800,000 x 12 = 9.6m per annum
300,000 x 12 = 3.6m per annum
9.6 take away 3.6 = 6.0
Yaani unafikiria kuziacha 6.0m kwa mwaka kwa kutegemea kazi ambayo hata haujui utapangiwa kitengo gani!
Yaani hata kama utapata safari za mara kwa mara, jua kwamba the first 6m sio kipato cha ziada, ni kipato cha kukufanya uwe level moja na ulikotoka. Zaidi ya hapo ndio extra income. (kwa hesabu za harakaharaka bila kuweka kodi etc). Sasa je utasafiri?
Kwa mfano ukaenda huko serikalini halafu ukapewa staff bus, kutwa kwenye foleni za dar, si utajuta?
Mambo ya security of employment yamepitwa na wakati. Security yako ni savings unayofanya na how you invest those savings upate extra income.