Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Achome miba ya samaki ataibuka tu
 
Aliuma kiatu cha mwanafunzi ina maana hakuifikia ngozi ya mwanafunzi
 
Pia amwage mbolea ya chumvichumvi.

Ila wawe makini, wasije wakamuua halafu wakaonekana kuwa wamemuua, maana nyoka ni nyara ya serikali kwa mujibu wa Kigwangara, au kama watamuua basi wasiwe na itikadi ya upinzani.
Achana na kigwangala mpuuzi yule 😃
 
Ajikaze achukue jiko lenye moto aweke ndani achome pilipili ya unga kama wanavyochoma ubani au achome mataili moshi uweze kuingia ndani au kama kina uwezekano amwage mafuta ya diesel au petrol lazima atahama huyo nyoka.
 
Sidhani kama ni kweli, mimi nilichoma juzi baada ya kuona nyoka chooni kwangu ila hakutoka hadi leo vinginevyo iwe alifia humo baada ya kuchoma maana hakuonekana kabisa.
Chooni sehemu gani?!
 
Mkuu unataka kumfukuza au kumuua kabisa?
Kama unataka kumfukuza njia zilizo shauriwa na wengi zitiumike yaani kumwaga oil chafu na mafuta ya taa kuzunguka eneo lote la nyumba. Ndani choma viwanda vya mpira pamoja na pilipili ila njia hii haitkupa amani kwakuwa anaweza kutoka akakimbia usimuone alafu ukawa unaendelea kuhofia kuwa yupo.

Toa taarifa idara ya wanyamapori waje wamsake nyoka wao huko kuna wataalamu wa nyoka hata wakiona mchirizi wanajua aina ya nyoka.

Kama unaweza ukapata wadudu wadogo kama panya wanaitwa nguchiro hawa watamsaka mpaka wamkate kichwa ndio wanaridhika, walipo hawa nyoka hawezi kuishi.

Tafuta sangara wapandikize hapo kwako, sangara ni wadudu wadogo kama siafu. Hawa walipo ni usumbufu tosha kwa nyoka lazima akimbie.
Hii njia ya sangara alituma mkoloni mmoja aliekuwa anamiliki mashamba makubwa ya karanga huko wilayani Nachingwea. Huyu mkoloni aliitwa John Mollam, aliamua kwenda Kwenye misitu huko Australia kutafuta nyoka ili akawapandikize kwenye mashamba ya karanga kwalengo la kudhibiti panya, baada ya nyoka kustawi na kuwa tishio wakamshinda akaenda kutafuta hawa siafu sangara ili kudhibiti nyoka na alifanikiwa kwani nyoka walikimbilia maeneo ya misitu na mlimani kukwepa sangara.
 
Mkuu Kwanza tulia,chukua lita ya petroli,changanya na disel lita moja na mafuta taa ya jero,spray vyumbani Kwanza,kaa siku mbili au tatu ili Kama yuko ndani atoke afu pulizia nje kwenye majani. Hii ikishindikana jua ni mkono wa mtu ambao ni lazima uondolewe kwa maombi au mtu vilevile. UKIFANYA HIVI,NIAMBIE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…