Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Msaada, kuna jirani yangu Kaingiliwa na nyoka mazingira ya nyumbani kwake, huyu nyoka ana week tangu aonekane mara ya kwanza, ila upo uwezekano ni zaidi ya week maana kabla ya hapo ilikua inatokea tu kuku kapotea, kelele za kuku bandani, usumbufu dirishani akiwa amelala n.k n.k.

Baada ya muda ndio akaonekana live. Kumtafuta imekua changamoto kwanza ni kwa mashaka maana yaweza kua naye anakutafuta au mshtukiziane akuwahi.

Na inaonesha ni mkali na ana sumu mbaya, Juzi paka wake alikua naye ndani, ile anatoka tuu nje paka akapiga kelele kutoka anamkuta paka ndio anakaukia, chini ya dk akawa tayari kafa.

Japo inaonekana alimjeruhi, maana mdomoni alikua na damu na ngozi.

Imebidi ahamishe watoto huku, hawakai tena pale. Mwenyewe anaenda kwa machale.

Nyumbani kwake kuna maua mengi sanaa yale yanayotanda mpaka ukutani, bustani ya mboga, kama mita 50 hivi kuna kijimto na nyasi nyingi, tumepatana leo tupulize ile dawa ya kuua mimea.

Kuna uwezekano anakuja na kuondoka, na si mara ya kwanza kuonekana maeneo ya nje, wanafunzi washamuona sana Kwa maelezo yao ashawahi mgonga mmoja wao kwenye kiatu.

Huyu ndugu tunamsaidiaje?
Jana kakutana na michirizi nje, akaishia nje.
Juzi katika kumsaka tukaambulia gamba tukasepa.
Mara anoe maua yanacheza au kuanguka.

Hakuna njia yoyote zaidi ya kumuua, ila njia gani sasa?

Naomba imani za kishirikina uwe ushauri wa mwisho.
Ipo dawa ya kupulizakama fammigation.. itamtoa mafichoni
 
Nyoka kwa kuku hasogei labda wa kizungu, kuku anaua nyoka! Choma Tyre mwaga disel. Mmefanya kosa kubwa kuhama mmempa utulivu na nafasi ya kutafuta makazi yake vizuri.
Labda awe nyoka mdogo kiumri ila aliyekomaa kuku anafyekwa kabisa. Akiingia kwenye banda kama kuku ni wengi hapo labda ndo wanaweza kumuua na hapo ameshafyeka kadhaa na mara huwa wanapiga kelele na kukimbia na si kushambulia. Nyoka ni kiumbe chenye akili sana hauwawi kizembe.
 
Mbolea ya
Kweli kabisa...watoke humo ndani, hii inapalia, wanunue pilipili kavu, wazichome humo, wenye jiko la mkaa au chetezo.

Nje machine matairi, lakini wakimwaga urea, kwenye majani na maua, watambamba tu.

Everyday is Saturday 😎
Mbolea ya chumvi inazuiaje snake
 
Nashauri wakuu msiue nyoka. Ni moja ya viumbe wanaosaidia kutuepusha na magonjwa na uharibifu wa mali na mazao.

Ni pest controllers.

Pia sio kila nyoka ana sumu kuna wengine ni nyoka wa nyumbani tu (house snakes) hawana madhara. Kama unamjua unaweza kumkamata na ukamtoa nje ya nyumba (uwe na uhakika 100% lakini).

Kama huna uhakika au kama unajua ni nyoka sumu jaribu kuwasiliana na maliasili walipo karibu watakuja kumtoa.

Haya maisha ya ki-CCM napata wapi muda wa kuanza kukaguana na nyoka ili nijue ni poisonous or non poisonous?tukigumiana ni rungu la kichwa tu alikuwa wa sumu hakuwa wa sumu atajijua mwenyewe kwani nilimuita?
 
Huwa najiuliza kwann Mungu alimuumba nyoka,siwapendi iwe live au kwenye picha hata kula sitoweza hasa nyama au samaki siku hio nahisi nakula nyoka ishajengeka hivyo kwenye brain yangu ngumu kutoka
 
Msaada, kuna jirani yangu Kaingiliwa na nyoka mazingira ya nyumbani kwake, huyu nyoka ana week tangu aonekane mara ya kwanza, ila upo uwezekano ni zaidi ya week maana kabla ya hapo ilikua inatokea tu kuku kapotea, kelele za kuku bandani, usumbufu dirishani akiwa amelala n.k n.k.

Baada ya muda ndio akaonekana live. Kumtafuta imekua changamoto kwanza ni kwa mashaka maana yaweza kua naye anakutafuta au mshtukiziane akuwahi.

Na inaonesha ni mkali na ana sumu mbaya, Juzi paka wake alikua naye ndani, ile anatoka tuu nje paka akapiga kelele kutoka anamkuta paka ndio anakaukia, chini ya dk akawa tayari kafa.

Japo inaonekana alimjeruhi, maana mdomoni alikua na damu na ngozi.

Imebidi ahamishe watoto huku, hawakai tena pale. Mwenyewe anaenda kwa machale.

Nyumbani kwake kuna maua mengi sanaa yale yanayotanda mpaka ukutani, bustani ya mboga, kama mita 50 hivi kuna kijimto na nyasi nyingi, tumepatana leo tupulize ile dawa ya kuua mimea.

Kuna uwezekano anakuja na kuondoka, na si mara ya kwanza kuonekana maeneo ya nje, wanafunzi washamuona sana Kwa maelezo yao ashawahi mgonga mmoja wao kwenye kiatu.

Huyu ndugu tunamsaidiaje?
Jana kakutana na michirizi nje, akaishia nje.
Juzi katika kumsaka tukaambulia gamba tukasepa.
Mara anoe maua yanacheza au kuanguka.

Hakuna njia yoyote zaidi ya kumuua, ila njia gani sasa?

Naomba imani za kishirikina uwe ushauri wa mwisho.
Nasubiri wamalize kukushauri nikupe USHAURI WA MWISHO.
 
Nyoka kamuuma paka anakukufa. 🙄

Then kamuuma mwanafunzi na hajakufa.😇

Ebu nyorosha maelezo mkuu, otherwise mnaweza mwagia mafuta ya taa ama diesel kuzunguka maeneo ambayo mnahisi huyo mgeni anaonekana.

Ama, nashauri mchome moto eneo linalo zunguka hiyo nyumba na hata ikiwezekana hayo maua mengi myateketeze kwa moto.
Hofu ni kitu mbaya sana
Soma vizuri .kamgonga kwenye kiatu
 
Umekuja na maelezo kidogo sana.

Edit uzi andika upo eneo gani tujue ni aina gani
 
Nyoka kamuuma paka anakukufa. [emoji849]

Then kamuuma mwanafunzi na hajakufa.[emoji56]

Ebu nyorosha maelezo mkuu, otherwise mnaweza mwagia mafuta ya taa ama diesel kuzunguka maeneo ambayo mnahisi huyo mgeni anaonekana.

Ama, nashauri mchome moto eneo linalo zunguka hiyo nyumba na hata ikiwezekana hayo maua mengi myateketeze kwa moto.
Hofu ni kitu mbaya sana
Mwanafunzi ameng'atwa kwa kiatu yaani kiatu ndo kilicuong'atwa
 
Jana usiku Kama saa 6 nimeishiwa bando nilikuwa nafuatilia live fainali ya Europa Sasa kufika hatua za penati bqndo likaisha ikabidi nitoke nikaulizie matokeo Sasa ile narudi nikaona paka wawili Kama wanapigana na kimtindo palikuwa Giza.

Ile nakaribia nikagundua hawapigani Kama wanacheza na kitu ikanibidi nipakaribie kuangalia vzr wanacheza na kitu gani

Ase kumbe nyoka walikuwa wanacheza nae huku wakimpiga makofi na kuruka sasa wkt nimewasha tochi ya simu kumulika niangalie vzr wale paka wakakimbia na ndio walikuwa kizuizi wa yule nyoka

Ikanibidi nichukue jukumu la kuokota mawe na kumpiga yule nyoka ,Sasa kwenye ile nyumba kwa dirishani nasikia vijana mabishoo wa chuo bila Shaka wale wanabishana kuhusu mpira ,nikawa nawaita waje kusaidia maana yule nyoka alikuwa anataka kuingia kwenye tobo pale kwao walivyo wajinga wakawa wananiona chizi sijui wakakaa kimya na kuacha kubishana nikaendelea kuwaita wakajikausha

Nikajisemea kwanza sio kwangu najihangaisha bure wacha aingie ndani kwao watajijua wenyewe na ubisho wao,nikazima tochi nikasepa zangu, na nyoka alikuwa mrefu kweli

Paka wanasaidia ase nimegundua Jana night
[emoji3][emoji3][emoji3]we jamaa
 
Nyoka kama kashajeruhiwa lazima afe ni swala la muda tu...vita ya paka na nyoka ni ndefu kama mlikuwa karibu lazima mngeishuhudia tu.
 
Back
Top Bottom