Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

...Katakakata vitunguu saumu na vitunguu maji kishwa vitowe nje sehemu mbali mbali za nyumba...kama yupo ndani atatoka tu! Uwe tu tayari...
huyu kweli ni nyoka huyuhuyu tunaemjua au ni mengine
 
Mkuu unataka kumfukuza au kumuua kabisa?
Kama unataka kumfukuza njia zilizo shauriwa na wengi zitiumike yaani kumwaga oil chafu na mafuta ya taa kuzunguka eneo lote la nyumba. Ndani choma viwanda vya mpira pamoja na pilipili ila njia hii haitkupa amani kwakuwa anaweza kutoka akakimbia usimuone alafu ukawa unaendelea kuhofia kuwa yupo.

Toa taarifa idara ya wanyamapori waje wamsake nyoka wao huko kuna wataalamu wa nyoka hata wakiona mchirizi wanajua aina ya nyoka.

Kama unaweza ukapata wadudu wadogo kama panya wanaitwa nguchiro hawa watamsaka mpaka wamkate kichwa ndio wanaridhika, walipo hawa nyoka hawezi kuishi.

Tafuta sangara wapandikize hapo kwako, sangara ni wadudu wadogo kama siafu. Hawa walipo ni usumbufu tosha kwa nyoka lazima akimbie.
Hii njia ya sangara alituma mkoloni mmoja aliekuwa anamiliki mashamba makubwa ya karanga huko wilayani Nachingwea. Huyu mkoloni aliitwa John Mollam, aliamua kwenda Kwenye misitu huko Australia kutafuta nyoka ili akawapandikize kwenye mashamba ya karanga kwalengo la kudhibiti panya, baada ya nyoka kustawi na kuwa tishio wakamshinda akaenda kutafuta hawa siafu sangara ili kudhibiti nyoka na alifanikiwa kwani nyoka walikimbilia maeneo ya misitu na mlimani kukwepa sangara.
ukiwabeba unawaweka kwenye chombo gani
 
Uwe makini inawezekana anamtafuta mkewe/mumewe,hivyo oil chafu mwaga sana maeneo ya milangoni nk ,au mlietaimingi ,
 
inategemea na nyoka mkuu, mimi paka wangu aliwahi kuua nyoka nikashangaa anakuja nae anataka kumuingiza kwenye mabanda ya kuku kwa kipindi hicho yalikuwa wazi. nilichofanya ni kumnyang'anya yule nyoka na kwenda kumfukia ila kadri siku silivyokuwa zinasogea paka alizidi kudhoofika nilijaribu kumtibia lkn haikuwezekana akafa ndani ya mwezi mmoja.

kilichoniuma zaidi siku aliyokufa alipata nguvu akaja miguuni kwangu akalala na ndio akaishia hapo.
Daah ulikosea sana ungeacha ale ilikua ndo kinga yake
 
Msaada, kuna jirani yangu Kaingiliwa na nyoka mazingira ya nyumbani kwake, huyu nyoka ana week tangu aonekane mara ya kwanza, ila upo uwezekano ni zaidi ya week maana kabla ya hapo ilikua inatokea tu kuku kapotea, kelele za kuku bandani, usumbufu dirishani akiwa amelala n.k n.k.

Baada ya muda ndio akaonekana live. Kumtafuta imekua changamoto kwanza ni kwa mashaka maana yaweza kua naye anakutafuta au mshtukiziane akuwahi.

Na inaonesha ni mkali na ana sumu mbaya, Juzi paka wake alikua naye ndani, ile anatoka tuu nje paka akapiga kelele kutoka anamkuta paka ndio anakaukia, chini ya dk akawa tayari kafa.

Japo inaonekana alimjeruhi, maana mdomoni alikua na damu na ngozi.

Imebidi ahamishe watoto huku, hawakai tena pale. Mwenyewe anaenda kwa machale.

Nyumbani kwake kuna maua mengi sanaa yale yanayotanda mpaka ukutani, bustani ya mboga, kama mita 50 hivi kuna kijimto na nyasi nyingi, tumepatana leo tupulize ile dawa ya kuua mimea.

Kuna uwezekano anakuja na kuondoka, na si mara ya kwanza kuonekana maeneo ya nje, wanafunzi washamuona sana Kwa maelezo yao ashawahi mgonga mmoja wao kwenye kiatu.

Huyu ndugu tunamsaidiaje?
Jana kakutana na michirizi nje, akaishia nje.
Juzi katika kumsaka tukaambulia gamba tukasepa.
Mara anoe maua yanacheza au kuanguka.

Hakuna njia yoyote zaidi ya kumuua, ila njia gani sasa?

Naomba imani za kishirikina uwe ushauri wa mwisho.
Umeandika kama unawasilisha malalamiko kwa mbunge au diwani, cha kufanya hapo ondoa hayo maua yote pawe safi ndipo umuue
 
Back
Top Bottom