Urefu wako? Kuna kitu kinaitwa BMI yaani Body Mass Index. Utefu au kimo chako na uzito wako ndiyo determinants za BMI. Ikizidi mpaka red ni hatari sana.
Kwanza usipaniki kabisa.
1. Anza na maji ya kunywa vuguvugu glass 4 kika asubuhi na mchana kunywa taratibu na jioni kabla ya kulala kunywa maji ya vuguvugu.
2. Acha kabisa refined wanga kama vitokanavyo na Michele, ngano kama chapati, maandazi n.k
3. Acha nyama nyekundu haraka mno.
4. Kula protein za mimes na nafaka zaidi. Na kidogo samani na kuku.
5. Kula mboga za majani kwa wingi sana na matunda ili uwe na space ndogo ya chakula. Kula mboga na matunda nusu saa kabla ya kula. Angalizo: kula mboga zaidi na matunda kiasi kwa kuwa yana sukari. Pia ukiweza punguza matunda yenye sukari nyingi. Google utaona sugar contents za matunda.
6. Kuhakikisha mlo wa mwisho uwe kuanzia saa 1 mpaka 2 usiku na uwe mwepesi.
7. Fanya light exercises kama kutembea taratibu maana kwa sasa presha iko juu hivyo mazoezi magumu yatakuletea shida ya presha kupanda zaidi.
8. Fanya Vipimo vya moyo ECG na ECHO ili kuona hali ya moyo kwa sasa na kama hakuna tatizo Dr atakuandikia vipimo vingine ambavyo vinahusiana na presha.
9. Pima cholestrol yaani wingi wa mafuta kwenye mishipa ya damu.
10. Pima hormones tests TSH, T3, T4 na Cortisol levels.
11. Pima Figo ( Renal Panel) na Sukari hasa fasting glucose. Acha kutumia sukari kwa sasa. Kunywa chai kavukavu au kunywa maji moto asubuhi inatosha.
Nataka nikuhakikishie kuwa Pressure inatibika kwa wewe mwenyewe kufanya maamuzi hasa kama inatokana na life style. Hata kama inatokana na hitilafu ya kwenye moyo bado unaweza kufanya control ya life style ili kupunguza overwork ya moyo.
Narudia pressure ni kubwa kidogo ila usiogope na itarudi haraka tu normal kama hakuna hitilafu kwenye moyo.
Mdogo mdogo kula punje 2 au 3 kitunguu swaumu kila asubuhi. Kunywa limao umelikata vipande na maganda yake ndani ya maji moto kila asubuhi na jioni. Usiweke Tangawizi kwa sasa.