Msaada: Nina presha 162/103 umri wangu miaka 33. Je, nianze dawa au nibadilishe lifestyle?

Msaada: Nina presha 162/103 umri wangu miaka 33. Je, nianze dawa au nibadilishe lifestyle?

Kupanic huwa napanic Ila situmii kilevi Cha Aina yoyote ile
Angalia normal pressure yako mkuu.

Pengine unadhani imepungua au imeongezeka kumbe ndo normal pressure yako.

Na jitahidi upime pressure ukiwa uko katika hai ya kawaidia umerelax huna hasira wala stress wala haujatoka mazoezi au kutembea umbali mrefu.

Hakikisha unapima presha ukiwa umetulia mapigo ya moyo yakiwa yametulia
 
Duu hizi coment zivyomiminika utadhani mtoa maada yuko ICU anakufa kesho...Hahah Mtoa maada usije ukapanic hata kidogo kwani hiyo ni hali ya kawaida ila fanyia kazi ushauri wa wadau haswa kwenye swala la diet na mazoezi
 
Wakuu habari zenu,

Kama nimevoandika hapo juu nimepima presha Leo na presha yangu ni kama hiyo nlioandika Ila sikuwahi kuwa na presha. Sasa wakuu ushauri wenu nianze dawa au nianze lishe ya kuacha wanga na sukari?
0. pata ushauri wa daktari, mwambie KILA kitu unachopitia! KILA kitu maana huenda kuna jambo lina trigger hii presha yako!
1. punguza mawazo
2. jitahidi kutembea dakika 30 kwa siku kama sehemu ya mazoezi (usihesabu mida unayotembea kikazi ama kwenye misele)
3. kata chumvi ili ujitahidi ku monitor zaidi
4. zingatia muda wa kupumzika.
5. kama upo kwenye mahusiano na ni kitimtim, basi jitahidi kuchukua break (wazo tu)
6. kama unatumia dawa, basi nazo zifuatilie

dawa iwe sehemu ya mwisho na nina uhakika daktari atakupa muongozo mzuri!

pole na pia kila la heri katika kupona...
 
Mimi tangu February nikipima ipo juu,but kila ninapotaka kupima nakuwa na hofu na pressure inakua juu inafika mpaka 203/113 ,nimeacha pombe,situmii chumvi nyingi,sivuti sigara,uzito wangu kg 64 umri miaka 32,nyama nyekundu nakula kwa nadra sana ,huwa natembea sana tena sana,sasa sijajua hii presha yangu inatokana na nini,kuna wakati fulani mwishoni kwa mwaka jana nilikumbwa na stress sana ,sasa sijajua kama hizo ndo chanzo au la,dokta kanipa madawa kibao ila sijaanza kutumia nataka niende hospital moja ya mwisho kikapate vipimo kamili kabla masuala mengine hayajaanza
 
Achana na madawa hayo mkuu.

Hayana mpango wowte ule.

Shida yako ni hofu kila ukitaka kupima hofu inakujaa.

Hakikisha huna stress,huna hofu,hujatoka kufanya shughuli ngumu kisha hapo sasa ndo pima pressure.

Katika fani ya utabibu katika mambo anayotakiwa daktari kukufanyia ni kutokujua kuwa unapimwa respiration rate yako ikoje kwa sababu kujua hilo kuna watu wanaoata hofu wanaanza kupandisha hali.

Usinywe madawa mkuu nakusihi sana mkuu,labda kama iko severe sana aisee.
 
Cha kwanza rekebisha BP tumia dawa kama unaweza pia kunywa Asprin kuzuia stroke haya uyafanye kwa ushauri wa daktari.

Badilisha life style, kula sana mboga na matunda ikiwezekana samaki. Fanya mazoezi, tembea walau kwa lisaa moja kila siku.

PB ikiwa sawa unaweza kuacha dawa kwa ushauri wa daktari pia. Nunua mashine uwe unajichek pressure kila wiki.
Hapo kwenye machine ndio umekosea ukinunua kile kidude umejiroga,presha utaishi nayo milele
 
Mimi tangu February nikipima ipo juu,but kila ninapotaka kupima nakuwa na hofu na pressure inakua juu inafika mpaka 203/113 ,nimeacha pombe,situmii chumvi nyingi,sivuti sigara,uzito wangu kg 64 umri miaka 32,nyama nyekundu nakula kwa nadra sana ,huwa natembea sana tena sana,sasa sijajua hii presha yangu inatokana na nini,kuna wakati fulani mwishoni kwa mwaka jana nilikumbwa na stress sana ,sasa sijajua kama hizo ndo chanzo au la,dokta kanipa madawa kibao ila sijaanza kutumia nataka niende hospital moja ya mwisho kikapate vipimo kamili kabla masuala mengine hayajaanza
Itakuwa ya kurithi.pole sana kuwa makini.stroke inakunyemelea
 
Tumia mkojo wako halafu baada ya muda upime tena utuletee mrejesho hali imekuwaje.
 
usianze dawa mkuu ,
1.Acha pombe kwa miezi 3
2.nenda gym 3 days kwa wiki fanya mazoezi 40m
3.kunywa lita 3.5 za maji kuanzia asubuhi hadi saa 10 daily
4.acha kutumia sukari na chumvi jitahidi kuiepuka sana
Ukipungua kilo 5 hiyo pressure byebye m
mimi sio daktari ila nilipokuwa na 34 nilikutwa na pressure kama hiyo hadi leo sina kabisa pressure
 
Dawa za kuondoa bad cholestrol ni zipi maana nahisi hio ndio itakuwa inansumbua mimi hata kabla sijaipima tu manaa nakula nyama daily!
Tumia binzari, nenda supermarket nunua binzari ya unga uwe unaweka kijiko cha chai kwenye maji ya moto kikombe cha kahawa unakunywa usiku kabla ya kulala, pia acha sukari kabisa ila tumia matunda ukiwa na kiu ya sukari, chai kunywa kavu bila sukari na juisi hivyo hivyo. Ukiwa vizuri urudi kulipa consultantion fee.
 
Shukrani, niitumie kwa muda gani
 
Tumia binzari, nenda supermarket nunua binzari ya unga uwe unaweka kijiko cha chai kwenye maji ya moto kikombe cha kahawa unakunywa usiku kabla ya kulala, pia acha sukari kabisa ila tumia matunda ukiwa na kiu ya sukari, chai kunywa kavu bila sukari na juisi hivyo hivyo. Ukiwa vizuri urudi kulipa consultantion fee.
Hii inasaidia kutokomeza presha au bad cholesterol?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hypertension is a Silent Killer.

TENA MSHUKURU MUNGU SANA KWA MAONO ALOKUPA UKAPME.

Kama umepimwa mara 2 -4 nyakati tofauti na Ukaona BP yako iko Juu. Basi wewe ni Mgonjwa wa BP.

Hiyo presha ipo juu,, kwa kubadili mfumo wa maisha utaishusha lkn kidogo.

Ni vema uanze Dawa angalau uishushe mpaka 140/90 wakati huohuo ndo uendelee na mfumo mpya wa maisha yako

[emoji117]Acha Pombe.
[emoji117]Usivute sigara
[emoji117]achana na vyakula vya mafuta
[emoji117]ACHANA NA MATUMIZI YA CHUMVI.
[emoji117]KUA MAKINI UNYWAJI WA MAJI, USIZIDISHE LITA 1-2 KWA SIKU.
10/// [emoji117]ACHANA NA MADEMU
11///[emoji117]ACHA KUKOPA

10 na 11 , nikwasababu mademu na madeni , vyote vinaanza na "Made..." hivi viwili vinasababisha stress za Kufa mtu[emoji23]

Sikudanganyi Bob, Ukishupaza Shingo, ukaacha DBP ifike 130 , utaanza kuisogolea parapanda adoado[emoji23]
Sasa mbona unamwambia aishushe mpk 140 hapo hapo asiiache ifike 130
 
Back
Top Bottom