Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Pia amwage mbolea ya chumvichumvi.
Ila wawe makini, wasije wakamuua halafu wakaonekana kuwa wamemuua, maana nyoka ni nyara ya serikali kwa mujibu wa Kigwangara, au kama watamuua basi wasiwe na itikadi ya upinzani
🤣
 
Nyoka anayeweza kuzurura eneo moja kuwinda ni ambaye anaona ana nguvu za kulihimili windo kwa hapo means ilitakiwa chatu ndiye awe anazunguka zunguka kwa kuona ana uwezo wa kuhimili mikiki mikiki.

Lakini chatu hana sumu.

Na pia umeng'enyaji wa nyoka ni wa taratibu yaani umeonyesha hana interval ya kuzunguka zunguka hapo home. Kwa umeng'enyaji wa nyoka ilitakiwa ichukue muda kutoka tangu kuku aliwe mpaka yeye kurudi tena.

Lakini huyu anaenda na kurudi na haoni noma mi naona hiyo mimea ondoeni, fanya kila ushauri uliogewa humu nilipo siku hizi imekua kawaida kukutana na kuwaona kiukweli nyoka wanatishia amani pole sana mkuu.

Natumaini utamaliza hii ishu mapema.
 
Hapo sawa! Maana nyoka kwa paka hua anapigwa,zile kucha akimparua hua ni burudani sana ukiona huo ugomvi!
Unaamini kwamba paka yuko faster na ana agility kubwa kumzidi nyoka?
 
Siyo nyegere tu mnyama yeyote ambaye atadevelope kinga ya nyoka hatokufa.

Nyegere amedevelope kinga kwa nyoka waliomzunguka maeneo yake ikatokea ameenda eneo jipya akakutana na aina mpya akigongwa anaweza akafa au akazima kidogo mpaka mwili wake utakapodevelope kinga mpya dhidi ya huyo nyoka.

Kuna binadamu hafi akigongwa na koboko na wote tunakubaliana kwamba koboko ana sumu kali.
Elzea hapo kwa binadamu
 
ni maeneo gani huko ili tujue aina ya nyoka??!!ukishajua ni aina gani ya nyoka na tabia zake itakuwa rahisi kumnasa.
kingine huwez kuchoma kila siku chupa za plastic cjui pilipili au kumwaga vitunguu maji sababu atakimbia then atarudi hali ikitulia!
taja eneo ulipo nikwambie ni aina gani hiyo ya nyoka wanapatikana hapo haswa wenye sumu!!
je ameweza kumeza kuku?au paka?
usije ukamuua bure kumbe alikuwa anasaidia kukupunguzia panya humo ndani!
inaonyesha toka dunia imeumbwa binadamu ameua nyoka mara 5000 kuliko nyoka kuua binadamu hata mmoja..
 
Wakuu unavyochoma tyre kinachomfukuza nyoka ni moshi, harufu ya moshi au moto?
 
Nyoka kamuuma paka anakukufa...🙄
Then kamuuma mwanafunzi na hajakufa..😇
Ebu nyorosha maelezo mkuu, otherwise mnaweza mwagia mafuta ya taa ama diesel kuzunguka maeneo ambayo mnahisi huyo mgeni anaonekana.
Ama, nashauri mchome moto eneo linalo zunguka hiyo nyumba na hata ikiwezekana hayo maua mengi myateketeze kwa moto.
Hofu ni kitu mbaya sana
Amegonga kiatu cha mwanafunzi sio kuuma mwanafunzi
 
Navyoogopa
emoji216.png


Eeh Mungu naomba nisije kutana nae

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app

Dah, hii thread yenyewe kuisoma naisoma kwa mashaka mashaka sana.

Mwili unasisimka.
🤣
 
Kuna vingi vya kuviconsider hapo.

Afya ya mtu. Umri. Eneo la mwili lililogongwa n.k.

Kuna kesi ya mwanamke aliyeng'atwa na black mamba zaidi ya wawili na bado akapona. Na black mamba mmoja anagonga zaidi ya mara moja so zaidi ya wawili wanagonga mara nyingi nyingi na mwanamke aliishi.
Wanawake sio watu
 
Elzea hapo kwa binadamu
Yaani ni kama mtu akiumwa surua mwili unatengeneza kinga baadaye hautaumwa tena.

Hivyo huyu jamaa alikua anajing'atisha koboko kila siku mpaka amekua na kinga ya sumu ya koboko.
 
Msaada, kuna jirani yangu Kaingiliwa na nyoka mazingira ya nyumbani kwake, huyu nyoka ana week tangu aonekane mara ya kwanza, ila upo uwezekano ni zaidi ya week maana kabla ya hapo ilikua inatokea tuu kuku kapotea, kelele za kuku bandani, usumbufu dirishani akiwa amelala n.k n.k....

Baada ya mda ndio akaonekana live,
Kumtafuta imekua changamoto kwanza ni kwa mashaka maana yaweza kua naye anakutafuta au mshtukiziane akuwahi...

Na inaonesha ni mkali na ana sumu mbaya, Juzi paka wake alikua naye ndani, ile anatoka tuu nje paka akapiga kelele kutoka anamkuta paka ndio anakaukia, chini ya dk akawa Tayari kafa,
Japo inaonekana alimjeruhi, maana mdomoni alikua na damu na ngozi.

Imebidi ahamishe watoto huku, hawakai tena pale.
Mwenyewe anaenda kwa machale,

Nyumbani kwake kuna maua mengi sanaa yale yanayotanda mpaka ukutani, bustani ya mboga, kama mita 50 hivi kuna kijimto na nyasi nyingi,, tumepatana leo tupulize ile dawa ya kuua mimea..

kuna uwezekano anakuja na kuondoka, na si mara ya kwanza kuonekana maeneo ya nje, wanafunzi washamuona sana Kwa maelezo yao ashawahi mgonga mmoja wao kwenye kiatu..

Huyu ndugu tunamsaidiaje????
Jana kakutana na michirizi njee, akaishia nje..
Juzi katika kumsaka tukaambulia gamba tukasepa.
Mara anoe maua yanacheza au kuanguka..

Hakuna njia yyt zaidi ya kumuua, ila njia gani sasa?
Naomba imani za kishirikina uwe ushauri wa mwisho.
Tafuta msukuma yeyote atakusaidia
 
Tulipi hamia nyumba mpya enzi zile viwanja vingine vilikuwa bado havijajengwa kulikuwa na nyoka sana. Tulichukua chupa za plastiki zili za soda tunajaza maji robo tatu na mafuta ya taa.Tunatoboa kwenye kila chupa na kuzichimbia chini mdomo ukiwa juu, nyoka hawakusogea mpk watu wakajaa.
 
Paka yupo fasta ila inategema na Weight ya nyoka kwa maelezo ya jamaa inaonesha uyo nyoka ni mbavu na sio falafala
Ni kweli kabisa na kama mpaka paka kafa inamaanisha nyoka ana sumu na mkubwa kuzidi futi 5. Ama la paka ni mdogo
 
Tulipi hamia nyumba mpya enzi zile viwanja vingine vilikuwa bado havijajengwa kulikuwa na nyoka sana. Tulichukua chupa za plastiki zili za soda tunajaza maji robo tatu na mafuta ya taa.Tunatoboa kwenye kila chupa na kuzichimbia chini mdomo ukiwa juu, nyoka hawakusogea mpk watu wakajaa.
Mnatoboa kwenye kifuniko cha mdomo au pembeni ya chupa?
 
Back
Top Bottom