Pantomath
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 842
- 3,449
Msaada, kuna jirani yangu Kaingiliwa na nyoka mazingira ya nyumbani kwake, huyu nyoka ana week tangu aonekane mara ya kwanza, ila upo uwezekano ni zaidi ya week maana kabla ya hapo ilikua inatokea tu kuku kapotea, kelele za kuku bandani, usumbufu dirishani akiwa amelala n.k n.k.
Baada ya muda ndio akaonekana live. Kumtafuta imekua changamoto kwanza ni kwa mashaka maana yaweza kua naye anakutafuta au mshtukiziane akuwahi.
Na inaonesha ni mkali na ana sumu mbaya, Juzi paka wake alikua naye ndani, ile anatoka tuu nje paka akapiga kelele kutoka anamkuta paka ndio anakaukia, chini ya dk akawa tayari kafa.
Japo inaonekana alimjeruhi, maana mdomoni alikua na damu na ngozi.
Imebidi ahamishe watoto huku, hawakai tena pale. Mwenyewe anaenda kwa machale.
Nyumbani kwake kuna maua mengi sanaa yale yanayotanda mpaka ukutani, bustani ya mboga, kama mita 50 hivi kuna kijimto na nyasi nyingi, tumepatana leo tupulize ile dawa ya kuua mimea.
Kuna uwezekano anakuja na kuondoka, na si mara ya kwanza kuonekana maeneo ya nje, wanafunzi washamuona sana Kwa maelezo yao ashawahi mgonga mmoja wao kwenye kiatu.
Huyu ndugu tunamsaidiaje?
Jana kakutana na michirizi nje, akaishia nje.
Juzi katika kumsaka tukaambulia gamba tukasepa.
Mara anoe maua yanacheza au kuanguka.
Hakuna njia yoyote zaidi ya kumuua, ila njia gani sasa?
Naomba imani za kishirikina uwe ushauri wa mwisho.