Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,449
Msaada, kuna jirani yangu Kaingiliwa na nyoka mazingira ya nyumbani kwake, huyu nyoka ana week tangu aonekane mara ya kwanza, ila upo uwezekano ni zaidi ya week maana kabla ya hapo ilikua inatokea tu kuku kapotea, kelele za kuku bandani, usumbufu dirishani akiwa amelala n.k n.k.

Baada ya muda ndio akaonekana live. Kumtafuta imekua changamoto kwanza ni kwa mashaka maana yaweza kua naye anakutafuta au mshtukiziane akuwahi.

Na inaonesha ni mkali na ana sumu mbaya, Juzi paka wake alikua naye ndani, ile anatoka tuu nje paka akapiga kelele kutoka anamkuta paka ndio anakaukia, chini ya dk akawa tayari kafa.

Japo inaonekana alimjeruhi, maana mdomoni alikua na damu na ngozi.

Imebidi ahamishe watoto huku, hawakai tena pale. Mwenyewe anaenda kwa machale.

Nyumbani kwake kuna maua mengi sanaa yale yanayotanda mpaka ukutani, bustani ya mboga, kama mita 50 hivi kuna kijimto na nyasi nyingi, tumepatana leo tupulize ile dawa ya kuua mimea.

Kuna uwezekano anakuja na kuondoka, na si mara ya kwanza kuonekana maeneo ya nje, wanafunzi washamuona sana Kwa maelezo yao ashawahi mgonga mmoja wao kwenye kiatu.

Huyu ndugu tunamsaidiaje?
Jana kakutana na michirizi nje, akaishia nje.
Juzi katika kumsaka tukaambulia gamba tukasepa.
Mara anoe maua yanacheza au kuanguka.

Hakuna njia yoyote zaidi ya kumuua, ila njia gani sasa?

Naomba imani za kishirikina uwe ushauri wa mwisho.
 
Nyoka kamuuma paka anakukufa. 🙄

Then kamuuma mwanafunzi na hajakufa.😇

Ebu nyorosha maelezo mkuu, otherwise mnaweza mwagia mafuta ya taa ama diesel kuzunguka maeneo ambayo mnahisi huyo mgeni anaonekana.

Ama, nashauri mchome moto eneo linalo zunguka hiyo nyumba na hata ikiwezekana hayo maua mengi myateketeze kwa moto.
Hofu ni kitu mbaya sana
 
Pia amwage mbolea ya chumvichumvi.

Ila wawe makini, wasije wakamuua halafu wakaonekana kuwa wamemuua, maana nyoka ni nyara ya serikali kwa mujibu wa Kigwangara, au kama watamuua basi wasiwe na itikadi ya upinzani.
Ni kosa kumuua ukiwa mbugani au porini. Nyumbani kwako kumuua ni sehemu ya kuokoa uhai wako.
 
Nyoka kamuuma paka anakukufa. 🙄

Then kamuuma mwanafunzi na hajakufa.😇

Ebu nyorosha maelezo mkuu, otherwise mnaweza mwagia mafuta ya taa ama diesel kuzunguka maeneo ambayo mnahisi huyo mgeni anaonekana.

Ama, nashauri mchome moto eneo linalo zunguka hiyo nyumba na hata ikiwezekana hayo maua mengi myateketeze kwa moto.
Hofu ni kitu mbaya sana
Nyoka aligonga kiatu cha mwanafunzi.
 
Nyoka kamuuma paka anakukufa. 🙄

Then kamuuma mwanafunzi na hajakufa.😇

Ebu nyorosha maelezo mkuu, otherwise mnaweza mwagia mafuta ya taa ama diesel kuzunguka maeneo ambayo mnahisi huyo mgeni anaonekana.

Ama, nashauri mchome moto eneo linalo zunguka hiyo nyumba na hata ikiwezekana hayo maua mengi myateketeze kwa moto.
Hofu ni kitu mbaya sana
Aligonga kwenye kiatu wakati wanapita Kwenye nyasi(kwa maelezo yao), ndio wakashtuka wakakimbia kuja kusema, alivyoangaliwa hakua na kovu lolote.
 
Sidhani kama ni kweli, mimi nilichoma juzi baada ya kuona nyoka chooni kwangu ila hakutoka hadi leo vinginevyo iwe alifia humo baada ya kuchoma maana hakuonekana kabisa.
Tuliitumia hii njia tulipokua wadogo, nyumba yetu ilizungukwa na shamba, nyoka walitutembelea sana hasa siku za mvua.

Mama alikua anaomba vipande vya ma tyre garage na tulichoma kila siku jioni. Tulisahau habari ya kupishana na nyoka ndani.
 
Nyoka kamuuma paka anakukufa. 🙄

Then kamuuma mwanafunzi na hajakufa.😇

Ebu nyorosha maelezo mkuu, otherwise mnaweza mwagia mafuta ya taa ama diesel kuzunguka maeneo ambayo mnahisi huyo mgeni anaonekana.

Ama, nashauri mchome moto eneo linalo zunguka hiyo nyumba na hata ikiwezekana hayo maua mengi myateketeze kwa moto.
Hofu ni kitu mbaya sana
Sumu huua kulingana na uzito, nyoka wanaoua tembo ni wachache sana ukiringanisha na binadam, na wanaua binadam ni wachache sana kuringanisha na panya
 
Back
Top Bottom