Jana usiku Kama saa 6 nimeishiwa bando nilikuwa nafuatilia live fainali ya Europa Sasa kufika hatua za penati bqndo likaisha ikabidi nitoke nikaulizie matokeo Sasa ile narudi nikaona paka wawili Kama wanapigana na kimtindo palikuwa Giza.
Ile nakaribia nikagundua hawapigani Kama wanacheza na kitu ikanibidi nipakaribie kuangalia vzr wanacheza na kitu gani
Ase kumbe nyoka walikuwa wanacheza nae huku wakimpiga makofi na kuruka sasa wkt nimewasha tochi ya simu kumulika niangalie vzr wale paka wakakimbia na ndio walikuwa kizuizi wa yule nyoka
Ikanibidi nichukue jukumu la kuokota mawe na kumpiga yule nyoka ,Sasa kwenye ile nyumba kwa dirishani nasikia vijana mabishoo wa chuo bila Shaka wale wanabishana kuhusu mpira ,nikawa nawaita waje kusaidia maana yule nyoka alikuwa anataka kuingia kwenye tobo pale kwao walivyo wajinga wakawa wananiona chizi sijui wakakaa kimya na kuacha kubishana nikaendelea kuwaita wakajikausha
Nikajisemea kwanza sio kwangu najihangaisha bure wacha aingie ndani kwao watajijua wenyewe na ubisho wao,nikazima tochi nikasepa zangu, na nyoka alikuwa mrefu kweli
Paka wanasaidia ase nimegundua Jana night