Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Tuliitumia hii njia tulipokua wadogo, nyumba yetu ilizungukwa na shamba, nyoka walitutembelea sana hasa siku za mvua.

Mama alikua anaomba bips de vya ma tyre garage na tulichoma kila siku jioni. Tulisahau habari ya kupishana na nyoka ndani.
Ngoja niendelee kuchoma pia labda alikimbia sikumwona tu
 
Mkuu tafuta dizel mwaga kwa kuzunguka nyumba na kama hayo maua huyataki yamwagie pia mwenyewe atatoka tu maana nyoka na mafuta hawaelewani
 
Nyoka hua hawezi kumuua paka
 
Ukubwa wa umbo la mnyama hutathmini uwezo wa sumu kusambaa mwilini.

Mnyama mwenye umbo dogo maana yake moyo utasukuma damu haraka haraka hivyo kurahisisha usambazaji.

Paka atawahi kufa kuliko binadamu.

Lakini binadamu atawahi kufa kuliko tembo.
 
Usiumize kichwa sana,katafute oil chafu, mwaga maeneo yote unayohisi zinawezakuwa maskaji zake na huko kwenye kuku.

Nimekwambia oil chafu, sababu ni ngumu kiasi kupotea, ila mafuta ya taa na petrol zinakimbia upesi.
 
Ukubwa wa umbo la mnyama hutathmini uwezo wa sumu kusambaa mwilini.

Mnyama mwenye umbo dogo maana yake moyo utasukuma damu haraka haraka hivyo kurahisisha usambazaji.

Paka atawahi kufa kuliko binadamu.

Lakini binadamu atawahi kufa kuliko tembo.
Kuna kenge na nyegere hawafi.
 
Hapa maana yake ata mtu mfupi mwenye umbo dogo atakufa haraka na mwenye umbo kubwa mrefu atachelewa au kutokufa kabisa...
 
Kuna kenge na nyegere hawafi.
Siyo nyegere tu mnyama yeyote ambaye atadevelope kinga ya nyoka hatokufa.

Nyegere amedevelope kinga kwa nyoka waliomzunguka maeneo yake ikatokea ameenda eneo jipya akakutana na aina mpya akigongwa anaweza akafa au akazima kidogo mpaka mwili wake utakapodevelope kinga mpya dhidi ya huyo nyoka.

Kuna binadamu hafi akigongwa na koboko na wote tunakubaliana kwamba koboko ana sumu kali.
 
Mkuu poleni sana,lakini nyoka hua anapigwa na paka! Sasa sijui inakuaje,Nyoka amuue paka! Anyway dawa ya nyoka ni kumwaga mafuta ya taa au diesel au chomeni mataili!
Inawezekana paka alileta ubabe akazidiwa na kukimbia baadae alisahau alirudi kulala na paka walivyo wavivu, mwamba akamgonga akiwa usingizini.
 
Paka hauawi na nyoka(fact)....
Ok dawA kiboko ni oil chafu changanya na mafuta ya taa au diesel mwaga mwaga maeneo tarajiwa harafu endeleeni na shughuli zenu hapo hakai na kama atakaa basi ndan ya nusu saa mtamkuta vipande vipande
 
Safisha maeneo yote kuzunguka nyumba ikiwemo kung'oa maua yote na hata hiyo bustani.
Fagia kabisa pawe peupe.
Atacha mwenyewe kuja.
 
Hapa maana yake ata mtu mfupi mwenye umbo dogo atakufa haraka na mwenye umbo kubwa mrefu atachelewa au kutokufa kabisa...
Kuna vingi vya kuviconsider hapo.

Afya ya mtu. Umri. Eneo la mwili lililogongwa n.k.

Kuna kesi ya mwanamke aliyeng'atwa na black mamba zaidi ya wawili na bado akapona. Na black mamba mmoja anagonga zaidi ya mara moja so zaidi ya wawili wanagonga mara nyingi nyingi na mwanamke aliishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…