MSAADA: Nimepata kazi Serikalini dereva ila mshahara mdogo kuliko wa Mwendokasi ninakofanya kazi sasa. Nimechanganyikiwa!

MSAADA: Nimepata kazi Serikalini dereva ila mshahara mdogo kuliko wa Mwendokasi ninakofanya kazi sasa. Nimechanganyikiwa!

Inategemea na taasisi uliyopo kiongozi kama hapa nilipo mimi ni driver na nalamba 1.2m kiongozi...!

Kuna sehemu driver anakula mpaka 3m acha kabisa chief...!
Sasa unaachaje salary hiyo ambayo ukikaa mwaka tu unaweza kufungua duka la jumlaa jijini dar na ukasahau kuwa ulikuwa dereva...halafu mtu aifuate laki 3 yenye makato kibao
 
Yeye amesema laki 3. Wewe unasema 1.2 m! Angekuwa na yeye anakwenda kupata 1.2 m, asingeleta hii mada hapa.
Inategemea na taasisi uliyopo kiongozi kama hapa nilipo mimi ni driver na nalamba 1.2m kiongozi...!

Kuna sehemu driver anakula mpaka 3m acha kabisa chief...!
 
Laki tatu bado hawajakata bima na nssf utabakiwa na 240,000/=
 
Kwa salary uliyosema hapo mbona haviendani na mazingira ya mishahara ya wakala wa baadhi ya taasisi,nijuavyo mimi waliopo serikali kuu ndio wanaolipwa kidogo ila Ngo,wakala na mashirika ya serikali wao ndio mishahara yao inakuwaga mikubwa,sasa hao hao wakala wa vipimo inakuwaje salary yao kuwa ivyo
 
... inategemea majukumu atakayopewa. Kuna taasisi kama UDSM zina hadi matrekta ya kupeleka takataka dampo na wengine wana bodaboda za kufuata barua posta. Ajiandae kisakolojia sio lazima akakabidhiwe V8 maana ndio dream za madereva huko sirkalini hadi wanalogana. Na 300 series muda wowote itaingia serkalini tegmeeni vifo vya ghafla vya madereva!
Hahahaaa kama kuna jamaangu alipata kazi udereva wizara ya kilimo akazogoa nini sijui wakamkabidhi trekta la kulimia mpunga na kubeba magunia chimala huko. Unakaa chaka kwa chaka

Wengi huwa wanatamani wapate V8 watuwashie taa tu za hazard tuwapishe barabaran
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwahiyo hapo nikujua kuubwabwaja, tena kwa majungu kama memory card haa haa haa
Hahahahaaa madereva wanapigana misumari balaa. Ukiwa dereva wa tengo lenye safari sana unaula wakuone unajenga au mnapatana na boss wako lazima ule majungu sana mpaka ukabidhiwe trekta la idara
 
Nimepata kazi Serikalini dereva mshahara 300,000/ kwa mwezi, wakati Mwendo kasi nachukua 800,000/. Nimechanganyikiwa!

Wanabodi mimi ni dereva mzoefu wa daladala kisha nikaajiriwa na Mwendokasi ambapo nakula 800,000/per month .

Wandugu kwa sasa nimevurugwa kwan baada ya interview iliyohusisha watu 760 ambao tuliomba kazi wakala wa vipimo tumepenya na kuajiriwa 57 tuu.

Nimepewa barua Jana napaswa kuripoti kituon kuanzaia 2/7 sasa aisee mbona hii salary Jau!? Yaani nipo kipindi kigumu wandugu hebu wenye uzoefu nisaidieni hill!?

Kiukweli napata wakati mgumu sana barua ninayo ila naipenda ajira za Serikali tatizo hiyo salary!?

Naomba ushauri.
Nina uhakika Mwendo kasi hifahamu hata kitu kinaitwa Per diem. Serikalini wapo madereva wanaishi vzr kushinda baadhi ya maofisa wakubwa. Nikushauri tu uendee, mwanzo mgumu lkn utafika. Changamoto mpya ndizo zinakuza akili.
 
800,000 x 12 = 9.6m per annum
300,000 x 12 = 3.6m per annum
9.6 take away 3.6 = 6.0

Yaani unafikiria kuziacha 6.0m kwa mwaka kwa kutegemea kazi ambayo hata haujui utapangiwa kitengo gani!
Yaani hata kama utapata safari za mara kwa mara, jua kwamba the first 6m sio kipato cha ziada, ni kipato cha kukufanya uwe level moja na ulikotoka. Zaidi ya hapo ndio extra income. (kwa hesabu za harakaharaka bila kuweka kodi etc). Sasa je utasafiri?
Kwa mfano ukaenda huko serikalini halafu ukapewa staff bus, kutwa kwenye foleni za dar, si utajuta?
Mambo ya security of employment yamepitwa na wakati. Security yako ni savings unayofanya na how you invest those savings upate extra income.
 
nyinyi mnaomshauri achukue mshahara wa laki 3 mna roho mbaya sana. yaani miezi mi 3 ndio sawasawa na mwezi mmoja mwendo kasi. kwa mwaka mwendo kasi ni 9.6m serikalini atapata 3.6m. mnaongelea marupu rupu na per dm, je yatafika laki 5 kwa mwezi? ili ifike hiyo laki 8. ukienda kuyakuta hayo marupu rupu sawa, je ukiyakosa au yakawa kidogo sana. Time is money, nenda sehem unayopata hela nyingi achana na story za vijiweni.
 
Nimepata kazi Serikalini dereva mshahara 300,000/ kwa mwezi, wakati Mwendo kasi nachukua 800,000/. Nimechanganyikiwa!

Wanabodi mimi ni dereva mzoefu wa daladala kisha nikaajiriwa na Mwendokasi ambapo nakula 800,000/per month .

Wandugu kwa sasa nimevurugwa kwan baada ya interview iliyohusisha watu 760 ambao tuliomba kazi wakala wa vipimo tumepenya na kuajiriwa 57 tuu.

Nimepewa barua Jana napaswa kuripoti kituon kuanzaia 2/7 sasa aisee mbona hii salary Jau!? Yaani nipo kipindi kigumu wandugu hebu wenye uzoefu nisaidieni hill!?

Kiukweli napata wakati mgumu sana barua ninayo ila naipenda ajira za Serikali tatizo hiyo salary!?

Naomba ushauri.
Kabla ya kushauri naomba kufahamu yafuatayo
1. Elimu yako ukiondoa cheti cha udereva
2. Una mke na watoto au single
3. Mkataba wa mwendo kasi ukoje? Kuna kupanda daraja au ndio hiyo laki 8 hadi unastaafu?
Ushauri wangu utategemea majibu yako.
 
Back
Top Bottom