Msaada: Nina presha 162/103 umri wangu miaka 33. Je, nianze dawa au nibadilishe lifestyle?

Msaada: Nina presha 162/103 umri wangu miaka 33. Je, nianze dawa au nibadilishe lifestyle?

Wakuu habari zenu

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
Kwa Umri wako hatutegemei uwe na Pressure.

Na kama umepima mara moja tu ukakuta iko juu unatakiwa urudie walau mara tatu kwa nyakati tofauti, hatuwezi jua ulipopima labda ulikua kwenye Panic/Fear. Namaanisha bila kurudia mara tatu tutabaki kuita WhiteCoat Hypertension(HTN kwa sababu ya woga wa mazingira ya hospitali)

Iwapo itabaki kuwa Juu baada ya kurudia walau mara tatu kwa siku tofauti basi shughulikia mambo yafuatayo.

BMI yako iko je?
Pima uzito wako na Urefu wako nenda Playstore au Appstore tafuta BMI calculator.

Utaitaji check out kubwa ya Figo, Goitre n.k ambavyo daktari wako inabidi akifanyie kunua sababu kwa nini unapata Hypertension udogoni.

Ikumbukwe kuna kitu kinaitwa Secondary Hypertension....Hii hata umeze dawa inaweza isisaidie iwapo hizo dawa hazitibu chanzo husika.

Fika hospitali wanayoweza kuku evaluate...Hypertension ni ugonjwa hatari sio wa kuombea ushauri hata mitandaoni
 
Pia hizo kilo ni nyingi kwa urefu huo.
Jamaani ni Overweight.
Uzuri ni kwamba sio Obese.
Screenshot_20210511-160452_BMI%20Calculator.jpg
 
Kwa Umri wako hatutegemei uwe na Pressure.

Na kama umepima mara moja tu ukakuta iko juu unatakiwa urudie walau mara tatu kwa nyakati tofauti, hatuwezi jua ulipopima labda ulikua kwenye Panic/Fear...
Mkuu kwa presha hii inafaa mim kuanza mazoezi yakukimbia napresha isiniletee shida wakati wakukimbia
 
Zingatia nilokueleza hilo swala lako naona halina maana yoyote.
Labda kama haujaelewa popote kwenye maelezo yangu!
Nimeeelewa vizur Kama natakiwa kupima Mara mbili kwa siku kwa nyanyakati fouti kwa siku tofauti pia nichek figo.. kwenye kupima nimepima leo presha Mara mbili sehem tofaut ikawa hivo pia nkaja jipima Mara ya tatu ktk mashine yngu ikawa hivo hivo
 
Wakuu habari zenu

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
Hypertension is a Silent Killer.

TENA MSHUKURU MUNGU SANA KWA MAONO ALOKUPA UKAPME.

Kama umepimwa mara 2 -4 nyakati tofauti na Ukaona BP yako iko Juu. Basi wewe ni Mgonjwa wa BP.

Hiyo presha ipo juu,, kwa kubadili mfumo wa maisha utaishusha lkn kidogo.

Ni vema uanze Dawa angalau uishushe mpaka 140/90 wakati huohuo ndo uendelee na mfumo mpya wa maisha yako

[emoji117]Acha Pombe.
[emoji117]Usivute sigara
[emoji117]achana na vyakula vya mafuta
[emoji117]ACHANA NA MATUMIZI YA CHUMVI.
[emoji117]KUA MAKINI UNYWAJI WA MAJI, USIZIDISHE LITA 1-2 KWA SIKU.
10/// [emoji117]ACHANA NA MADEMU
11///[emoji117]ACHA KUKOPA

10 na 11 , nikwasababu mademu na madeni , vyote vinaanza na "Made..." hivi viwili vinasababisha stress za Kufa mtu[emoji23]

Sikudanganyi Bob, Ukishupaza Shingo, ukaacha DBP ifike 130 , utaanza kuisogolea parapanda adoado[emoji23]
 
Hypertension is a Silent Killer.

TENA MSHUKURU MUNGU SANA KWA MAONO ALOKUPA UKAPME.

Kama umepimwa mara 2 -4 nyakati tofauti na Ukaona BP yako iko Juu. Basi wewe ni Mgonjwa wa BP...
Vp mazoezi kwahii presha nikiyaanza Itakua shida? Je presha itapanda Zaid pindi nikiwa nafanya mazoezi?
 
Wakuu habari zenu

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
Waafrika tunarogana sana, jikabidhi kwa Mungu akupe ulinzi wake na akuondolee hiyo mijigonjwa isiyoambikizwa
 
Wakuu habari zenu

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?

Rudia kupima hio blood pressure hata mara tatu kwa siku hio hio moja ila pishanisha masaa..angalia kama bado inasoma kua ipo juu kama bado ipo juu nenda hospitali ya jirani uonane na muuguzi kwa ushauri zaidi huku ukianza kubadilisha mfumo wa maisha kuanzia lishe mazoezi na kupunguza chumvi katika milo yako haswa haswa chumvi ya kuongezea.Kila la kheri
 
Vp mazoezi kwahii presha nikiyaanza Itakua shida? Je presha itapanda Zaid pindi nikiwa nafanya mazoezi?
Hapana ,mazoez ni mazuri ,husaidia kushusha presha..mazoez kama kukimbia, kutembea, kuruka kamba ,husaidia kushusha presha .

Kimbia angalau dakika 20 kwa siku nne ndan ya wiki.

Ila kama unafanya mazoez na ukaanza hisi maumivu ya kifua, kukosa pumzi, kizunguzungu, maumivu ya mikono, mabegan n..k Uache.
 
Mkuu kuna dawa nataka nikushauri kuitumia ila usiidharau... Ukishaitumia hiyo dawa ndani ya wiki moja jaribu kupima tena alafu ulete mrejesho tuone imekuwaje.
 
Hivi pressure ni vizuri kipa mara moja tu na kuchukuamajibu yake au kipima mara mbili kwa wakati mmoja.
Na ukipima twice unachukua mateo ya kwanza au ya pili?

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom