Msaada: Nimepatwa na changamoto kwa "Wife" na huyu dada

Msaada: Nimepatwa na changamoto kwa "Wife" na huyu dada

Nimeyumba kidogo kiuchumi toka mwezi wa 1. Kutokana na Corona na sehemu nyingi duniani kuyumba kiuchumi pia.

Binafsi huwa nanunua kila kitu mwisho wa mwezi na kuweka nyumbani, kila kitu kwa maana ya kwamba hata ikitokea mwezi mzima tukaamua kukaa ndani bila kutoka tutaishi vizuri tu. Pia mwisho wa week naenda nunua vegetables like nyanya, vitungu, carrots etc ambavyo haviwezi kaa mwezi hadi mwezi. Pamoja na hayo kila siku naacha Tsh. 7000 nyumbani. Hiyo siulizi watanunulia nini coz kila kitu kipo mafuta, gesi, sukari, mchele n.k

Kutokana na hali ya uchumi kuyumba kiwango cha kucha home kilipungua from 7000 mpaka 5000 na sometimes 4000. But still mahitaji mengine kama kawaida, hapo nami najiwekea mafuta kila week kwenda kazini.

Wife hajawa muungwana. Nampa pesa sometimes anafoka sasa hii ya nini (kwa maana ya kwamba ni ndogo kuacha home). Pamoja na kuwa hata yeye anafanya kazi but akinunua kitu lazima nije kumrudishia pesa. So imefikia hatua nikawa napata mawazo sana, binti mmoja aliona sipo ok huyu ni rafiki toka miaka ya nyuma sana 2014.

Sababu ya kujali na nini akawa karibu nami na mwishowe tukawa wapenzi, kiuhalisia yeye anaonesha kujali sana, atanipa pole, atanisaidia napokwama n.k. nimejaribu kumwambia sipo vizuri kiuchumi ili anikimbie ndio kwanza ananitia moyo.

Hili huwa linanitesa sana, anaonesha kunipenda no matter what na kuniheshimu, nilijaribu kuangalia kuwa maybe mke wangu ana nicheat miaka yote hii sijapata ushahidi wowote, so yupo hivyo tu ni mkaidi na si mtu wa huruma sana. She is cold hearted. Mjeuri sana kwa almost kila mtu hana marafiki wengi na mara nyingi hugombana na rafiki zake coz anajiona ni much better than them.

Sasa napata shida huyu mpango wa kando sometimes ndio nawish angekuwa mke ana sifa zote kwa uzuri wa sura na umbo na very romantic pia, ingawa hana elimu kubwa ana certificate tu. Sasa inafikia hatua nawaza kufanya naye mambo ya maendeleo coz anapokuwa na jambo ananishirikisha nikimshauri anafanya tofauti na wife ni mkaidi mpaka jambo liharibike ndo anakubali alikosea.

Huyu dada nilimshauri aache kazi alipokuwepo afanye biznez flani akaacha kweli na kuanza kwa nguvu hiyo business. Sasa anatengeneza pesa, anajituma sana. Mdada anaondoka saa 11 na kurudi home saa 2 usiku ukimwona huwezi mdhania sababu ya uzuri na mwili wake but si mvivu hata kidogo.

Pia, kwenye mapenzi anajituma sana, anaonekana kabisa ana enjoy mapenzi sana nami popote tuna make love na kufurahi. Wife tukifanya naye akimaliza tu hapo anaanza kunambia nimalize na sometimes ananiacha sijamaliza anaomba alale. Hii nayo ni shida kwangu.

Sasa najikuta kwenye hard time sana maana huyu dada ananipenda na kunisikiliza sana. Nikimwambia jambo analifanyia kazi na si kwa sababu anapata pesa kwangu, No yaani yupo hivyo tu.

Naumia ndugu zanguni nawaza nifanye nini sababu nashindwa kumwacha huyu dada hata kumtafutia sababu ni ngumu. Hajanikosea toka miaka yote namfaham hajawahi nikosea. But naumia pia namsaliti mke wangu. Nipo njia panda sana katika hili nahitaji faraja lakini aliyepaswa kunipa faraja doesnt do that badala yake mtu mwingine kabisa ndio anachukua jukumu hilo.

Ushauri wenu.
Jaribu kuishi na huyo dada hata week tu uone rangi zoteee. Utataman kurudi kwa mkeo
 
pole sana mkuu, hizi nyumba zina siri kubwa sana ukisema umwache unaweza kukuta uko unakoenda utakutana na majanga Zaidi, jaribu kukaa na mkeo uone kama atabadilika kama atazingua unaweza kuchukua hatua nyingine
 
Wewe jamaa unamsingizia mkeo ili uwe na huo mchepuko unadai toka 2014 upo nae. Sidhani kama mkeo ni mkosefu kiasi hiki uenda umembadilisha mwenyewe ndani. Uenda kajua kila ovu lako sasa nadeal na wewe kihuni. Achana na mchepuko hivi unawezaje kuhudumia wake wawili. Tafuta demu piga futa vumbi urudi kwa mkeo ndani. Kutoka 7000 mpk 5000 na bado analalamika sio sahihi kuna jambo ebu funguka vyema.
Unajikuta FBI, sasa kashasema alikuwa anaacha 7000, uchumi ukayumba kidogo akaanza kuacha 5000 lakin bado mke ana leta gubu..sasa afunguke vp? ww toa ushaur kwa ulichokisoma mengine ya kufunguka hayakuhusu mkuu...
 
Hapo usichokijua ni kuwa ht huyo mkeo angekuwa mchepuko angefanya yote hayo
 
Back
Top Bottom