Wakuu habari zenu
Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
Pole mkuu!
Nikupe hongera kwa kupata alert kuwa kuna tatizo na u need to work hard kuliepusha. Wengi wetu tunayo hayo matatizo lkn huja kugundulika late wakati hali ishakuwa mbaya sana... mfano ni pale mtu anapopigwa stroke.
Mimi kuna wakati nilikuwa na kg kama 89 hivi kwa height yangu nilikuwa overweight lkn sikujua kbs hilo suala... ilikuwa kawaida sana kuumwa kichwa na kuchoka sana hata kwa kutembea kidogo tu....
Siku moja kichwa kiliniuma sana kila nikipiga panadol wapi, maji litre na litres wapi....
Nikaenedha gari hadi Hosp ya GEMSA kwa watu wa Arusha wanaifahamu. Kufika hapo nikafuata taratibu na kufika pale kwa nurse kwa ajili ya vipimo vya awali yaani pressure na weight na height.
Baada ya kuoima pressure niliona nurse kama amwshtuka kidogo ingawa alijitahidi kujizuia... mara akaseme subira nakuja, akaingia chumba cha daktari, dakka kama 7 hv nikaona kile kiuzio cha kijani kinasogezwa pale kwangu na maktari wakaja kama 5 hivi.... nikashtuka...
Wakaanza kunipima baadae wakanipa dawa fulani nikaweka kwenye ulimi zikawa zinayeyuka kidogo baadae wakanioima tena pressure ikawa imeshuka 140/96 kama sikosei. Hapo wakanambia ndo imeshuka.
Baada ya hapo nikabaki na madaktari wawili tukahamia consultation room
Daktari akanihoji style yangu ya maisha akanieleza kuwa nipo katika risk kubwa na nisipochukia hatua hali haitakuwa shwari. Akanishauri kuounguza wanga, sukari na fried +junk food. Na kwamba nikizembea hilo nitaanza dawa tena ikiwa sitopata mqdhara makubwa zaidi.
Nilirudi nyumbani mnyonge sana
From that day nilianza jogging naenda 1.5Km, it was 2017 nipunguza kabisa wanga, sukari, soda mitungi ikawa No etc... maisha yangu yalikuwa ni mazoezi kama 6 months nikaanza kupungua sana, mwaka hv nikawa nimekata 15kg....kukimbia nKo nikagain nikawa naenda 10km-21.1kms nikaanza kushiriki marathons na nikawa addicted na ruuning. Gym ni kidogo sana kuhudhuria.
Niseme ukweli hali ile imenisaidia sana sasa kila mtu anatamani kuwa kama nilivyo nipo slim, No wese mwilini na katika kipindi hicho sijawahi tumia dawa yyt ya pressure zaidi ya mazoezi.
Kwa sasa nishakuwa nguli i run 200km kwa mwezi last year nilijiwekwa target y kukimbia 2000km na nilifanikiwa. Nipo kwenye ckub mbalimbali za runners, na member wa gym kadhaa hapa mjini.
Nikutie moyo ndugu yangu una nafasi ya kubadili life style yako kbl hujakutwa na makubwa.... i have a friend alipigwa stroke ofcn akaka bench 2 yrs ashukuriwe Mungu amekaa vzr sasa.
I have friend pia alipigwa stroke hadi sasa ahajaka sawa ni kama 4 year.
Nilichoamua from 2019 ni kuwahamasisha marafiki zangu na ndugu zangu juu ya kufanya mazoezi, namshukuru Mungu wengi wanaitikia vzr and they are doing good.
Download application inaitwa strava itakusaidia kukupa motivation na uta-grow vzr kwenye mazoezi hasa walking na running.
Kama unaweza kuruka kamba ni nzr sana pia it will help.
Gym sikushauri wengi wanaenda kwa show off tu hakuna kitu wanafanya cha kuwasaidia.
Apart from afya mwonekano wako unakuwa super sana. Unene haujawahi kumpendeza mtu nadhani ni kwa sababu ya madhara yake.
Karibu sana ukihitaji ushauri.
Ngoja nilale kesho chap 05:00Am niamke nipige 10kms kwa pace ya 5:00