Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Msaada, kuna jirani yangu Kaingiliwa na nyoka mazingira ya nyumbani kwake, huyu nyoka ana week tangu aonekane mara ya kwanza, ila upo uwezekano ni zaidi ya week maana kabla ya hapo ilikua inatokea tu kuku kapotea, kelele za kuku bandani, usumbufu dirishani akiwa amelala n.k n.k.

Baada ya muda ndio akaonekana live. Kumtafuta imekua changamoto kwanza ni kwa mashaka maana yaweza kua naye anakutafuta au mshtukiziane akuwahi.

Na inaonesha ni mkali na ana sumu mbaya, Juzi paka wake alikua naye ndani, ile anatoka tuu nje paka akapiga kelele kutoka anamkuta paka ndio anakaukia, chini ya dk akawa tayari kafa.

Japo inaonekana alimjeruhi, maana mdomoni alikua na damu na ngozi.

Imebidi ahamishe watoto huku, hawakai tena pale. Mwenyewe anaenda kwa machale.

Nyumbani kwake kuna maua mengi sanaa yale yanayotanda mpaka ukutani, bustani ya mboga, kama mita 50 hivi kuna kijimto na nyasi nyingi, tumepatana leo tupulize ile dawa ya kuua mimea.

Kuna uwezekano anakuja na kuondoka, na si mara ya kwanza kuonekana maeneo ya nje, wanafunzi washamuona sana Kwa maelezo yao ashawahi mgonga mmoja wao kwenye kiatu.

Huyu ndugu tunamsaidiaje?
Jana kakutana na michirizi nje, akaishia nje.
Juzi katika kumsaka tukaambulia gamba tukasepa.
Mara anoe maua yanacheza au kuanguka.

Hakuna njia yoyote zaidi ya kumuua, ila njia gani sasa?

Naomba imani za kishirikina uwe ushauri wa mwisho.
Kwanza poleni kwa majaribu kisha ondoeni hofu,huyo nyoka atakufa mwenyewe ndani ya siku zisizozidi tano, amini usiamini nyoka hawezi kuishi na jeraha na kwakua alishajeruhiwa na Paka na akanyofolewa ngozi mpaka kutokwa na damu basi hana maisha tena huyo. Jiandaeni kuokota mzoga.
 
Nyoka kwa kuku hasogei labda wa kizungu, kuku anaua nyoka! Choma Tyre mwaga disel. Mmefanya kosa kubwa kuhama mmempa utulivu na nafasi ya kutafuta makazi yake vizuri.
Inategemeana na ukubwa wa nyoka mwenyewe, siyo kila nyoka ni Mnyenge kwa nyoka.
 
tafuta oil chafu au mafuta ya taa mwaga au nenda duka la madawa ya mifugo na wanyama,kuna dawa zenye asili ya baruti yenye unga ukimwaga nyoka hasogei anaungua tumbo
 
Nashauri wakuu msiue nyoka. Ni moja ya viumbe wanaosaidia kutuepusha na magonjwa na uharibifu wa mali na mazao.

Ni pest controllers.

Pia sio kila nyoka ana sumu kuna wengine ni nyoka wa nyumbani tu (house snakes) hawana madhara. Kama unamjua unaweza kumkamata na ukamtoa nje ya nyumba (uwe na uhakika 100% lakini).

Kama huna uhakika au kama unajua ni nyoka sumu jaribu kuwasiliana na maliasili walipo karibu watakuja kumtoa.
 
Msaada, kuna jirani yangu Kaingiliwa na nyoka mazingira ya nyumbani kwake, huyu nyoka ana week tangu aonekane mara ya kwanza, ila upo uwezekano ni zaidi ya week maana kabla ya hapo ilikua inatokea tu kuku kapotea, kelele za kuku bandani, usumbufu dirishani akiwa amelala n.k n.k.

Baada ya muda ndio akaonekana live. Kumtafuta imekua changamoto kwanza ni kwa mashaka maana yaweza kua naye anakutafuta au mshtukiziane akuwahi.

Na inaonesha ni mkali na ana sumu mbaya, Juzi paka wake alikua naye ndani, ile anatoka tuu nje paka akapiga kelele kutoka anamkuta paka ndio anakaukia, chini ya dk akawa tayari kafa.

Japo inaonekana alimjeruhi, maana mdomoni alikua na damu na ngozi.

Imebidi ahamishe watoto huku, hawakai tena pale. Mwenyewe anaenda kwa machale.

Nyumbani kwake kuna maua mengi sanaa yale yanayotanda mpaka ukutani, bustani ya mboga, kama mita 50 hivi kuna kijimto na nyasi nyingi, tumepatana leo tupulize ile dawa ya kuua mimea.

Kuna uwezekano anakuja na kuondoka, na si mara ya kwanza kuonekana maeneo ya nje, wanafunzi washamuona sana Kwa maelezo yao ashawahi mgonga mmoja wao kwenye kiatu.

Huyu ndugu tunamsaidiaje?
Jana kakutana na michirizi nje, akaishia nje.
Juzi katika kumsaka tukaambulia gamba tukasepa.
Mara anoe maua yanacheza au kuanguka.

Hakuna njia yoyote zaidi ya kumuua, ila njia gani sasa?

Naomba imani za kishirikina uwe ushauri wa mwisho.
Watu wengi wanaokaa porini wanasema ukitaka kuuwa na kufukuza nyoka kwenye mazingira yako, tumia mafuta ya samuli, zungusha eneo husika akipita hapo anakatika vipande vipande, au weka mafuta ya samuli kwenye taili washa Moto hile harufu inaenda mbali sana na nyoka watasogea mbali sana.
 
Nyoka kamuuma paka anakukufa. [emoji849]

Then kamuuma mwanafunzi na hajakufa.[emoji56]

Ebu nyorosha maelezo mkuu, otherwise mnaweza mwagia mafuta ya taa ama diesel kuzunguka maeneo ambayo mnahisi huyo mgeni anaonekana.

Ama, nashauri mchome moto eneo linalo zunguka hiyo nyumba na hata ikiwezekana hayo maua mengi myateketeze kwa moto.
Hofu ni kitu mbaya sana

Ukisoma ili ukosoe ndo kinachotokea hiki.mtoto aligongwa kwenye kiatu
 
Nyoka wahaina gan? mwambie ande kwenye maduka ya asili anunue dawa inaitwa kibiliti upele af haichome harufu yake inafukuza wadudu
 
Kama ni black mamba mtaimba kazi mnayo nyoka hatar sana yule akiku ng'ata akwepeshi
 
Back
Top Bottom