Msaada: Nimetupiwa kipande nateseka mwaka wa 3 sasa, nahitaji msaada

pole sana mkuu , ufanikiwe katika kutatua unayopitia naelewa sana hiyo hali , Mungu awe nawe mkuu ktk kipindi chote


Note ; Tukienda kutafuta ugenini , ni vyema tukajikita kataka malengo yetu ya awali kama hulifuata fursa bas ni bora utafute fursa tu nje ya hapo utakuna na ubaya wa mwanadamu
 
Uko mkoa Gani nikupe Namba ya Fundi mzuri tu..... Am serious
Fundi mkubwa kuliko wote ni Mungu tu, kama kuna fundi zaidi na zaidi watu wasingekufa, cha msingi amrudie Mungu wake vizuri na Mungu atamjibu, aachane na vitendo vyote vya hovyo namaanisha awe msafi, asali sala za usiku na kumlilia Mungu, Mungu wetu yupo muda wote kusikiliza shida zetu, matatizo yetu lakini hatumuombi badala yake tunakimbilia kwa waganga, kuwa na yakini yupo Mungu mwenye nguvu sana anayesema kuwa na ikawa, si mchawi, si mashetani, si majini hakuna anayeweza kuzuia ulichoandikiwa na Mungu juu yako. Jenga tabia na mazoea ya kuomba mara kwa mara, hakikisha moyo wako unakuwa safi, penda kutoa sadaka kusaidia wenye uhitaji, unapotoa sadaka nuia shida zako zote, unaposali eleza matatizo yako yote kimoyomoyo.
 
Kwa imani yangu niliyonayo ninaamini husda, roho mbaya, vijicho vipo katika maisha yetu ya kibinadamu na ndio maana tumeambiwa kuwa wasiri sana kwenye mafanikio yetu, wengi hawapendi mafanikio yetu bali wanapenda kuanguka kwetu.

Walihusudiwa manabii wa Mwenyezi Mungu sembuse sisi, nabii Yusuf akiwa mdogo sana alimwambia baba yake, nimeota ndoto, nyota kumi na moja, mwezi na jua, nimeviota vyote hivi vikinisujudia. Baba yake mzee Yakub akamwambia usije ukawasimulia ndoto yako hii ndugu zako. walimfanyia mambo mengi sana ya vurugu lakini hakuwahi kumuacha Mungu hatma yake haikubadilika akaja kuwa waziri wa misri.

Pia tusiache kumuomba Mungu atupe ustahmilivu kama wa nabii Ayubu, hakika yupo Mungu ambaye hajawahi kutuacha, achana na mambo ya manabii feki wanaotaka pesa akuombee, achana na waganga wanaotaka pesa, kama ni muislam kama imani yangu ilivyo basi ninapoona kuna jambo haliko sawa haraka namshtakia Mungu mwenyewe na amekuwa akinijibu.

Kwa imani yako yoyote, piga goti lia na Mungu na nina imani atakujibu. Mungu ni wa woe, hatma yako ni wewe na Mungu wako na hakuna yoyote anayeweza kubadili hatma yako, cha muhimu ni kuomba sana.
 
Ccm imesababishia watu mdongo wa mawazo,si ajabu nawe ni ccm
 
Mwamba Mshana Jr alishaachana na hizi mambo! Ingawa sina hakika kama huwa yanaachwa!!
 
Asee ubarikiwe kwa kila jema na baya lako. Nikuulize tu kuna siku umewahi kusafiri ukapiga goti kumuomba Mungu upate ajalI ufe au upate kilema ktk safari yako?

Kama hakuna basi hakuna mwanadamu anayeweza kuomba apite ktk magumu.

Asante
Umeandika deep sana! Unaendeleaje sasa hivi ndugu yangu?
 
Tuma majina yako na changamoto yako pm

Usiku saa nane ntakuombea . utapona .

Then tafuta hawa watu

Mwana Saikolojia
Mentor wa biashara
Spiritual FATHER.

Business -inaonekana hadharani so bila kujilinda you can attract evil eyes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…