko wa Mwendokasi ninakofanya kazi sasa. Nimechanganyikiwa!

I agree, mleta mada usikurupike.
 
Ngoja aje atoe maelekezo usije kuta ni zile kazi za vibarua yaani kazi za kungoja mapato ya ndani ndio ulipwe..
 
Daaaaah, wee jamaa bhana aisee...!

Haya bwana, umenikumbusha TXL langu aisee jamaa kama anakuja barabarani hivi akija kucheki kibao tu mwenyewe anarudi kichakani aisee.

Hatari sana mzee baba...!
Hahahaaa wanangu sana hao nawajua mambo yao na nishayaendesha sana. Yani mie kwenye udereva nishapitia sehem nyingi sana

Nawajua siku hizi hadi SM,SU zina vimulimuli mbele dah
 
Kwani mwendokasi siyo serikalini, kwa nini umetoka au ulikuwa na ajira ya muda na sasa umepata ya kudumu?
 
Nenda serikalini kama utapata mkataba wa kudumu, asikudanganye mtu serikalini raha
 
Nenda karipoti kazini baada ya miezi 6 rudi tena utatupa habari njema sana, kila la heri.
 
Sasa wee jamaa umefunguka hivi si watakung'amua kirahisi tu.
 
Mkuu nilipitia scenario The same nayo Ila basic salary ilikua tofauti ya Tsh 42,000/=


Ya serikalini ilikua pungufu Kwa Tsh 42,000/= ukilinganisha na ile ya mkataba

Ila kwako ni mtihani pungufu ya 500,000/=
Sio mchezo tena kama unafamilia

Ila Mkuu ushauri umetolewa na wengi changanya na zako
Naamini utafanya uchaguzi sahihi kbsa

All the best
 
Nenda serikalini
 
[emoji3516]
USITHUBUTU KUFANYA UPUMBAVU WA KUACHA MSHAHARA WA 800,000/- UNAKIMBILIA 300,000/- KWA MATARAJIO YA PER DIEM AMBAYO HAUNA UHAKIKA KUWA ITAKUWA NI KWA KIASI GANI!!!

USITHUBUTU KABISA!!!
 
Ajira za serikalini sivyo kama unavyofikiria, hyo range ni kubwa mno. Ni kweli kuna per diem ila huwa sio constant kiasi hicho mda mwingne hazitokei kutegemeana na ofisi, mshahara wako ndo kila kitu usije ukaingia ukitegemea hzo per diem utachanganyikiwa.
 
Hahahahaaa madereva wanapigana misumari balaa. Ukiwa dereva wa tengo lenye safari sana unaula wakuone unajenga au mnapatana na boss wako lazima ule majungu sana mpaka ukabidhiwe trekta la idara
[emoji3][emoji3][emoji3] eti trekta la idara
 
Wengine tulikataa serikalini tukakimbilia kwenye mashirika, yamebinafsishwa halafu yakafa majuto tuliyonayo hayasemeki umri na Sura tofauti kabisa labda niishie hapo, Ila asiiachie hiyo nafasi wenzake wanaitafuta, huko kwenye laki nane hakuna kinga yoyote
 
Kabla ya kushauri naomba kufahamu yafuatayo
1. Elimu yako ukiondoa cheti cha udereva
2. Una mke na watoto au single
3. Mkataba wa mwendo kasi ukoje? Kuna kupanda daraja au ndio hiyo laki 8 hadi unastaafu?
Ushauri wangu utategemea majibu yako.
Form iv,watoto wawili babu
 
Mkuu nenda karepoti Kati ya watu wanaopiga hela nchi hii ni madereva, mshahara unauona mdogo Ila posho huwa nyingi Sana. Tena huko wakala wa vipimo kuko vzr Sana nenda aise
Poa aisee
 
Haya acha aende..but asije kutuomba tena ushauri..
 
[emoji3][emoji3][emoji3] eti trekta la idara
Hahahaaa we fikiria ukabidhiwe trekta la kupeleka takataka Pugu mshahara lak3 halaf wenzako wanasukuma VXR V8 ya bosi kila wiki safari anakula nyt za hata ef60 tu lazima kazi iwe chungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…